Rais Magufuli hajavunja Katiba kumteua CAG mpya, tatizo ni Kiingereza kilichotumika kwenye Katiba

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,431
2,000
Tumpende au tusimpende Rais Magufuli kwenye hili hajakosea wala kuvunja katiba, Kiingereza ni tatizo kwa Watanzania wengi sana.

Maneno ya Kiingereza hutumika kulingana na muktadha au Mazingira husika, Kwa mtu aliyejifunza lugha ya Kiingereza au kuishi huko uingereza na kuongea lugha hii basi hawezi kupingana na tafsiri ya neno "Shall be eligible" kuwa siyo shall be re appointed

Neno "shall" kwenye katiba au sheria ya ukaguzi ni tegemezi, halijasimama lenyewe.

Madhara ya walimu wale wa UPE enzi hizo yaani walimu wa fasta fasta waliomaliza tu darasa la saba na kuamuliwa kufundisha shule za msingi ndio hao wameleta shida hii kwenye neno "shall"

Watu waliaminishwa shall maana yake ni lazima kufanyika, Hawa kuambiwa shall nyuma ya baadhi ya maneno ina tafsiri yake

Mfano. All graduate of Tanzanian local University shall be eligible for government employment, Hii haimaanishi kuwa lazima uajiriwe na serikali, Yawezekana umemaliza chuo Yes na unavigezo Yes lakini hazilazimishi serikali itoe ajira kwako

"Shall be eligible " haimaanishi kuwa ''shall be reappointed''

Hapa Tanzania kila raia zaidi ya miaka 18 shall be eligible to vote, haimaanishi kila mwenye miaka 18 Tanzania lazima apige kura bali anastahili kupiga kura.

CAG Assad alistahili na ana sifa za kuendelea kuwa CAG kwa kipindi cha miaka 5 au mpaka kufikisha umri wa kustaafu, hapa haimaanishi kuwa ni lazima awe CAG hata kama anastahili kipindi kingine cha miaka 5.

Mkataba wa CAG ni miaka mitano tu, siyo mkataba wa miaka kumi, CAG shall be eligible for another term haimaanishi shall be re appointed by president again,

Tutakosoa kwenye ukweli na kupinga kwa hoja, Kwa jambo hili Rais Magufuli hajavunja katiba.

Watu wanaendeshwa kwa hisia eti CAG mpya ni rafiki yake, Rais kwa Katiba yetu ana mamlaka makubwa awepo CAG au asiwepo akiamua kutokaguliwa anaweza kutokaguliwa.

Ripoti ya CAG kuanza kupeleka bungeni ni hisani ya Rais kikwete tu, Hapo awali iliwekwa na kupumzishwa ikulu hiyo Ripoti

Tusitafsiri sheria tofauti, Shall be elegible sio shall be reappointed.

CAG Assad anastahili kwa miaka mitano mingine lakini sio lazima awe yeye, mkataba wake ni miaka mitano na siyo kumi.

Sasa kama Rais ameona kuna mtu mwingine eligible kuna shida gani?

Wanabodi, neno "shall be eligible" lisiwachanganye ni simple English tu.

Assad ana sifa kweli na hajafikisha miaka 60 kweli na anastahili kipindi cha miaka mingine 5 kweli, lakini sio lazima ateuliwe tena.

Shall be eligible haimaanishi shall be reappointed.Povu la chuki kwa Rais linaruhusiwa lakini kwa hili Kiingereza ni tatizo kwa Watanzania wengi.
 
Kidyjr

Member
Mar 18, 2018
15
45
Ni kweli lkn umesahau la sivyo unajitia upofu wa makusudi. Katiba imeweka utaratibu maalamu, endapo kwa namna zilivyoainishwa "zingatia" kikatiba kama Rais aataona kuna sababu ya kutoendelea baada ya hiyo miaka Mitano Naye hajafika umri wa kustaafu! Upo utaratibu wa kumwondoa toka nafasi hiyo.
 
GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,431
2,000
Kaka Unatafsiri Kiingereza kwenda Kiswahili ndio tatizo linalokusumbua.

Shall be eligible to vote not necessarily you have to vote.

Kwenye sheria neno shall be eligible for the next term of five years haimaanishi shall be re appointed.

Acha kutafsiri lugha ya Kiingereza kwa neno moja moja.

Wewe umesoma Kiingereza nchi gani usiyeelewa kutafsiri Kiingereza.

Mtoto mdogo wa shule ya msingi International anakushinda.

Shame upon you
Nikuulize swali jepesi tu, nini tofauti kati ya maneno haya ya kiingereza MAY na SHALL??

Ukinijibu hapo ndipo tutajua kama Rais amevunja Katiba au laa
 
GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,431
2,000
Unatetea ujinga, yeye kashasema kama ana mamlaka ya kuteua basi pia lazima ana mamlaka ya kutengua. Haya kayasema yeye mwenyewe na kamwambia Kichere kuwa anaweza kukaa kwa mwaka mmoja tu akatumbuliwa.
Yes ana uwezo huo pia na anao mkubwa tu
Tume ya maadili anIteua Yeye

Anaweza waambia Tume watoe report kichele hakuwa na maadili TRA ndio maana wafanyabiashara walilalamika

Sasa mamlaka ya Rais yapo kwenye katiba au wewe hukuwepo wakati wa rasmu ya warioba
 
GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,431
2,000
Hakuna cha upofu, Kazi yake ni mkataba wa miaka 5 tu na siyo miaka kumi

Eligibility unafahamu maana yake,

All form 4,student shall be eligible for National form four examination not necessary they must sit for National form 4 examination
Ni kweli lkn umesahau la sivyo unajitia upofu wa makusudi . Katiba imeweka utaratibu maalamu, endapo kwa namna zilivyoainishwa "zingatia" kikatiba kama rais aataona kuna Sababu ya kutoendelea baada ya hiyo miaka Mitano Naye hajafika umri wa kustaafu! Upo utaratibu wa kumwondoa toka nafasi hiyo.
 
GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,431
2,000
Wewe ndio wale mliofundishwa

Matumizi ya shall na will kule kayumba kwenye shule za nyasi

Mwalimu wako alikuambia shall maana yake lazima,

Mwalimu wako alipaswa kukufundisha kiingereza kinatamkwa na kutafsiri wa kwa muktadha maalum

Hivi hao walimu wenu wa shule ya msingi walikuwa wa chuo gani?

Shall be eligible to.......

Bado ana sifa lakini not reappointed
Upumbavu wake aubebe mwenyewe. Kama hata neno shall hajui maana yake, huko nje ataongea Nini? MAGWANGALA IZI NOTI MAKINIKIA
 
REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
3,146
2,000
Kipindi watu wanadai mabadiliko ya katiba hawakuwa wajinga lawama zote hizi ujinga wote huu tunampelekea mh jakaya kikwete kukataa mabadiliko ya katiba

Mh magufuli tutampigia kelele bure katumia udhaifu wa katiba yetu kufanya huu ujinga wanasheria wanapiga kelele tu ila mh rais katumia udhaifu wa katiba katika lugha kufanya huu ujinga

Tukumbuke mwanasheria siyo mtaalamu wa lugha sasa ukienda kwenye taaluma ya kugha hususani kingereza kuna hii kitu

"Linguistic prescription, or prescriptive grammar," hii kwa lugha nyepesi tunaweza isema ni kanuni ambayo inaonyesha matumizi sahihi ya lugha katika vipengele vya uandishi, utamkaji, misamiati, maana ya maneno, na muundo wa sentensi katika lugha😀😀😀😀

Wataalamu wa lugha mnajua kingereza kinachotumika kwenye sheria na biblia ni kingereza kipi middle English, siyo modern English na ndio maana vigum mtu asiye mwanasheriakusoma judgment ya mahakama akaielewa au mtu ambaye ajasoma Bible knowledge akachukua biblia anasoma akaelewa hata awe kasoma kingereza vipi atatoka kapa sababu English ilitotumika mule siyo English tunayotumia leo hii wanaojifunza mashuleni uko

Hilo neno "Shall" maana ambayo mwanasheria wetu wanaipigia kelele is out dated wenzetu washatoka uko shall not obligation tena hata kwenye sheria kwa sasa kwaiyo kipindi sheria ya kuwepo kwa CAG inatungwa wataalamu wetu hawakuchunguza hii helping verb shall kwa dunia ya sasa kwenye sheria je bado inabeba nguvu ile ile au vipi wakaandika tu

Kwaiyo kwa udhaifu huu wa katika yetu na tukio hili ni muda muafaka tena tuombe katiba mpya

Miye siyo mwanasheria pengine wanasheria watuambie je kwenye katiba huwa kuna sehemu hizi helping verb tata mfano shall je kuna sehemu huwa inaekezewa maana mfano

Shall katika katiba hii imetumika kuonyesha ulazima siyo hiyari ni lazima kwaiyo popote ilipotumika shall basi lazima je ipo

Kama ipo twendeni magogoni tukamchukue mzee kama haipo tuwe Walpole tu
 
Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,942
2,000
Mie nadhani pande zote zina hoja za msingi wale wanaosema katiba imevunjwa na wale wanaodai raisi hana ulazima wa kumuongezea muda.

The literature does not provide clear demarcation with the statement “shall be eligible” .

Kwenye nchi za wenzetu kwa uelewa ya kuwa draftsman anaweza leta mkanganyiko with the ‘literal rule’ kama ilivyo kwenye hili sakata.

Mahakama ingeamia kwenye “purposive rule” kutaka kujua hiyo sheria ilikuwa inalenga nini haswa na hapo ndio wanarudi mpaka kwenye Hansard za bunge kusoma mijadala na bill yenyewe kuona intentions zilikuwa ni zipi CAG ataendelea baada ya fixed term kama hana makosa (na hii stage ni kama review tu) au anaweza timuliwa baada ya miaka mitano.

If you ask ntasema ajatendewa haki simply for customary reasons ambazo kwa wenzake zilitumiwa kuwaongezea muda na yeye kunyimwa haki hizo.
 
GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,431
2,000
Mkuu wewe umeongea point sana

Tatizo watu walifundishwa shall maana yake lazima na walimu wa UPE
Kipindi watu wanadai mabadiliko ya katiba hawakuwa wajinga lawama zote hizi ujinga wote huu tunampelekea mh jakaya kikwete kukataa mabadiliko ya katiba

Mh magufuli tutampigia kelele bure katumia udhaifu wa katiba yetu kufanya huu ujinga wanasheria wanapiga kelele tu ila mh rais katumia udhaifu wa katiba katika lugha kufanya huu ujinga

Tukumbuke mwanasheria siyo mtaalamu wa lugha sasa ukienda kwenye taaluma ya kugha hususani kingereza kuna hii kitu

"Linguistic prescription, or prescriptive grammar," hii kwa lugha nyepesi tunaweza isema ni kanuni ambayo inaonyesha matumizi sahihi ya lugha katika vipengele vya uandishi, utamkaji, misamiati, maana ya maneno, na muundo wa sentensi katika lugha

Wataalamu wa lugha mnajua kingereza kinachotumika kwenye sheria na biblia ni kingereza kipi middle English, siyo modern English na ndio maana vigum mtu asiye mwanasheriakusoma judgment ya mahakama akaielewa au mtu ambaye ajasoma Bible knowledge akachukua biblia anasoma akaelewa hata awe kasoma kingereza vipi atatoka kapa sababu English ilitotumika mule siyo English tunayotumia leo hii wanaojifunza mashuleni uko

Hilo neno "Shall" maana ambayo mwanasheria wetu wanaipigia kelele is out dated wenzetu washatoka uko shall not obligation tena hata kwenye sheria kwa sasa kwaiyo kipindi sheria ya kuwepo kwa CAG inatungwa wataalamu wetu hawakuchunguza hii helping verb shall kwa dunia ya sasa kwenye sheria je bado inabeba nguvu ile ile au vipi wakaandika tu

Kwaiyo kwa udhaifu huu wa katika yetu na tukio hili ni muda muafaka tena tuombe katiba mpya

Miye siyo mwanasheria pengine wanasheria watuambie je kwenye katiba huwa kuna sehemu hizi helping verb tata mfano shall je kuna sehemu huwa inaekezewa maana mfano

Shall katika katiba hii imetumika kuonyesha ulazima siyo hiyari ni lazima kwaiyo popote ilipotumika shall basi lazima je ipo

Kama ipo twendeni magogoni tukamchukue mzee kama haipo tuwe Walpole tu
 
Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
5,132
2,000
GUSSIE

Yaani umekaa ukafikiria na ukatumia muda kuanza kuandika pumba hizi. Acheni ushabiki, mara nyingine chukua muda kuuliza werevu wakujuze kabla hajapost au soma tu mada za wenzio kisha sepa.
 
Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
5,132
2,000
Kipindi watu wanadai mabadiliko ya katiba hawakuwa wajinga lawama zote hizi ujinga wote huu tunampelekea mh jakaya kikwete kukataa mabadiliko ya katiba

Mh magufuli tutampigia kelele bure katumia udhaifu wa katiba yetu kufanya huu ujinga wanasheria wanapiga kelele tu ila mh rais katumia udhaifu wa katiba katika lugha kufanya huu ujinga

Tukumbuke mwanasheria siyo mtaalamu wa lugha sasa ukienda kwenye taaluma ya kugha hususani kingereza kuna hii kitu

"Linguistic prescription, or prescriptive grammar," hii kwa lugha nyepesi tunaweza isema ni kanuni ambayo inaonyesha matumizi sahihi ya lugha katika vipengele vya uandishi, utamkaji, misamiati, maana ya maneno, na muundo wa sentensi katika lugha😀😀😀😀

Wataalamu wa lugha mnajua kingereza kinachotumika kwenye sheria na biblia ni kingereza kipi middle English, siyo modern English na ndio maana vigum mtu asiye mwanasheriakusoma judgment ya mahakama akaielewa au mtu ambaye ajasoma Bible knowledge akachukua biblia anasoma akaelewa hata awe kasoma kingereza vipi atatoka kapa sababu English ilitotumika mule siyo English tunayotumia leo hii wanaojifunza mashuleni uko

Hilo neno "Shall" maana ambayo mwanasheria wetu wanaipigia kelele is out dated wenzetu washatoka uko shall not obligation tena hata kwenye sheria kwa sasa kwaiyo kipindi sheria ya kuwepo kwa CAG inatungwa wataalamu wetu hawakuchunguza hii helping verb shall kwa dunia ya sasa kwenye sheria je bado inabeba nguvu ile ile au vipi wakaandika tu

Kwaiyo kwa udhaifu huu wa katika yetu na tukio hili ni muda muafaka tena tuombe katiba mpya

Miye siyo mwanasheria pengine wanasheria watuambie je kwenye katiba huwa kuna sehemu hizi helping verb tata mfano shall je kuna sehemu huwa inaekezewa maana mfano

Shall katika katiba hii imetumika kuonyesha ulazima siyo hiyari ni lazima kwaiyo popote ilipotumika shall basi lazima je ipo

Kama ipo twendeni magogoni tukamchukue mzee kama haipo tuwe Walpole tu
Kweli JK alishindwa kutuletea katiba mpya, lakini tusimlaumu sana kwa suala la Katiba mpya bali tumlaumu kwa kutuletea Jiwe anaye kataa kumalizia katiba mpya na anaye vunja hata hiyo katiba ya zamani yenye vitu vichache vizuri.

Ina maana hata kama JK angeleta katiba mpya, huyu Jiwe angeivunja tu kwa hulka yake.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,323
2,000
Naunga mkono hoja
Tusimlaumu Rais Magufuli kwa lolote, yote anayoyafanya ni kwa mujibu wa katiba
He has all the powers to hire and fire as he pleases

P.
 
mikeimani

JF-Expert Member
Jun 20, 2015
3,037
2,000
Screenshot_20191105-072343.jpg
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom