Rais Magufuli aweka jiwe la msingi ujenzi wa meli kubwa kuliko zote katika Maziwa Makuu: Ina uwezo wa kubeba abiria 1,200

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Rais John Pombe Magufuli leo anatarajiwa kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Meli kubwa na ya kisasa, yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 400. Meli hiyo itakuwa kubwa kuliko meli zote zilizowahi kutengenezwa katika maziwa makuu barani Afrika. Mkataba huo utatiwa saini na MSCL na Kampuni kutoka Jamhuri ya Watu wa Korea. Ujenzi huo unatarajiwa kuajiri vijana wapatao 400.

Aidha, Mikataba mingine I tahusisha: Ujenzi wa Chelezo cha kujengea meli; pamoja na ukarabati wa meli nyingine mbili za Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL) ambazo ni: MV Butiama inayobeba abiria 200 na tani 100 za mizigo, inayofanya route ya Mwanza - Ukerewe; pamoja na MV Victoria yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 200 za mizigo, inayofanya route ya Mwanza - Bukoba.

Updates:


DmJa0pXXgAE6dv9.jpg large.jpg


Meli mpya itakuwa na:
  • Urefu wa Mita 90; upana mita 17; kimo mita 10.9 (sawa na ghorofa 3).
  • Injini kubwa 2 za KW 1720; generator kubwa 2 za KVA 875 na generator ndogo ya KVA 100.
  • Speed (knots) ya 14 - 16.
  • Itapunguza masaa ya kwenda Bukoba (km 174) kutoka masaa 10 hadi 6 pekee.
  • Ni ya kwanza kutengenezwa na Serikali katika Ziwa Victoria tangu MV Serengeti mwaka 1988.
  • Itajengwa na Kampuni za Korea kwa kushirikiana na Suma JKT.
  • Gharama ya Mradi ni bilioni 88.76.
  • Itatumia muda wa miezi 24 kukamilika.
  • Ujenzi utafanyikia Mwanza South ambako ndiko kutakakojengwa Chelezo (Slipway).
  • Ujenzi utaajiri vijana wapatao 250.
Aidha, Chelezo itakayojengwa, itakuwa na:
  • Urefu wa mita 100.
  • Uwezo wa kubeba meli zenye uzito wa hadi tani 4,000.
  • Gharama ya Mradi ni bilioni 35.99.
  • Muda wa Mradi ni miezi 12.
Kwa kuwa, Meli itatengenezewa Korea na kuunganishiwa Mwanza; hivyo Mkandarasi atatumia miezi minne (4) kufanya usanifu (designing); miezi minne (4) kutengeneza; na miezi mitatu (3) kusafirisha vipande vya Meli kutokea Korea hadi Mwanza. Ikifika Mwanza, tayari Chelezo itakuwa imeshakamilika na hivyo uunganishaji utafanyika.

Vilevile, Mkataba mwingine ni Ukarabati wa MV Victoria inayofanya safari za Mwanza - Bukoba, iliyosimama kufanya kazi tangu mwaka 2014. Ukarabati utahusisha kuweka injini 2 mpya, generator mpya, vyumba vya kuongozea meli na vifaa vya uokozi. Mradi utagharimu bilioni 22.7.

Mwisho, kuna Mkataba wa Ukarabati wa Meli ya MV Butiama, inayofanya safari za Mwanza - Nansio (Ukerewe) na ambayo kabla ya kuharibika mwaka 2010, ndiyo iliyokuwa na kasi kuliko meli zote kubwa za abiria kwenye maziwa. Gharama ya ukarabati ni bilioni 4.897.

Jumla ya gharama ya Miradi hiyo ni bilioni 152.

Aidha, Serikali iko mbioni kuingia mikataba ya miradi mingine ya utengenezaji wa meli nchini, ambao uraweka jumla ya gharama za bilioni 279.

09752CB8-9A87-4245-B2AB-A3FB2FAA76BB.jpeg


Hotuba ya Rais Magufuli

Kwakuwa tumesimama basi tuwakumbuke ndugu zetu waliokufa kwenye ajali ya meli ya MV Bukoba miaka 22 iliyopita. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Amen

Ninajisikia faraja kubwa watanzania tunashududia utiaji saini wa meli hii kubwa, chelezo na ukarabati wa meli mbili.

Ninafahamu wakati tunatoa ahadi hii wapo watu walisema haitowezekana, kwasababu wanafahamu gharama za ujenzi wa meli na hasa gharama kubwa katika ziwa Victoria ambapo tulikuwa na chelezo isiyokuwa na uwezo wa kutengeneza meli kubwa kama hizi.

Ukarabati wa meli 2 za Mv Butiama na Mv Victoria utagharimu Shilingi Bilioni 27.61, tumeamua kufanya ukarabati mkubwa.Meli ya Mv Liemba iliyopo mkoani Kigoma nayo tumepanga kuikarabati

Zile tani zote zilizokuwa zikibebwa na Mv. Victoria ni mara mbili zaidi ya meli hii itakayokuwa ikibeba. Sifahamu hii meli itakuwa inaitwa jina gani lakini ndio ina beba.

Hii meli badala ya kutumia saa 10 hadi 12 kwenda Bukoba, sasa hivi hii itakuwa inatumia saa 6. Kwa hiyo inaweza ikawa inaenda na kurudi

Haiwezekani shirika liwe na meli 24, halafu wafanya kazi wake wakose mishahara, wakati wafanya kazi wa kwenye mitumbwi wanalipwa mishahara. Nitatoa shilingi bilioni 3.7 ya malimbikizo ya mishahara ndani ya wiki mbili.Nawahimizwa kuendelea kufanya kazi kwa juhudi vinginevyo mtazitapika fedha hizo

Watakao kuwa wanasimamia hapa hata ulinzi, Jeshi la Wananchi lazima liusike. Hii ni mara ya watanzania na fedha za watanzania, na tunataka hata msumali usiibiwe. Ukiuiba hata kama umeumeza ukautapike, kwasababu watanzania nao ni wajanja

Tupendane tuujenge uchumi wa pamoja, hakuna mtu atakayekuja kuujenga uchumi wetu, tumechelewa. Nchii hii ina mali nyingi hatukupaswa kuwa masikini hivi .Tusikwepe kodi ndugu zangu watanzania, kodi ni msingi wa maendeleo ya Tanzania

Tunatekeleza miradi hii yote kwa manufaa ya watanzania wote, tumeamua na hatutarudi nyuma, watanzania tunaweza

Ukishakuwa kiongozi ni msalaba na hasa uongozi wa awamu yangu, ni msalaba nasema kwa dhati. Ukae mguu pande na mwingine sawa, kwasababu hata na mimi mguu upo pande na mwingine upo sawa. Ni lazima tutimize malengo ya wananchi

======

Taarifa kwa vyombo vya habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 03 Septemba, 2018 ameshuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa meli mpya, chelezo na ukarabati wa meli za Mv Victoria na Mv Butiama katika ziwa Victoria kati ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania (MSCL) na Kampuni za kutoka nchini Korea ambazo ni M/S Gas Entec Co. Limited, Kangnam Corp, M/S STX Engine Co. Ltd, Saekyung Construction Ltd, KTMI Co. Ltd, zinazoshirikiana na kampuni mbili za Kitanzania ambazo ni Suma JKT na Yuko’s Enterprises.

Hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo imefanyika katika bandari ya Mwanza Kusini Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Balozi wa Korea hapa nchini Mhe. Song Geum-young, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jen. Venance Mabeyo, Viongozi wa Mkoa wa Mwanza na Mara, Wabunge na wananchi.

Meli mpya itajengwa kwa muda wa miezi 24 kwa gharama ya shilingi Bilioni 88.764, ikiwa na urefu wa mita 90, upana mita 17, kimo mita 10.9, uwezo wa kuchukua abiria 1,200, mizigo tani 400, magari madogo 20, na itakuwa na uwezo wa kwenda kasi zaidi (ambapo itatumia saa 6 ikilinganishwa na saa 12 za meli zilizopo) kati ya Mwanza na Bukoba na itakuwa ndio meli kubwa kuliko zote hapa nchini na katika Maziwa Makuu.

Chelezo (mahali pa kujengea na kutengenezea meli) itajengwa kwa muda wa miezi 12 kwa gharama ya shilingi Bilioni 35.99 na itakuwa na urefu wa mita 100.

Katika mradi huu, meli ya Mv Victoria yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 200 za mizigo ambayo ilisimama kutoa huduma tangu mwaka 2014 kutokana na ubovu itakarabatiwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 22.712, na meli ya Mv Butiama yenye uwezo wa kuchukuwa abiria 200 na tani 100 za mizigo ambayo ilisimama tangu mwaka 2010 kutokana na ubovu itakarabatiwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 4.897.

Kaimu Meneja Mkuu wa MSCL Bw. Eric Benedict Hamissi amesema pamoja na ukarabati wa meli hizo 2, MSCL itakarabati meli nyingine 3 ambazo ni Mv Serengeti na Mv Umoja katika Ziwa Victoria na Mv Liemba iliyopo katika ziwa Tanganyika.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Selemani Kakoso amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa dhamira yake ya kuimarisha usafiri wa majini katika maeneo mbalimbali hapa nchini na amewahakikishia Watanzania kuwa miradi na fedha za utekelezaji wa miradi hiyo zimepitishwa na Bunge, na kwamba sio kweli kuwa Serikali inatumia fedha bila kuidhinishwa na Bunge.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe ameahidi kusimamia utekelezaji wa mradi huo ipasavyo na kwamba wizara yake imeanza kuchukua hatua za kuongeza ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam ikiwemo kuongeza kiwango cha mizigo kutoka tani Milioni 16.2 za mwaka 2017/18.

Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini wa utekelezaji wa miradi hiyo Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na kuanza kwa ujenzi meli mpya na chelezo pamoja na ukarabati wa meli za Mv Victoria na Mv Butiama ambazo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015.

Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Wabunge waliopitisha bajeti ya Serikali iliyowezesha kuanza kwa utekelezaji wa miradi hiyo ambayo itasaidia kukabiliana na tatizo kubwa la usafiri wa majini katika ziwa Victoria baada ya Mv Bukoba kuzama mwaka 1996 na Mv Butiama na Mv Victoria kusimama kutoa huduma.

Kuhusu madai ya wafanyakazi wa MSCL wanaodai kutolipwa mishahara kwa miezi 27, Mhe. Rais Magufuli ameahidi kuwa Serikali itatoa shilingi Bilioni 3.7 za kuwalipa wafanyakazi hao ndani ya wiki mbili lakini amemtaka Kaimu Meneja Mkuu wa MSCL kusimamia vizuri utendaji na mapato ya kampuni hiyo pamoja na kudhibiti wizi wa mafuta ambao hufanywa na wafanyakazi.

“Fedha hizi shilingi Bilioni 152 zilizotolewa kwa ajili ya miradi hii zimetokana na kodi za Watanzania, nataka kampuni hii ifanye kazi kwa ufanisi na izalishe gawio kama mashirika mengine ya Serikali, Kaimu Meneja Mkuu ukadhibiti mapato na wizi wa mafuta, anza kutumia tiketi za kielektroniki” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Mwanza

03 Septemba, 2018
 
Huyu bwana sijui anadhani yeye bado ni waziri wa miundombinu na uchukuzi?!

Uchumi wa nchi haujengwi kwa kutoa kipaumbele kwenye miundombinu pekee japo ni kweli miundombinu ni ya muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi.

Utanunua mandege, treni na kujenga meli ila mwisho wa siku utaacha wananchi wakiwa hohehahe na watashindwa hata kutumia hiyo miundombinu kujieletea maendeleo maana mifukoni wakavu, hawakoposheki na hata wale wanaokesheka wanalipa mikopo yao kwa tabu, n.k.

Uvuvi mmeuvuruga, kilimo mmekipuuza, ajira kwa manati,watu biashara zimedorora, mikopo hailipiki na mabenki faida zinaporomoka.Sasa hizi ndege, meli na treni zinazopewa kipaumbele kuliko vitu vingine vyote ndio vitu pekeee vitavyomuinua mtanzania huyu?!

Hata huko vijijini ukijenga mabarabara mazuri kila mahali hizo barabara haziwei kuwa na tija yoyote katika uchumi wa nchi kama huko vijijini kilimo kimedoraro.

Barabara nzuri vijijini huku mazao ya kusafirsha hakuna ni kazi bure kiuchumi.

Awamu hii tunaelekeza fedha nyingi sana kwenye miundombinu na kusahau kabisa sekta nyingine jambo ambalo sidhani kama ni sahihi.
 
tenda imetangazwa lini? Na makampuni gani yalishindanishwa!
Tenda ilishatangazwa tangu mwaka jana na ujenzi ulikuwa uwe umeanza mwanzoni mwa mwaka huu wa 2018 lakini inaonekana Rais alilipotezea lile Kampuni la Kikorea baada ya kuwepo madai ya kuongezeka kwa gharama za ujenzi hata kabla ya ujenzi kuanza.
Naona Wakorea walijifunza kuwa, huyu jamaa wakimletea ujuaji atawatolea nje, ndo maana walinywea. Unakumbuka hivi karibuni alikuja Kiongozi kutoka South Korea? So ndo hivyo.
 
Huyu mtu anadhani yeye bado ni waziri wa miundombinu na uchukuzi.

Uchumi wa nchi haujengwi kwa kutoa kipaumbele kwenye miundombinu pekee.

Utanunua mandege, treni na kujenga meli ila mwisho wa siku utaacha wananchi wakiwa hohehahe na watashindwa hata kutumia hiyo miundombinu kujieletea maendeleo.
Waziri ni msaidizi wa Rais
Nafikiri unajua maana ya neno msaidizi

Cha muhimu ni kwamba pesa inatumika kwa maendeleo ya nchi huo upuuzi mwingine kwamba anafanya kivipi tunawaachia vigagula
 
Back
Top Bottom