Rais Magufuli, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Hatua tunazopiga

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,466
2,860
Dira ya Maendeleo ya Taifa iliyoasisiwa mwaka 1997 na Rais Mkapa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango wakati huo Nassoro Malocho ililenga na bado inalenga kututoa kutoka uchumi wa chini kwenda uchumi wa kati.

Malengo ya dira ni kuhakikisha tunakuwa na

Uchumi wa kati (High quality livelihood)

Amani, Utengamano na Umoja (Peace, stability and unity)

Utwala bora (Good governance)

Jamiii iliyoelimika na inayojifunza (A well educated and learning society)

Uchumi shindani wenye uwezo wa kutengeneza maendeleo endelevu na kufaidika kwa pamoja kupitia maendeleo hayo.

(A competitive economy capable of producing sustainable growth and shared benefits)



Tukirejea maadua watatu wa Taifa hili walio-ainishwa na baba wa Taifa Mwl. Nyerere bado wapo mpaka leo. Umasikini, Ujinga na Maradhi.



Inaboa sana na inavunja moyo pale ambapo mbinu na mikakati ya kuwashinda maadui hao sio jumuishi. Na kama inajumuisha kuna nyakati inafunga milango na kutatua matatizo kwa jina la sera, taratibu na mazoea. Kwa kifupi huwa tunafanyaga hivi… na hatufanyagi hivyo wewe mtu mpya unapokuja na model inayoweza kuwa suluhisho.



Sio vibaya kujikumbusha maneno ya Jemedari wa Vita huko Uchina Sun Tzu aliyosema katika karne ya 6 kabla ya Kristo.

If you know the enemy and know yourself, you need not fear the result of a hundred battles. If you know yourself but not the enemy, for every victory gained you will also suffer a defeat. If you know neither the enemy nor yourself, you will succumb in every battle. - The Art of War by Sun Tzu, 6th century BC.

Kama wamjua adui na wajijua vyema, huhitaji kuogopa matokeo ya vita mia mbele yako. Isipokuwa, kama wajijua ila humjua adui yako, kwa kila ushindi unaoupata kuna uwezekano tena kushindwa. Kama hujijui na humjui adui yako, utanyoosha mikono juu kwenye kila pambano.

Rais JPM toka aingie amejipambanua kuwa very decisive kwa yale anayoona yako sawa bila kujali “dunia” inamuunga mkono au la, JPM amekuwa very optimistic kuhakikisha kinatimia/kinafanyika.

Watendaji au wasaidizi wa JPM huku tuliko ambako sisi wengi tunaweza kuwafikia, naomba kusema, baadhi yao either ni waoga au hawajui nini kitakiwa kufanyika kwa kujifichia kwenye kivuli cha sera haisemi hivyo au huo sio utaratibu wa serikali.

Leo hii dunia anafadika na watu wafuatao ambao hawakupita katika mifumo rasmi ambayo kama ingetumika kama msingi wa mafanikio bila shaka ilitakiwa wasiwe pale walipo na dunia isifaidi kazi zao.

Mark Zuckerberg, ali-drop Harvard ili ku-develop kitu kipya kabisa ambacho leo kinamuingiza mabilioni ya hela na Marekani kufaidika nae kwa kutoa ajira na kodi wka Serikali. Bill Gates wengi tunajua nae ali-drop out akaja na Microsoft. Leo hii MS program zimekuwa user friendly kwa watumiaji wengi. Jack Ma, mwl wa Kingereza ameunda mtandao Alibaba, Alipay na Ali-Exepress kuziunganisha biashara za Wachina na dunia nzima. Jeff Bezoz alianzishia ofisi yake kwenye “car park” leo hii ni Jeff anafungasha “mpunga” USD 156.8 billion USD sawa na 358,664,320,000,000.00

Leo hii kuna Wanzania wana very very feasible projects/not ideas…Project. Zishafanyiwa tafiti za kutosha, zifanyanyika sehemu zingine za dunia, ikifikia wakati unawataka/unawahitaji wadau katika sekta ya umma wacheze nafasi zao… hapooo patamu sana… It takes ages for decisions to be made.

Jamani, jamani Watanzania, ina maana mpaka sasa hatumjui adui yetu na umasikini, ujinga na maradhi? Bila shaka ukosefu wa ajira nae anaingia kama mmoja wa maadui.

Mifumo ya wapiganaji wakiwa vitani huwa wanaua maadui/wanaondoa maadui. Anemies are eliminated. Tanzania kuna nyakati chance zinatokea, ili tusimame kwa pamoja kuwaondoa maadui… It breaks hearts and it hurts when you see the other part does not player their role?

Nataka kuamini, ili tushinde vita hii hatuwezi kushinda kwa jeshi la mtu mmoja aitwae JPM. Mpira wa miguu una wachezaji 23. 11 uwanjani na substitute nje ya uwanja. Waliobakia kuna nafasi ya kufanyiwa rotation.

Sweden ina idadi ya watu million 9.85. Pamoja na udogo wao kwa size na idadi ya watu wamekuwa na mkakati wa kupata maarifa na taarifa za kutosha ili kuwa na compepetiv advantage duniani. Walihakikisha kila M-Swede anafaamu kwa ufasaha lugha zingine 3 ili kufidia mapungufu waliyonayo dhidi ya ushindani dunani. Mwaka 2010, iikuwa na kampuni 30 kati ya 2000 katika orodha ya Forbes.

Ndugu zangu, tunaweza kwenda mbele tukiamua. Rais Magufuli amejipambanua kutumia mizinga ya akina Kafulila, Machali, Shonza na Patrobas Katambi kufikia malengo ya kisiasa. Kuna vijana wa Kitanzania watumiani basi kufikia malengo endelevu ya Kiuchumi. Vetting kuwapata wanasiasa huchukua muda. Katika kupigana dhidi ya maadui umasikini na ujinga, msifanye vetting weeeee… muda unapopoteza haiwezekani kabisa kukomboa.

Maadui umasikini, ujinga na maradhi tunawafahamu, tutumieni kila silaha kuwaangamiza. Adui wa nne ajae ni ukosefu wa ajira anaua fursa ya kuwatumia vijana kama wazalishaji kwa kuwa tu kuna fursa chache za wao kufanya kazi.

Jamiii iliyoelimika na inayojifunza (A well educated and learning society)Tukubali kujifunza kwa wenzetu walo nje ya mfumo wa sekta ya umma kwa lengo ya kutufanya tupige hatua. Kila mmoja ana kiwango cha maarifa na tunahitaji maasada we wenzetu ili kuwa na wachezaji 11 ambao. Sote ni Watanzania jamani.

Watanzania tuko tayari, tunaomba huko sekta ya umma muongeze kasi ya kufanya kazi nasi.
 
Mtoa mada una kichwa cha panzi na unatakiwa kukumbushwa kubakiza akiba ya maneno, uchafu unaorusha kwa Makonda wewe mwenyewe utakuja kuusafisha. Kumbuka ya Lowasa.

Siku Makonda akihamia chadema atapata mapokezi makubwa
na kusafishwa kwa kila aina ya Omo na kubatizwa mleta mabadiliko wa Ufipa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amani, utengamano na umoja nadhani tumeanza kuutengeneza kwa kuwashawishi wapinzani wawe kitu kimoja na watawala

'HOW MUCH IS TOO MUCH?'
 
Back
Top Bottom