Rais Magufuli azindua barabara ya Kaliua-Kazilambwa, aagiza ujenzi wa barabara nyingine 2 kuanza

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358


Rais Magufuli ameendelea na ziara nchini na leo yupo Mkoa wa Tabora kwa ajili ya uzinduzi wa barabara ya Kaliua-Kazilambwa.

Rais Magufuli ameambatana na viongozi wengine wa Serikali.

Matangazo ya moja kwa moja yanarushwa na TBC.

Magdalena sakaya(Mbunge wa Kaliua);

=>Nichukue fursa hii kukushuru sana mh rais kututembelea katika wilaya yetu.
Tunakuunga mkono kwa juhudi unazofanya kwa kuwatumikia watanzania.
Kwa kuwa umetutembelea leo tungependa uondoke na ujumbe huu. Barabara hii ya km 56 itatusaidia sana katika kilimo, tungetamani sana kilometa 48 zilizobaki ziweze kuunganishwa kwa lami.

=>Mh rais, uliahidi kupata km 5 na pamoja na km 2 alizoahidi raisi aliyepita katika mji wetu wa Kaliua.

=>Tatizo la maji ni kubwa sana kwa mji wa Kaliua. Tunaomba kwa namna ya kipekee uliangalie.

=>Mipaka iwekwe kwa wananchi wanaoishi karibu na eneo la mbuga ili kuondoa migogoro.

=>Tunaomba vijana waweze kupata mikopo ili kupambana na tatizo la ajira.

=>Ni matumaini yetu kuwa utatumbelea tena, Mungu akubariki sana.

===========

Rais Magufuli baada ya kukaribishwa;

=>Kaliua hoyeeeeee

=>Mh waziri Prof Mbarawa, waziri wa Elimu prof Ndalichako, Mwenyekiti wa kamati ya miundombinu, wabunge wa Tabora, wabunge wa kaliua, madiwani, maDC, wenyeviti wa bodi mbalimbali, wananchi mlioko hapa.

=>Nawashukuru viongozi wa dini, namshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufika hapa.

=>Nawashukuru sana kwa kunipa kura, nimekuja hapa kutoa shukrani zangu kwa kunipa kura.

=>Nimekuja hapa kuwathibitishia kuwa yale niliyowaahidi na hata ambayo sikuyaahidi nipo tayari kuyatimiza.

=>Tumetimiza kile tulichoyaahidi,

=>Barabara hii imejengwa kwa fedha za serikali bila kutegemea fedha kutoka nje.
Napenda kuwashukuru wizara kwa kazi kubwa ya kusimamia ujenzi barabara hii.

=>Asanteni sana waziri wa ujenzi, kwa kweli nimeimis hiyo wizara na najua ugumu wa kazi hii.

=>Kazi ya barabara imekamilika lakini kazi tuliyoanayo ni kuitunza.
=>Tukianza kuzidisha mizigo, barabara hii haitadumu

=>Kwa mujibu wa sheria ya barabara uzito wa juu ni tani gross weight 56

=>Niwaombe wananchi msichimbe mchaga wala kokoto kandokando ya barabara.

=>Nimuombe Meneja ukiona mtu anajenga nyumba katika hifadhi ya barabara, bomoa bila hata kutoa taarifa.

=>Kwa wananchi ambao wamejenga katika hifadhi ya reli wajiandae kasaikolojia, wajiandae kupisha ujenzi.

=>Mimi katika maswala ya sheria huwa sipindishi.

=>Najua kuna wanasiasa wanapindisha na kusema hakuna atakayebomoa tena wengine ni wanaCCM, Tena nawaambia mtakapoanza kubomoa anzeni na nyumba zao

=>Nimeamua kutoka Kigoma-Nyakanazi kwa barabara ili nione vipande vilivyobaki.

=>Nikuombe waziri, barabara ya kutoka Kaliua hadi Urambo haina lami.
Nataka ndani ya mwezi mmoja pawepo na kandarasi kwenye hiyo barabara yaani mwezi wa nane barabara hiyo ianze kujengwa kwa kiwango cha lami. Na amalize hicho kipande cha km28.

=>Nimezungumza na mfalme wa Kuwait na amekubali kutoa fedha.
=>Natoa mwezi mmoja na nusu barabara ya Chanya Nyaua km 84 kandarasi iwe imeanza.

=>Nataka mtu akitoka hapa kaliua asikanyage vumbi. Najua watu watasema huyu jamaa ni mkorofi kweli lakini mtu ukiwa mpole mambo hayataenda.

=>Suala la tumbaku; kama yalivyo mazao mengine yanaenda vibaya.
Serikali iliruhusu kodi nyingi, kodi zimeleta usumbufu.

=>Serikali ya awamu ya tano tumetambua haya matatizo, tumefuta baadhi ya kodi.
Nilimtuma waziri mkuu na wapo viongozi walishtakiwa siku hiyo hiyo.

=>Hatukujenga ushirika wetu kama inavyotakiwa, tulijenga ushirika kwa majizi, walaji.
Nimeenda kwenye ushirika mmoja, wanadaiwa sh bilioni 1.

=>Wapo watu walioandikiwa pembejeo hewa, tunafanya ukaguzi nchi nzima.
Tumekagua mikoa 11, tumekuta madai yaliyokuwa yanadaiwa ni bilioni 38

=>Hii ndiyo Tanzania, kila kitu ni hewa; nimeenda kule Kigoma nimekuta hata wakimbizi hewa. Nimeamua kushughulikia hizi hewa na kubakiza hii ya kupumulia tuu.

=>Kwahiyo serikali iko pamoja na ninyi.
=>Tabora ndiyo ilikuwa inaongoza kwa uhifadhi wa mazingira, leo tumeingiwa na ugonjwa wa kufyeka.

=>Na mkoa wa Tabora ulikuwa unaongoza kwa asali safi.

=>Na ndiyo maana hapa Tabora watu wanaongezeka kwa asilimia 5.6 tofauti na sehemu nyingine utakuta asilimia 2, ni kwasababu ya asali.

=>Nchi yetu tunaiua sisi wenyewe
Wapo watu wanawakaribisha watu wa wanyamapori na wengine ni wa CCM, nashukuru mliwanyima kura kwani hizo ni kura batili.

=>Tutafika mahali nchi yetu itakuwa jangwa, sijui tutahamia wapi. Ni lazima wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya mzingatie sheria.

=>Lazima tubadilike, mimi ni mtoto wa mkulima na mfugaji. Baba yangu alikuwa na ng'ombe 300 na mpaka juzi zilikuwa zimebakia ng'ombe 75. Na juzi nimeuza ng'ombe 50.Lazima tufuge kisasa.

=>Ni lazima wataalam wa ardhi waanze kupanga matumizi bora ya ardhi.

=>Na wale waliotaka km 20 kwenye pori, siwaongezei.

=>Katika bajeji ya mwaka huu tumefuta tozo za kilimo 80, ufugaji 7 na uvuvi 5.

=>Sasa iwe ni marufuku iwe ni marufuku, nataka wakuu wa mikoa wa mikoa, wilaya na wakurugenzi walielewe hili.

=>Tunafanya hivyo kwasababu mlituchagua tuwatumikie.

=>Na wale vijana na hata wazee wenye tabia ya kuwapa mimba wanafunzi wajiandae kufungwa miaka 30 ili kusudi hizo nguvu wakazitumie huko.

=>Serikali ninayoiongoza nitakuwa mkali kidogo.

=>Tumeanzisha mahakama maalumu ya kupambana wala rushwa na tutadili nao kikamilifu.

=>Huduma za afya tumeziongeza kutoka bajeti ya bilioni 31 hadi bilioni 250.

=>Natambua ndugu zangu wakulima wapo wanaohitaji maeneo ya kulima. Mkoa tuangalie namna ya kuwapatia.

Ninawashukuru sana kwa zawadi hasa ya asali, ngoja na mimi nikaijaribu nijue siri iliyo ndani ya asali.

Namshukuru sana mbunge wa hapa. Nawaomba wanaCCM mshirikiane naye kwani ni mchapakazi na maendeleo hayana chama.

Ni mara mia uwe mbunge wa CUF au CHADEMA anayefanya mambo ya CCM kuliko CCM anayefanya mambo ya CUF.

=>Na uchaguzi wa CCM najua umekaribia, niwaombe msitoe rushwa.

Niwashukuru sana ndugu zangu, Mungu awabariki.
 
Hivi Sakaya na kaliua wapi na wapi au ndo wahenga walivyosema kuwa ni chakula cha mwenyekiti uchwara.
 
Back
Top Bottom