Rais Magufuli, Barrick na Nasaha za Profesa Zartman*

Cybercrime

JF-Expert Member
Feb 14, 2014
3,248
2,000
_Na Mwamba wa Kaskazini_

Bingwa wa masuala ya utatuzi wa migogoro duniani, Profesa William Zartman amewahi kueleza nadharia yake inayoshadidia wakati gani ni muafaka kuumaliza mgogoro unaoumiza pande zote mbili.

Katika nadharia yake aliyoiita “Mutual Hurting Stalemate,” Prof. Zartman anasema hakuna wakati muafaka katika kutatua mgogoro kama pale ambapo pande zote mbili zinakubali kuwa zimeumia na hakuna namna nyingine ya kuondoa maumivu hayo zaidi ya kuyaondoa.

Anaandika: “_The key to successful conflict resolution lies in the timing of efforts for resolution. Parties resolve their conflict only when they are ready to do so—when alternative, usually unilateral, means of achieving a satisfactory result are blocked and the parties find themselves in an uncomfortable and costly predicament._"

Nimetazama SAFARI ya Tanzania chini ya Jemedari Rais Magufuli katika kuutatua mgogoro na kampuni ya Barrick nikasema hakika Profesa Zartman aliona mbali na Tanzania nayo ikazingatia kuona mbali.

Watanzania wanajua jinsi ambavyo laana ya madini imesambaa katika ulimwengu huu. Wanajua kwamba nasi tumekuwa wahanga kwa kiasi fulani wa laana hiyo lakini sasa tunamshukuru Rais Magufuli. Amekuja kutufutia dhambi ya laana hii kabla haijatutafuta.

Watanzania tuliumia kuona tuna dhahabu lakini tunaishia kuona mashimo tu kule Bulyankulu huku hadi mchanga ukienda nje ya nchi-makubaliano aliyoyasimamia Rais Magufuli kidete na kuwaweka mbele wataalamu wetu akina Profesa Kabudi, Dotto James, Profesa Luoga na wengineo, ni ya kihistoria sana.

Wengi mmetazama asilimia tutakazovuna katika mkataba huu wa makubaliano, mmetazama jinsi watanzania zaidi watakavyoingia katika kusimamia uendeshaji wa migodi na uwazi zaidi katika ulipaji kodi. Hamjakosea kabisa.

Lakini kwangu kama kuna mafanikio makubwa ya makubaliano haya na Barrick ni somo ambalo Rais Magufuli na team yake ya majadiliano wamelitoa kwa nchi yetu, Afrika na dunia.

Ni kweli kwamba Barrick na wao walifikia “murual hurting stalemate” Hasa kwa sababu ya jina lao lililokuwa limeanza kuchafukwa kwa sababu ya maslahi ya watendaji wa chache wa iliyokuwa kampuni yao tanzu hapa nchini ya Acacia.

Ndio maana sikushangaa kumwona siku ile Ikulu pale nikiwa kwenye TV yangu Bw. Mark Bristow, Mtendaji Mkuu wa sasa wa Barrick International akikiri kwa kusema: “Ni kweli tulikosea. Tuko tayari kufungua ukurasa mpya.”

Hadi Barrick kufikia hatua hii, tuelewane, haikuwa safari fupi. Mnajua unaweza kusema umeibiwa usiwe na ushahidi wa kuibiwa! Kikwazo cha kwanza. Kikwazo cha pili ni uzandiki tuliouona kwa baadhi ya wenzetu waliokuwa wakinufaika na Acacia akina Zitto Kabwe, Fatma Karume na Tundu Lissu jinsi walivyoshiriki kutaka kutudhoofisha wakiwaunga mkono Acacia.

Lakini kikwazo cha tatu ni uwezo wa Barrick kifedha, na kiutaalamu. Wangeamua tu kugoma kukiri kosa, kukomaa na kutumia rasilimali zao hizo kupambana nasi.

Labda hamjui enyi wana wa Adam. Kiujuzi, uzoefu wa siasa na stratejia nyuma ya Barrick kuna watu wazito sana duniani—achilia mbali mtaalamu yeyote ambaye wangetaka kumleta katika majadiliano na kutuzidi na nasikia waliwaleta. Hadi makomandoo wa Uingereza huko!!

Nilikuwa naitazama Bodi Ya Ushauri ya Kimataifa ya Barrick (The International Advisory Board), ni hatari tupu kwa maana ya kwamba ni watu hatari na wazito-wangeweza kuleta nyodo na vitimbi. Hebu angalia baadhi ya wajumbe wao:

The Right Honourable Brian Mulroney: Huyu alikuwa Waziri Mkuu wa Kanada [1984-1993];

His Excellency José María Aznar: Alipata kuwa Waziri Mkuu wa Hispania 1996 hadi 2004

Secretary William S. Cohen: Seneta wa zamani wa Marekani (1979-1997) na amepata kuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani [1997-2001]

Lord Charles Powell of Bayswater: Amepata kuwa mshauri wa masuala ya kimataifa wa Waziri Mkuu wa Uingereza Mama shupavu Margareth Thatcher kati ya 1983 hadi 1991.

Angalia mijamaa kama hii, halafu kama alivyosema Kabudi, unakutana na mtu shule yenyewe alikuwa anakwenda siku za mahafali na michezo, halafu anakuja kubeza kazi kubwa aliyoifanya Rais Magufuli kwa kiwango cha Barrick yenye vichwa hivi kuiona hoja ya Tanzania na kuikubalia majadiliano na maafikiano.

Tunaelezwa pia ukimsifu aliyeongoza mbio, usiwasahau waliomkimbiza-kipekee niwashukuru hawa wote sijui Maseneta, Lord, maHis Excellencies na wote ndani ya Barrick kwa uaminifu wao kwa mwanadamu, kwa Mungu na kwa watanzania kwa kukubali yaishe bila vitimbi.

Asanteni sana JPM, Kabudi, Dotto, Prof Luoga na wenzenu wengi, lakini asanteni Barrick.

Ngarenaro
 

Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
4,076
2,000
Utasifu na kuimba mapambio ya kila namna lakini Wazungu ni wajanja sana... Ni suala la muda tu... Utasikia ambayo utashindwa kuyaamini...
Tuwemo!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom