Rais Magufuli: Dhana ya Viwanda; je, unafuatilia maagizo yako?

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,337
4,667
Baadhi ya Watanzania tunakuelewa vizuri sana juu ya ndoto na dhana yako nzima ya Ujenzi wa Viwanda nchini.Tunakuelewa kuwa wajenzi wakubwa wa viwanda katika nyakati zetu hizi za Uchumi wa Soko wanapaswa wawe wananchi wenyewe na sio Serikali.

Tunakuelewa vizuri kuwa Serikali ikiwa ndio mjenzi mkuu wa Viwanda hivyo kuna uwezekano mkubwa viwanda hivyo vikafa baada ya Uongozi wako kumalizika sababu ya ufisadi,kutowajibika na Uzembe utakaoweza kujitokeza wakati huo.

Katika mazingira kama hayo,juzi ulipotoa tamko la mtu yeyote yule anayeona anao uwezo wa kujenga kiwanda basi asicheleweshwe na Taratibu kama vile za NEMC,OSHA,TBS na wengineo badala yake mtu huyo ajenge tu kiwanda na taratibu hizo zitamfuata wengi wetu tulifurahia sana.

Katika kuitikia wito wako huo leo nilipiga hodi ofisi za NEMC,Regent Estate.Nilichokikuta huko ni tofauti kabisa na tamko lako.Tamko lako halijashuka kwenye mamlaka husika na wala hakuna hadi muda huu mkakati wowote wa utekelezaji wa agizo lako.NEMC wanadai wao wanaongozwa na sheria na wala sio "matamko" tu. NEMC wanatekeleza sheria iliyotungwa na Bunge.Mtu yeyote yule atakayejenga kiwanda bila kufuata sheria akigundulika kuwa amekiuka taratibu,kanuni na sheria na kwamba mbaya zaidi hicho kiwanda ni Polluting basi mkono wa sheria utamwangukia!

Mheshimiwa Raisi,kwa nini unatoa maagizo na maelekezo na wasaidizi wako wanachelewa kushusha chini miongozo ya utekelezaji wa hayo matamko? Tunataka kujenga viwanda kwa ajili ya uchumi wa Taifa letu lakini inavyoelekea wasaidizi wako wengi sio Active.Wengi wao ni lazy.Ni non-visionary.Wengi wao ni wasindikizaji.Baafhi yao wako kwenye foleni wakisubiria wakucheke pale utakaposhindwa juu ya dhana yako ya Viwanda na mengineyo.Waziri wako wa Mazingira hadi leo anafanya nini? Kwa nini toka utoe tamko hilo yeye hajatoa mwongozo wowote ule? Je,tujenge viwanda bila ku-mind cha OSHA au NEMC kisha tuje tushitakiwe? Je,tukishitakiwa nani atakuwa mtetezi wetu?
 
mkuu ..malalamiko yako yanahusu kucheleweshwa kupata clearance au unataka na taratibu zikiukwe?
 
Kama uko kwenye hii industry ya uwekezaji utakuwa unaelewa tamko la Raisi Magufuli halikutoka hivi hivi tu.Ni kwamba kuna malalamiko ya muda mrefu sana juu ya taasisi alizozitaja Raisi kama ni vikwazo kikubwa kwa wanaokusudia kujenga viwanda.Hiki ni kilio cha muda mrefu.Mimi nilienda huko kwa sababu nataka kujenga kiwanda.Nilitaka kupata ufafanuzi iwapo bidhaa zangu tarajiwa zinaangukia kwenye eneo ambalo NEMCniControllers au siyo.Sasa katika kuwauliza wamepokeaje agizo la Raisi maana mimi natarajia kujenga kiwanda kwanza kadri ya maagizo ya Raisi kisha ndio wao wa-chip in na taratibu zao (ikiwa wanahusika) basi ndio wataka-respond kama nilivyoeleza hapo juu kwenye "Uzi mama".Kwa hiyo, hoja ni kwamba: je,Raisi anafuatilia utekelezaji wa maagizo yake mintarafu hili la Kuto-mind Regulatory Authorities katika uanzishaji wa Viwanda? Kama sivyo,watu wengi tutajikuta tunafuata maelekezo yake halafu mbeleni tunaumia.Juzi nimeongea na taasisi za fedha nao wanakutaka ili uweze ku-enjoy investment loans ni lazima requirements za regulatory authorities ziwepo.Katika mazingira kama hayo wajasirimali wanawekwa kwenye cross-roads na wataishia kuwa productively stranded.
 
Mkuu kwanza nikipongeze kwa jitihada zako za kuanzisha kiwanda na mwitiko wa kizalendo kabisa...lakini tukubali kuwa ni lazima uanzishwaji wa viwanda uendane na ubora na regulations zilizopo...ili tu baadae tusije kuanza kulia kilio cha uharibifu wa mazingira n.k

Mimi naamini alichokisema Rais ni kwa taasisi zinazoregulate ziwe quick na ziwasaidie watu katika process ya kuanzisha viwanda.

Kama kuna mkwamo kwenye hilo la kuharakisha na kusaidia basi ni wazi Serikali itatakiwa ijirekibishe...

Kama unaweza kueleza ni kipi specifically kinachokukwamisha ingekuwa nzuri wahusika waweze kusikia.
 
Mkuu mintarafu kunipongeza kwa hatua ninayoichukua huo ni wajibu wangu toka kuumbwa.Kwamba naulimbwa na "kunyunyizwa" uwezo wa Kimungu ili niendeleze uumbaji.Bila uumbaji mwingine maisha hayana ladha.Kwa hivi,sistahili pongezi yoyote ile.

Hili la kufuata sheria ili kutoharibu mazingira Siku za usoni kila mtu analijua.Tatizo ni lao hao jamaa kufanya regulation kama vile kusubiria safari ya kwenda Mars.Agizo la Raisi limelenga kuondoa hiyo hali ya watu kukaa kana kwamba wanangojea sakrament ya Kitubio. Sasa unasema agizo la Raisi limelenga kuwafanya mamlaka zinazohusika wafanye mambo haraka? Kwa hiyo unamaanisha Raisi asieleweke kuwa alimaanisha watu tuanze tu kwanza kujenga viwanda madhali uwezo wa kufanya hivyo upo kisha hao OSHA na NEMC wengineo ndio watakuja baadaye na taratibu zao? Kwa hiyo tumuelewe Raisi Kinyumenyume?
 
Viwanda ni porojo tu
ndo maana wenye viwanda wengi wako kiimya kabisa
mambo hayaeleweki
 
Mkuu kwa uoni wangu Mkuu wa nchi ana dhamira ya dhati ila wanaomkwamisha ni watendaji wake.Wale wanaopaswa kutafsiri maelekezo na maagizo ya Raisi ndio shida.Kwa mfano suala hili la NEMC linamhusu Makamba Jr.Je,hadi wakati huu ameshatoa maelekezo gani kwa NEMC? Haiwezekani NEMC waendelee kuwa kikwazo katika sekta ya uwekezaji.Kwanza fee zao ni very high. Halafu Wanasema wao wataendelea kutekeleza sheria hadi itakapobadilishwa.Wanalalamika kwa mfano kuna watu walienda kuomba kufungua viwanda vya vifungashio vya plastic (mifuko ya rambo) lakini NEMC ikawakatalia kuwa hiyo mifuko mwisho wake unakaribia (kwa kadri ya tangazo la Serikali) lakini cha ajabu hadi muda huu hiyo ban haijawa operational! Maana yake nini? Huoni tatizo ni la wasaidizi kama huyo Makamba?
 
Mkuu ni kweli kabisa usemavyo....WATENDAJI NI JIPU kwenye hizi harakati za ujenzi wa Tanzania ya viwanda
 
Kwa hili agizo lake la kutojali Assessment of Enviromental Impact ni kama mtego kwa January Makamba. Anasubiri ajiingize kwenye kumi na nane ili afyeke kichwa.
 
Kwa mtizamo wangu afyeke tu.Ni kati ya watu wasio-perform kwa mtizamo wangu.
 
Mkuu mintarafu kunipongeza kwa hatua ninayoichukua huo ni wajibu wangu toka kuumbwa.Kwamba naulimbwa na "kunyunyizwa" uwezo wa Kimungu ili niendeleze uumbaji.Bila uumbaji mwingine maisha hayana ladha.Kwa hivi,sistahili pongezi yoyote ile.

Hili la kufuata sheria ili kutoharibu mazingira Siku za usoni kila mtu analijua.Tatizo ni lao hao jamaa kufanya regulation kama vile kusubiria safari ya kwenda Mars.Agizo la Raisi limelenga kuondoa hiyo hali ya watu kukaa kana kwamba wanangojea sakrament ya Kitubio. Sasa unasema agizo la Raisi limelenga kuwafanya mamlaka zinazohusika wafanye mambo haraka? Kwa hiyo unamaanisha Raisi asieleweke kuwa alimaanisha watu tuanze tu kwanza kujenga viwanda madhali uwezo wa kufanya hivyo upo kisha hao OSHA na NEMC wengineo ndio watakuja baadaye na taratibu zao? Kwa hiyo tumuelewe Raisi Kinyumenyume?
Hivi unaanzaje mjibu huyo jamaa.. huyo ni mtu wa Chama kwanza ufahamu baadae
 
Back
Top Bottom