Rais Magufuli azungumza na wananchi wa Jimbo la Kongwa mkoani Dodoma

Two dimension array

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,593
2,380
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ameagiza wizara katiba na Sheria pamoja na vyombo vingine vya ulinzi vinavyohusika na Mahakama wapitie magereza yote nchini huko wakae wazungumze na watuhumiwa waliopo mahabusu ili kubaini mahabusu wote wanaoshikiliwa kimakosa waachiliwe.
Rais Magufuli amesema hayo leo Alhamisi Julai 18, 2019 wakati akizungumza na wananchi wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Amesema baada ya kutoa maagizo kwa wizara ya sheria, alipokuwa mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi, maofisa wa wizara hiyo walikwenda katika gereza la Butimba jana Jumatano Julai 17 mwaka 2019 na kukaa na watuhumiwa hao kwa saa saba, ambapo baada ya mazungumzo hayo watuhumiwa mbalimbali waliachiwa.

Aidha Rais Magufuli ameeleza baada ya maofisa wa wizara hiyo kutembelea katika magereza mbalimbali, jumla ya watuhumiwa 300 waliokuwa wanashikiliwa kimakosa wameachiwa huru ambapo katika gereza la Butimba watuhumiwa 75 waliachiwa kutoka mahabusu.

“Wilayani Bariadi wameachiwa watuhumiwa 100, Mugumu Serengeti watuhumiwa 52, Tarime watuhumiwa 6, Bunda watuhumiwa 24 na Kahama watuhumiwa 43 wameachiwa” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameeleza maofisa hao wanaendelea kupitia kila gereza kufanya uhakiki kwa watu wanaoshikiliwa kimakosa waachiwe, na leo Alhamisi maofisa hao watakuwa kwenye gereza la Kasungamile na Geita.

Magufuli ampigia Ndugai ‘kampeni kiaina’ Kongwa

Rais Dk. John Magufuli ameonekana kumpigia ‘kampeni’ Mbunge wa jimbo la Kongwa, Job Ndugai baada ya kusema kuwa Mbunge huyo anatosha kuliongoza jimbo hilo na kwamba haina haja ya kumchagua kiongozi mwingine kwani mbunge huyo anaisaidia nchi nzima kwa nafasi yake aliyo nayo.

Ameyasema hayo leo Alhamisi Julai 18, alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kongwa mkoani Dodoma, ambapo amewataka wagombea waliogombea nafasi ya ubunge 2015, kuachana na mawazo ya kutaka kugombea tena kwani nafasi hiyo ni ya Ndugai.

“Ninawashukuru kwa kumchagua Mbunge wenu Ndugai, maana wakati mwingine ni vigumu kwa mtu wa pale pale watu wakajua huyu ni mfalme ndiyo maana katika maandiko wafalme wengi walikataliwa maeneo walipozaliwa lakini ninawambia kuwa mmechagua mtu ambaye anasaidia nchi nzima kwa nafasi yake na msingemchagua kuwa mbunge kwa vyovyote asingekuwa spika,” amesema.

“Ninafahamu wakati wa kampeni kulikuwa na wengine waliohitaji ubunge na nilipofika hapa niliwaambia kazi si ubunge na ukweli ni kwamba wale wote waliogombea niliwateua nafasi mbalimbali wengine wakawa wakurugenzi na wengine wakuu wa mikoa hivyo nitashangaa sana kama 2020 watakuja tena kugombea hapa na wakija wajue hizo nafasi zilizowapa hawataziona tena labda wajitokeze wengine,” amesema.

Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa muda umefika wa kulienzi Jimbo la Kongwa kutokana kubeba historia ya Tanzania katika ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika

“Unapotamka Kongwa kwenye nchi ambazo zimepata uhuru kutokana na kujitolea kwenu wanaelewa, wapo walioacha hata damu zao hapa na wengine walizikwa hapa, baba wa taifa alipoamua kuzikomboa nchi zote za kusini mwa Afrika alitumia Kongwa kwa hiyo hapa kuna historia ya ukombozi.

“Ninakubaliana na ombi la spika kuwa wakati umefika wa kuienzi Kongwa hata kama ni kwa kuwa na jengo ambalo litakumbusha haya au uwanja wa ndege alioutumia Rais wa Misri na Algeria na nitakapokutana na marais hawa nitawaeleza kwamba kuna uwanja waliutumia viongozi wenu lakini bado haupo vizuri, nitachomekea chomekea,” amesema Rais Magufuli.

Leo sjui Nani atabanwa mbavu hapo
Maana magu akija ujipange

Ova
 
Baada ya rais kutembelea gereza la butimba kumekuwepo uvumi kwenye mitandao kwamba rais aliwatamukia wafungwa eti nayeye ni "mfungwa mtarajiwa".

Pia leo alipokua kongwa amesema maneno yanaumba hatuwezi kua tunaimba miaka yote sisi ni masikini ili hali nchi ni tajiri imebarikiwa kila kitu ni vile tu tumeshindwa mipango madhubuti na usimamizi madhubuti.

Je,kwa maana hiyo ya maneno huumba aliyoitoa mwenyewe kwa ulimi wake na yeye yataumba kwa Kauli yake(mfungwa mtarajiwa)aliyoitoa kwa wafungwa?
 
Kauli za kisiasa hizo

Akiwa Kongwa mchana wa leo Mheshimiwa Rais wa JMT amesema,

"kwa wafugaji wanaelewa, ukiwa machungoni simba akatokea na kukamata ng'ombe wako na ukapambana naye ili kumnasua ng'ombe huyo, utashangaa simba anavyokuwa mkali na kumng'ang'ania ng'ombe huyo utadhani ni mali yake na ukifanya masihara anaweza kukula hata wewe"

hapa alikuwa akizungumzia changamoto zinazojitokeza ktk kuleta maendeleo na kuibadilishi nchi.

Binafsi nimemuelewa na ni ushauri mzuri hata ktk maisha yetu ya kila siku.

Mungu ibariki TANZANIA, Mungu wabariki WATANZANIA na Mungu mbariki Rais wa JMT.
 
Kwa hiyo akirudi Dar asione huruma awabatize kwanza kwa moto ndiyo awatoe figo zisaidie wagonjwa
 
Akiwa Kongwa mchana wa leo Mheshimiwa Rais wa JMT amesema,

"kwa wafugaji wanaelewa, ukiwa machungoni simba akatokea na kukamata ng'ombe wako na ukapambana naye ili kumnasua ng'ombe huyo, utashangaa simba anavyokuwa mkali na kumng'ang'ania ng'ombe huyo utadhani ni mali yake na ukifanya masihara anaweza kukula hata wewe"

hapa alikuwa akizungumzia changamoto zinazojitokeza ktk kuleta maendeleo na kuibadilishi nchi.

Binafsi nimemuelewa na ni ushauri mzuri hata ktk maisha yetu ya kila siku.

Mungu ibariki TANZANIA, Mungu wabariki WATANZANIA na Mungu mbariki Rais wa JMT.
Kwahiyo yeye ndiyo simba na wananchi ndiyo mchungaji wa Ng'ombe
 
Simba hana jeuri kwa mbwa mwitu, yeye awafungulie kwa wingi tu wa shughulike na hao simba mdogomdogo mpaka watadondoka na kuwa mizoga kwa fisi.
 
Nimegundua mimi napenda sana majungu, hapa nasubiri kwa hamu sana mkuu atakaporudi Dar nione ubatizo wa moto maana tangu mzee makamba aliposema, sijawahi kuona mtu anavyobatizwa kwa moto
 
Back
Top Bottom