Rais Magufuli, Bashiru wagonga mwamba, walazimisha maamuzi yao kupita bila pingamizi, NEC wagoma kuburuzwa

GARETHBALE

Member
Dec 22, 2013
76
332
Kikao cha NEC kikiendelea kusubiriwa kwa hamu sana, ili kujipanga kwa ajili ya Uchaguzi mkuu ujao pia kwa ajili ya kupokea Maazimio ya Central Committee juu ya Kinana, Membe na Makamba.

Tayari wanaCCM nchini kote wamewashangaa Magufuli na Bashiru kwa kukiuka kanuni za ccm na kutoa maazimio yao mfukoni na kuyakataa yale ya kamati ya Maadili chini ya Mzee Mangula.

Tayari MAGUFULI na Bashiru wametumia kipindi hiki cha corona kushawishi WaNEC wakubaliane na Maamuzi yao ya Mfukoni, wanasahau kuwa Mzee Mangula anaumwa.

Mnec mmoja kutoka kanda ya kati alisikika akisema " Tumechoshwa na uhuni unaofanywa na Mwenyekiti na Katibu, wamekuja kutuharibia ccm yetu,".

WaNEC wanasema wao ndio walioituma kamati ya Mangula iwahoji akina Kinana, kwa hiyo wanasubiri ripot kutoka kamati ya maadili ili watoe maamuz rasmi ya chama.

WaNEC wengi wanasikitika kitendo alichofanyiwa Mzee Mangula, cha kugombezwa kama mtoto mbele ya wajumne pale alipotaka kuisoma ripot ya kamat yake.

Corona inaua, tuchukue taadhali na tufuate maelekezo ya wataalamu wa afya.

Mungu ibariki Tanzania.

Ni mimi Mwajuma Mwasapili
Kutoka Ileje- Mbeya
0754297651
 
Hakuna chombo Cha kutangua maamuzi ya kamati kuu ndani ya CCM zaidi ya kamati kuu yenyewe na maamuzi ya Kamati kuu ndio ya mwisho. Vikao vingine vya CCM ni kupokea maazimio ya Kamati kuu.

Maamuzi ya mfukoni ni yapi hayo? Maamuzi yaliyotolewa ni maamuzi ya pamoja. Utaratibu ukiukwe wakati wa kutoa maamuzi wakati uamuzi unatolewa kwa taratibu zilizopo?

Kamati ndogo ya maadili na usalama kazi yako ni kupeleka mapendekezo kamati kuu. Kamati kuu inaweza ikakataa mapendezo yote au sehemu ya mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ndogo ya maadili na usalama.
 
Huyo ni Chadema anajitekenya Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mwenyekiti ana genge lake ambalo litawaburuza kama wake zao. Mwenyekiti na genge lake alianza kuwaona wajumbe wote ni Mabwege baada ya kuleta mamluki toka upinzani na kuwapa nafasi za kugombea ubunge kihuni, bila kufuata utaratibu na mkakaa kimya. Sasa hivi kawaona nyie ni bendera fuata upepo hivyo anawaburuza tu atakavyo. Na tatizo la mwenyekiti wenu kuwaburuza, ni baada ya kugundua kuwa mnategemea ile kofia yake kubwa kupata madaraka.

Tuliwaambia wanaccm kuendelea kupata madaraka bila ridhaa ya wananchi, bali kupitia kofia nyingine ya mwenyekiti wenu, tabia hiyo ataitumia pia hata kuwafanyizia nyinyi. Nadhani sasa mnaona jinsi ule uhuni unavyowageukia. Mtu muovu huingia kwa nyimbo za uzalendo, na mkiingia mkenge anaanza kuwafanyia uhuni. Ukiona mzalendo anachezea box la kura, basi hapo anza kustuka.
 
Back
Top Bottom