Rais Magufuli, baada ya kukusanya kodi, sasa elekeza nguvu watumishi wa umma walipwe arrears zao

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,673
149,860
Mh.Raisi,kuna urasimu sana serikali wa kulipa malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa umma baada ya kuwa wamepandishwa vyeo.Mtu anapanda cheo leo na anakabidhiwa barua yake ya promotion ila mshahara utabadilika baada ya miezi hata 6 na malimbikizo yake ndio yamaweza kuchukua hata mwaka kuja kuyapata na huu kwa miaka mingi umekuwa ni kama tu utamaduni wa kawaida serikalini wakati ni jambo ambalo halipaswi kuwepo.

Hali hii mara nyingi ni matokea ya uzembe, urasimu, kutojali wafanyakazi na zaidi kufanya kazi kwa mazoea na ni moja ya vitu vinavyokatisha tamaa sana watumishi wa serikali.Mh.Raisi tunaomba hili sasa ulifanyie kazi na kila mtu aonje/aone faida ya jitihada zako za kukusanya kodi kwani kisingizio cha ukosefu wa fedha kitakuwa kimepata dawa kwa kiwango fulani.

Mh.Raisi,hili ukilisimamia na kutoa agizo,litatekelezwa mara moja na watumishi wa umma wataona matunda ya kazi yako. Tofauti na hapo,itakuwa ni sawa na zile story za watawala kujisifu uchumi umekuwa wakati mwananchi wa kawaida maisha yake yako pale pale.

Mh.Raisi,jambo lingine ni ucheleweshaji wa salary slip baada mishahara kutoka.Salary slip zina matumizi mengi kwa wafanyakazi hivyo nazo ziwe zinatolewa mapema maana sehemu nyingi huwa wanataka salary slip ambazo ni current katika kukuhudumia.

Jambo lingine mh.Raisi ni kuagiza watumishi wote wa umma wawe wamelipwa mishahara yao ifikapo tarehe 23 ya kila mwezi kama ilivyokuwa miaka ya 2006/2007 ingawa utaratibu huu ulikuja potea kwa kukosa usimamizi/ufuatiliaji.

Nchi hii kila kitu kinawezekana kukiwa na usimamizi mzuri na ufuatiliji wa shughuli za kila siku serikalini.

Umefika wakati sasa swala la malimbikizo ya watumishi wa umma liwe historia. Mnapowabana watumishi wa umma basi muwape na haki zao tena kwa wakati na si vinginevyo.

Tunaipongeza serikali kwa kutoa mishahara mapema mwezi huu na kuwawezesha watumishi kusherehekea sikukuu za Maulid na Christmass vizuri.Huu ni ushahidi kuwa kulipa mishahara ifikapo tarehe 23 ya kila mwezi ni jambo linalowezekana ebndapo litapewa uzito.
 
acha hizo mbona wakulima hawajapewa ruzuku wako kimya.. Nyie mafisadi na wazembe ndio mnataka mlipwe
 
Hivi wakulima wanalipa kodi? Bei gani baada ya kuvuna magumia matatu ya mahindi?
 
Uzi bora kuliko zote ulizowahi kuweka humu..hongera Sana umeongea jambo ambalo lipo.
 
Nadhani errers hazihaitaji audit kwa mda mrefu.nadhani serikali iwalipe ila icontrol kupandisha vyeo wakati watu hawaperform
 
kuna hela naidai tangu 2012, nikipata hata leo nafikiri hata thamani itakuwa imepungua. ajabu yake ni kwamba watanipatia ile ile bila kujua kuwa imekaa kwao kitambo na imeshashuka value.
 
...ni kweli..nina uhakika JPM akitaka apate ufanisi huko sekta ya umma basi jambo moja la msingi la kurudisha nidhamu ya kazi ni kulipa madeni ya watumishi wa umma(arrears)....hili nina hakika litachangia kuleta tija serikalini..maana wafanyakazi wanaidai serikali kwa kiwango cha kutisha...walipeni waalimu,madaktari,watafiti na wataalam wengine wote muone kama tija haitarudi....maana mnapolazimisha tija pia jalini maslahi ya watumishi wenu....

....angalizo hili liende kwa mawaziri type ya kigwangala na wengine wanaodhani kuwa unaweza kuamka asubuhi toka kwa mke wako ukalazimisha tija kwa umma bila kujali mazingira ya kazi na maslahi mapana ya watumishi wenu...
 
HALMASHAURI ZA TANZANIA ni JiPu linalosubiriwa kutumbuliwa kwa msumari wa moto tena wenye kutu kwani UOZO wote na upuuzi wote umejaa uko..WAZIRI MKUU na TAMISEMI lazima waifumue hii kitu...Wakurugenzi wengi ni MAJIPU, WAKUU WA WILAYA wengi hawajui ata job discrition zao
 
Back
Top Bottom