Rais Magufuli azindua ghala na mitambo ya gas ya LPG ya Taifa Gas Tanzania Ltd

Ni jambo la ajabu sana kujifanya tumesahahu au hatujui role ya Rostam kwa nchi fulani za middle east..huyu mtu hatufai!! inakuwaje bado anapewa security clearance hata baada ya mabaya yote aliyofanya dhidi ya nchi hii??? watanzania tuna shida kubwa pengine ni kwa sababu akili ya hao tuliowatask masuala ya usalama wetu akili yao imedhoofu kwa miaka sasa! kila mahali makosa..mara arab contractors ya Misri ndio wanajenga rufiji dam..watu ambao hawajaridhia kabisa Tanzania kutumia maji ya ziwa victoria kuweka miradi ya maji inayoendelea leo, halafu unawapa wakujengee dam una uhakika hiyo ndiyo kazi pekee watafanya wakiwa hapa nchini???
Kwa kifupi hata hilo jina alilotumia Rostam kuita TAIFA GAS wamzuie..huwezi ita biashara yako binafsi jina TAIFA/NATIONAL akili ya watanzania sijui hata huwa inafikiria nini, tuna timu ya Taifa inaitwa TAIFA STARS, neno Taifa linapaswa litumiwe kwa niaba ya NCHI, au kwa kitu chochote chenye umiliki wa nchi sio ovyo ovyo tu kama hivyo alivyoita Rostam biashara yake!

👍
 
Mkuu wa mkoa Makonda anafanya utambulisho na am3muita DC Msafiri aje aelezee miradi ya wilaya kwa sababu akielezea yeye watu watadai anataka JIMBO.
1.Alitaka jimbo la Misungwi akamchafua Gwajima akatolewa K.O
2.Kwasasa anataka Jimbo la Kawe ila hawezi kupata pamoja na harakati zake zote anazofanya za kampeni za chini kwa chini labda Baba yake aligawe jimbo ndio anaweza akapata.
3.Hilo la Kusema kwamba akiongea ataonekana anataka jimbo ni kutaka kujisafisha tu na kampeni zake anazofanya jimbo la kawe.
 
Karibu!
Mh Rais Magufuli anafungua ghala na mitambo ya gas ya kampuni ya Taifa gas Tanzania ltd, wilayani Kigamboni jijini Dsm.

Hafla hiyo imehudhuriwa na waziri wa nishati mh Medadi, RC Makonda pamoja na mwekezaji Rostam Aziz.

Mkuu wa mkoa Makonda anafanya utambulisho na am3muita DC Msafiri aje aelezee miradi ya wilaya kwa sababu akielezea yeye watu watadai anataka JIMBO.

Msafiri amemshukuru Rais Magufuli kwa uzalendo na uongozi uliotukuka.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Taifa Gas Rostam Aziz amemsifia Rais Magufuli kwa kutokomeza tabia ya " Ujanja Ujanja" miongoni mwa wafanyabiashara.
Rostam Aziz amesisitiza kuwa Rais Magufuli ni rafiki wa kweli wa sekta binafsi na amewataka wawekezaji duniani kote kuja Tanzania kwani sasa kumenoga.

Waziri wa nishati anasema maghala haya ndio makubwa zaidi barani Afrika!

Rais Magufuli anawashukuru wakazi wa kigamboni kwa kuiunga mkono serikali, pia amesema mbunge wao ndugu Ndugulile hayupo hapo kwa sababu ana jukumu muhimu bungeni la kuipigia kura bajeti ya serikali na kwamba aliomba ruhusa na amemruhusu.
Rais Magufuli amempongeza Rostam Aziz kwa uwekezaji huu mkubwa ambao umetoa ajira kwa wananchi na pia kulipa kodi na ana imani kodi itazidi kuongezeka kadri uwekezaji unavyokua.
Rais Magufuli amewataka watendaji wa serikali kutowazongazonga wawekezaji na kujifanya wanajua sana kudhibiti wakati wao kazi yao ni kukusanya revenue, hivyo amewataka washirikiane vizuri.

Rais pia amewataka wananchi kuachana na matumizi ya mkaa na badala yake waanze kutumia gesi. Amewataka wawekezaji wa gesi kupunguza bei za mitungi ili wananchi waweze kuimudu.
Mwenzake Filipe Nyusi wa Msumbiji anazindua ujenzi wa liquefaction plant ya US $25 billion, yeye anahangaika na wezi akina Rostam wakati mradi wetu wa gesi umekwama kwa ufisadi wa CCM
Anadarko to invest $25bn in Mozambique gas project
 
Nimemuona Rostam Aziz, Mzee wa deal done seat ya mbele.
Rostam anajua Kula na vipofu na mambo yanazidi kumnyookea, e.g Caspian kule Brela ni kampuni ya ujenzi lakini inafanya kazi Migodini {Mwadui} huku akiendelea kugoma kulipa wafanyakazi wake Kwa ngazi ya migodini na hakuna anayetetea si serikali wala OTTU.,.? Caspian tajiri mkuu nafikiri yupo Iran kwenye utajiri mkubwa wa mafuta sasa tujitahidi kuunganisha dots kwenye hii LPG Yao na kuiacha LNG ya Lindi je kuna nini mbeleni?
 
Rostam anajua Kula na vipofu na mambo yanazidi kumnyookea, e.g Caspian kule Brela ni kampuni ya ujenzi lakini inafanya kazi Migodini {Mwadui} huku akiendelea kugoma kulipa wafanyakazi wake Kwa ngazi ya migodini na hakuna anayetetea si serikali wala OTTU.,.? Caspian tajiri mkuu nafikiri yupo Iran kwenye utajiri mkubwa wa mafuta sasa tujitahidi kuunganisha dots kwenye hii LPG Yao na kuiacha LNG ya Lindi je kuna nini mbeleni?
Hapo Mzalendo Kuliko Sisi ana MoU na huyu CIA/FBI agent.
 
Back
Top Bottom