Rais Magufuli, BoT wamefanyaje kuifanya Tsh. kuwa stable against USD?

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,396
2,000
Wakati wa Tawala zilizopita shilingi ilikuwa inacheza sana, ilikuwa haitulii kabisa. Hata JPM alipoingia madarakani kuna kipindi shilingi iliyumba sana hadi tukalamika hapa JamiiForum kuwa mabeberu kuna namna wanatuhujumu katika hili.

Badae serikali ikaingilia kati tatizo likaisha shilingi ikarudi 2270 kama nakumbuka vizuri. Tokea hapo ikashuka tena kidogo hadi 2300 na vipoint hivi . Tangu kipindi hicho shilingi imechezea 2300 hadi 2319, hili limedumu kwa muda mrefu sana.

Watalaam wa uchumi hebu tufafanulieni kipi kimetokea huku kuna tetesi kuwa uchumi wetu unasinyaa.

New.JPG
 

Thomas10

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
580
1,000
Yan hapo imekuwa stable!!??
Ilipanda kwa 300/= kwa miaka 10, yaani 2005 ($1=tsh1200) hadi 2015 ($1=tsh1500)

Tangu 2015 umepanda kwa tsh800, yaan 2015 ($1=tsh1500) hadi 2020 ($1=tsh2300)

Sasa na wew tusaidie huo u-stable lioufanya JPM na BOT ni upi???
 

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
4,647
2,000
Tulia utafurahi baadae dunia haingozwi Kwa ubabe na vitisho Ila inaongozwa Kwa nguvu ya demand and supply. Just FYI BOT tuna audit wenyewe nayanayo endelea humo wanajuwa wenyewe.

Requirement ya world Bank and IMF ni kwamba BOT iwe audited na independent auditor kwasababu huwezi tumia mwenyewe nakujikaguwa mwenyewe nakusoma report mwenyewe. Kiufupi baadae Sana tutachekea chooni nakulilia bafuni. Naipenda Tanzania Ila I say no for other policies we introduce.
 

Thomas10

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
580
1,000
Sijakuelewa mkuu, una maanisha kimefanyika kama cha Nyerere yeye kuamua change iweje bila kuzingatia hali halisi ya uchumi? Kama ndiyo mbona mabeberu kipindi kile waliingilia kati hadi mwl akasalimu amri katika hili sasa iweje leo wakae kimya?
Mabeberu et!!?
Km tu mafisiccm
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
57,975
2,000
Yan hapo imekuwa stable!!??
Ilipanda kwa 300/= kwa miaka 10, yaani 2005 ($1=tsh1200) hadi 2015 ($1=tsh1500)

Tangu 2015 umepanda kwa tsh800, yaan 2015 ($1=tsh1500) hadi 2020 ($1=tsh2300)

Sasa na wew tusaidie huo u-stable lioufanya JPM na BOT ni upi???
Wanatafutana teuzi, hivyo basi wapo kwenye ibada ya kusifu na kuabudu.
Hivi mfuko wa saruji ni shilingi ngapi?
Sukari je?
 

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
6,530
2,000
Kumbuka pia katika kudhibiti hili ofisi nyingi za kubadili pesa za kigeni (Bureau de Change) zilifungwa na watu wengi hasa wanasiasa walilalama sana. Hilo ilikuwa ni mojawapo ya njia kukabili hili kwani utakatishaji fedha ulifanyika kwa kiasi kikubwa katika maduka hayo.

Pia uhamasishaji wa matumizi ya bidhaa za ndani kupunguza uagizaji toka nje na kuongeza mauzo ya nje kumechangia. Utamsikia Magu anasema, ni aibu kuagiza ngano na sukari nje.

Tukiepuka kuagiza baadhi ya vitu kama sukari na ngano na vingine tunavyoweza kuzalisha hapa nchini tunakuwa tumepunguza uhitaji wa pesa za kigeni ikiwemo dola ya US.

Kwa maana hiyo sasa dola isipohitajika thamani yake inapungua, na pesa yetu ikahitajika zaidi ili watu waweze kununua kwetu ina maana shilingi yetu inazidi kuimarika.

Kitu kisipokuwa na wateja hukosa soko na thamani yake hushuka
 

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,396
2,000
Yan hapo imekuwa stable!!??
Ilipanda kwa 300/= kwa miaka 10, yaani 2005 ($1=tsh1200) hadi 2015 ($1=tsh1500)

Tangu 2015 umepanda kwa tsh800, yaan 2015 ($1=tsh1500) hadi 2020 ($1=tsh2300)

Sasa na wew tusaidie huo u-stable lioufanya JPM na BOT ni upi???
2015 nakumbuka usd ilienda hadi 1700 kama sio 1650. Ila nimekiri kuwa mwanzoni mwa utawala wa Jpm usd ilipanda sana ndio maana nikasema toka iliposhuka kuwa 2270 hadi kuwa 2300 ni miaka kama minne kasoro nadhani, sasa nauliza kipi wamefanya kwenye hii miaka mitatu na uchafu? Ndio swali langu liko hapo mkuu
 

secret file

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
4,155
2,000
Kimbuka pia katika kudhibiti hili ofisi nyingi za kubadili pesa za kigeni (Bureau de Change) zilifungwa na watu wengi hasa wanasiasa walilalama sana. Hilo ilikuwa ni mojawapo ya njia kukabili hili kwani utakatishaji fedha ulifanyika kwa kiasi kikubwa katika maduka hayo...
Well said hata wasio na uelewa wakisoma hapa wanaelewa
 

Thomas10

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
580
1,000
2015 nakumbuka usd ilienda hadi 1700 kama sio 1650. Ila nimekiri kuwa mwanzoni mwa utawala wa Jpm usd ilipanda sana ndio maana nikasema toka iliposhuka kuwa 2270 hadi kuwa 2300 ni miaka kama minne kasoro nadhani, sasa nauliza kipi wamefanya kwenye hii miaka mitatu na uchafu? Ndio swali langu liko hapo mkuu
Kuna mambo mawili, moja kati ya hayo lina ukweli
1. BOT wanaedit data wenyewe ili kutuaminisha kuwa tsh imekuwa imara dhidi ya fedha za kigeni.
Na hii ni kutokana na kuendesha finance wenyewe, kujikagua wenyewe na kuripoti wenyewe

2. Inaweza kuwa kweli kwa sababu maduka ya kubadirisha pesa yamedhitiwa hivyo ubadirishaji holela umeondoka na kufanya mfumo wa imara.

Sasa hapo sote hatujui, ila wao na wafuatiliaji.

Lakin kuna namna rahis ya kujua, moja wapo ni kuwa mteja wa kubadirisha fedha za kigeni, hapo utajua
 

At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
3,332
2,000
Tulia utafurahi baadae dunia haingozwi Kwa ubabe na vitisho Ila inaongozwa Kwa nguvu ya demand and supply. Just FYI BOT tuna audit wenyewe nayanayo endelea humo wanajuwa wenyewe. Requirement ya world Bank and IMF ni kwamba BOT iwe audited na independent auditor kwasababu huwezi tumia mwenyewe nakujikaguwa mwenyewe nakusoma report mwenyewe. Kiufupi baadae Sana tutachekea chooni nakulilia bafuni. Naipenda Tanzania Ila I say no for other policies we introduce
Aaah,

Kumbe ni wewe?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom