Rais Magufuli azidiwa umaarufu na Mh.Tundu Lissu

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,073
114,571
Katika kipindi cha mwanzo wa mwaka 2017 umaarufu wa Rais wa Tanzania Dr.Magufuli umeonekana kushuka huku umaarufu wa Mbunge wa Singida na Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu ukizidi kuimarika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania

Utafiti niliofanya unaonyesha kuwa umaarufu wa Mh.Magufuli umeshuka na unaendelea kushuka japo kwa kasi ndogo,ukilinganisha na umaarufu wa Mbunge Tundu Lissu ambao unapanda kwa kasi kubwa

Kushuka kwa umaarufu wa Rais kumechangiwa na mambo kadhaa kubwa ikiwa ni ukiukwaji wa misingi ya katiba na sheria katika serikali anayoiongoza. Serikali ya Rais Magufuli imekuwa ikishutumiwa kukiuka katiba katika baadhi ya matamko na kukandamiza Uhuru wa kutoa maoni kwa kigezo cha uchochezi

Mengine ni:-
1.Kushindwa kuimarisha uchumi kinyume na matarajio huku mzunguko wa fedha ukiwa katika hali mbaya.
2.Kushindwa kuboresha maslahi ya watumishi wa umma ikiwa ni pamoja na Kushindwa kuongeza mishahara
3.Kushindwa kutoa ajira huku mahitaji ya watumishi katika sekta ya elimu na afya yakiwa makubwa
4.Ubutu wa kupambana na ufisadi huku akituhumiwa kwamba huenda serikali yake ikakumbwa na ufisadi zaidi kutokana na kubinya Uhuru. Pia Kushindwa kuwawajibisha baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi licha ya kuandamwa na kashifa za kutumia madaraka vibaya kwa wasaidizi wake. Jana Mbunge wa Chadema Mh.Selasini alihoji jumba la kifahali analomiliki Mkuu wa Mkoa wa Dar kutokuendana na kipato chake

Aidha umaarufu wa Mbunge wa Chadema Tundu Lissu kwa ujumla umesababishwa na ujasiri wake wa kutetea kufa na kupona misingi ya katiba sheria na haki za binadamu. Tundu Lissu amekuwa akikumbwa na misukosuko mingi ikiwepo kuwekwa ndani Mara kwa Mara lakini juhudi zake zimekuwa zikiendelea bila hofu ya kutiwa nguvuni.

Hivi karibuni Lissu amekuwa mmoja kati ya wanasheria wasomi wanaowania urais wa chama cha wanasheria wa Tanganyika
 
Hahahahahaha DW swahili inasikilizwa kwenye nchi zinazoongea kiswahili so kama umaarufu wa Lundu Lissu ni kwa nchi zinazoongea kiswahili sawa
bt si Duniani

Tundu anajitafutia matatizo tu anawezeje kuwa maarufu kuliko mnunuzi wa chama?
 
Mkuu,
Ni kweli ndo maana serikali inajaribu kubana kila eneo la wananchi kupata habari au kupashana habari maana serikali ya awamu ya tano chini ya mhimili wa dola (executives /state) ngazi zote imekosa mvuto na ushawishi wa kisiasa, kisheria, kimatendo na wananchi wanaamua kupeleka masikio na matamanio yao kwa upinzani, bunge na viongozi wa dini.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom