Rais Magufuli azua gumzo nchini China

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
JINA la Rais John Magufuli limekuwa gumzo nchini China kutokana na serikali yake kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

Aliyekuwa Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing pamoja na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wa China, ambao wanataka kuwekeza nchini Tanzania, wamemuelezea Magufuli kama Rais aliyeonesha ushujaa kupambana na rushwa ambayo imekuwa ni tatizo kubwa miongoni mwa nchi za Afrika.


Rais Magufuli alielezewa katika majadiliano maalumu, yaliyoandaliwa kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na China, kujadili fursa za kibiashara, ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya Kimataifa ya Canton yaliyofanyika katika Jiji la Guangzhou nchini China.

“Tangu Rais Magufuli aingie madarakani kuna mambo makubwa yamefanyika katika mapambano dhidi ya rushwa. Serikali ya China itaendelea kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kupambana na rushwa,” alieleza Balozi Lu Youqing.

Balozi Lu alieleza wazi kwamba msimamo wa Rais Magufuli wa kutovumilia vitendo vya rushwa, utajenga misingi imara ambayo itasaidia Tanzania kutimiza malengo yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025.


Pamoja na kusifu juhudi zinazofanywa na serikali kudhibiti rushwa nchini Tanzania, Balozi Lu aliwaeleza wafanyabiashara wa China, wanaotaka kuwekeza nchini kuwa Tanzania ni nchi yenye mazingira bora ya uwekezaji kutokana na uimara wa ukuaji wa uchumi ambao umekuwa ukikua kwa zaidi ya asilimia saba kwa mwaka na kuwa nchi inayoongoza kwa ukuaji wa uchumi Afrika Mashariki.

“Tanzania ni nchi yenye amani na utulivu wa kisiasa na kuleta matumaini katika uwekezaji. Napenda kuwashauri wafanyabiashara na kampuni zinazowekeza Tanzania kumuunga mkono Rais katika vita ya rushwa,” alieleza Balozi Lu huku akisisitiza kuendelezwa kwa ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo mbili.

Pia katika mkutano huo, Makamu wa Rais Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo wa China kwa nchi za Afrika (CAD Fund), ambao unasaidia makampuni kuwekeza Afrika, Wang Yong alieleza kuwa Tanzania ni nchi muhimu kwa uwekezaji miongoni mwa nchi za Afrika hasa katika kilimo, madini na nishati.

“Nazishukuru Serikali za Tanzania na China kupitia Balozi Kairuki na Balozi Lu kwa kuwezesha kampuni za kutoka China kuwekeza nchini Tanzania,” alishukuru Yong. Mkutano wa kibiashara kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na China ambao ulienda sambamba na Maonesho ya Kimataifa ya Canton katika jiji la Guangzhou nchini China, ulilenga kuwakutanisha wafanyabiashara hao na kufungua fursa mbalimbali za kibiashara huku Watanzania wengi walionekana kuvutiwa zaidi na biashara ya muhogo ambapo kampuni ya Sino Light International Holdings ilionesha nia ya kununua tani 100,000 za muhogo mkavu kutoka Tanzania kila mwezi


Chanzo: Habari Leo
 
China mashitaka ya mauaji yanachukua dakika kama 10 hukumu inatolewa hapo hapo na mtu anayongwa baada ya siku moja! Wakimsifia sawa!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Acacia wakisusa wenzao wapo mlangoni wanabisha hodi.

ukikataa ukweli wewe ni mchawi..NDIO MAANA WATANZANIA WENGI NI WACHAWI.. na mchawi hawezi kuona tatizo, wala kutatua tatizo YUKO PAMOJA NA SHETANI. ndio maana watanzania wengi masikini
 
Anayepambana na rushwa anatoabhela za kununua madiwani? Ananunua wabunge ili wapitishe miswada mibovu!! Sisi wenye akili timamu hatuhadaiki!
 
Wamchangani wakishindwa kuona juhudi zinazofanywa na mh. rais, wa kimataifa watamtetea.
 
Binafsi sitaki kumpa sifa kila kukicha..nataka maisha bora kwanza.. hizo sifa zinafaa wakati wa kampeni.
 
Mnajadili upupu tu

Kuna kampuni hapo inataka kununua mihogo hamjaiona fursa hiyo?
Nilitegemea hicho ndo kiwe kiini cha mjadala
Mnaanza vijembe tena,hamchoki!!
 
Haio madiwani waliwanunua kwa mavii!??? Yanii alivyodanganya kuhusu acacia nimepoteza imanii naee jumlaa... viongozii wapendaa sifaa tuu hakuna cha maana....yanii wanatia hasiraa sanaaa... Umeme siku ya pilii nchi nzima unazingua... li inchii la kiboya sanaaa
 
Mnajadili upupu tu

Kuna kampuni hapo inataka kununua mihogo hamjaiona fursa hiyo?
Nilitegemea hicho ndo kiwe kiini cha mjadala
Mnaanza vijembe tena,hamchoki!!

maisha bora yanaanzia kwako kwanza... umeifanyia nini Tanzania kabla ya kufikilia imekufanyia nini? stop being a looser
 
Back
Top Bottom