Levels baby
JF-Expert Member
- Sep 26, 2019
- 831
- 768
Kwanza nianze kwa kusema mimi ni mwana CCM asilia sio wa kuja kama wapiga gitaa hapo ndani Lumumba na mtaani ili mradi mkono uende kinywani na wengine kuanzisha vikundi vya kwaya/blogs kwa ajili ya kumsifia mkuu wa nchi ili wapate chochote maana wameujua udhaifu wa mkuu wa nchi.
Turudi kwenye mada kumekuwa na malalamiko mengi sana ya watumishi wa umma kudai kuongezewa mshahara, 1sasa hapa linakuja suala mbona wenzetu wanang'ang'ania kuongezwa mshahara kwani hizo kazi za umma si ni kama kujitolea na ambae kachoka kujitolea anaweza kutoka na kuja kupambana na wajasiliamali huku mtaani aone mchezo unavyoenda.
Pia mtumishi akiona mshahara haumtoshi si aje mtaani awaachie wengine maana kuna vijana wengi sana mtaani wanahitaji ile nafasi yake na kwa mshahara ule ule anaodai haumtoshi, lakini vijana huku wanaona utawatosha kabisa na wataendesha familia kupitia hikohiko kidogo watachopata serikalini.
Namalizia, mkuu wa nchi haina haja ya kuongeza mshahara ambae hawezi awapishe wenzie ambao wataweza bora hizo hela peleka kwa maendeleo mengine sio kuwapa hao wakaa kwenye viti kungoja mshahara kila mwisho wa mwezi.
Sent using Jamii Forums mobile app