Bana likasi
JF-Expert Member
- Jan 7, 2020
- 6,927
- 6,417
Kate ya utekaji,Maisha kuwa magumu,kusomeshwa namba ccm hawana hoja ya utetezi.Tegemeo lao ni ndege,sgr ,Stella goerge,Ninashauri wapinzani waipe uzito hii hoja ya utekaji wakati wa kampeni, mtu anapaswa akigeuka kulia ni Ben saa nane yuko wapi? Akigeuka kushuto Azory yuko wapi, akigeuka nyuma ni kina nani waliompiga tundu lissu
risasi.
Amin Amin nawaambia, hakuna kete nzito kama hiyo, maana mtakuwa na platform huru ya kuongea bila kuzuiwa. Mnakumbuka 2015 mwigulu alivyokuwa anatembea na bwana yule aliyemwagiwa tindikali? Sasa imagine nyepesi kama ile kwa ccm ndo ilikuwa hoja tegemezi, hili la wapendwa wetu lenye kutia majonzi mazito inapaswa kuwatoa wao chozi la damu kabisa ikibidi. Bila kujali mgombea ni nani hii iwe hoja kuu
Hapo lazima mbichi na mbivu zitajulikana. Msimamo ni ule ule, mtu akiongelea madaraja swali ni wapendwa wetu wako wapi?
Akiongelea ndege swali wasiojulikana tutawajua lini?
Hapo Tutaelewana tu. Ndo kile kipindi mtu atatubu bila kupenda kwa kuona roho za waliopotea zinamuandama kila aendako
Itakuwa vizuri tukawa na picha kubwa za hawa wapendwa wetu zitandazwe kwenye kila mkutano wa kampeni, ikibidi hata katikati ya bendera za vyama wawekwe maana najua polisi hawatakuwa nyuma kupambana nazo.
Nionavyo mimi, hii kete ya utekaji inatosha kumweka pembeni ikijengewa hoja kwa uzito wa kipekee kabisa kama kauli mbiu ya kila mkutano wa kampeni.
Kwa akili ya kibinadamu hii itawapandisha hasira watawala na kujikuta wanashindwa hata kuzungumza sera yeyote kwani kazi yao itakuwa moja tu kujitetea dhidi ya tuhuma.
Kazi kwenu kina Zitto njia nyeupe kabisa hiyo
Sent using Jamii Forums mobile app