Rais Magufuli, funga ma-Profesa

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
3,834
2,000
Rais wangu unayeonyesha njia. Naomba niseme hakuna kitu kibaya kama mtu muelewa anapoonyesha ujinga kwa amkusudi. Ma-profesa wanaongoza taasisi za elimu ya juu, taasisi ambazo kwa wengi wetu ndo ulikuwa mwisho wa kukaa darasani, taasisi ambazo zinafundisha masomo ya taaluma. Huko ndo tunatengeneza wanasiasa, wataalamu na hata wagunduzi. Imekuwaje taasisi hizi zimekuwa ndiyo kitovu cha wizi na ubadhilifu wa mali ya umma?

Viongozi wa taasisi hizi wamekuwa ni mfano wa uongozi mbaya kabisa. wanaonyesha kizazi kijacho kwamba, elimu si chochote bila wizi. Najiuliza swali rahisi linalonipa hasira, iweje mwanafunzi afariki dunia na bado wanapeleka jina lake ili apewe mkopo!

Hii ni makusudi, bila kisingizio cha walioko chini yao. Viongozi hawa wanawatumia walioko chini yao kudumisha wizi.

Bila kujali heshima unayowapa naomba wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. wanatutia 'uchuro.'
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom