Rais Magufuli aweka Jiwe la Msingi Mahandaki Reli ya Kisasa

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,685
11,987
Anatatua shida za Wananchi kijiji kwa kijiji

Pia ataweka jiwe la msingi ujenzi wa reli ya kisasa kutoka kilosa hadi makutupora

===

Rais Magufuli amekwishafika eneo la uwekaji wa jiwe la msingi ambapo amepewa maelezo ya kina juu ya Mahandaki hayo na namna ambavyo yatakavyofanya kazi.

Rais ameshiriki katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Mahandaki katika reli ya kisasa pamoja na kupiga picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu ya tukio hilo.

Rais ameshafika tayari kwa ajili ya kuongea na Wananchi kuhusu tukio la uwekaji wa jiwe la msingi la Mahandaki reli ya kisasa ambapo Wimbo wa Taifa na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeimbwa.

Viongozi wa Dini ya Kiisalamu na Kikristo wamekaribishwa ili kufungua tukio hili kwa dua ambapo kwa pamoja wamemshukuru Mungu pamoja na kumuombea mafanikio Rais Magufuli na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amepata nafasi ya kuwatambulisha viongozi waliohudhuria katika tukio hili pamoja na kumshukuru na kumkaribisha Rais katika tukio hilo. Zaidi ya hayo Mkuu wa Mkoa ameeleza baadhi ya miradi na mafanikio yaliyotelekezwa na awamu ya tano.

Mhandisi na mtendaji Mkuu wa TANROADS Mfugale amepata nafasi ya kuzungumza na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu ujenzi huu wa SGR. Ameeleza kuwa Mradi huu unatarajiwa kukamilika Mwezi januari mwaka 2021.

Zaidi ya hayo, Viongozi mbalimbali Wabunge na Mawaziri wamepata nafasi ya kuzungumza ambao wote kwa pamoja wameendelea kumpongeza Rais Magufuli kutokana na maendeleo na miradi mbalimbali aliyoifanikisha katika mkoa wa Morogoro.

Rais Magufuli: leo ni siku muhimu sana. Nimeweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mahandaki manne yenye urefu wa km 2.7 ukijumlisha barabara ya juu ya aina yake ya nusu kilomita itakayojengwa hapa, sasa barabara za juu haziko Dar es Salaam tu hata Kilosa zipo

Amesema mara yake ya kwanza kuona barabara ya kupita chini ya Mlima aliiona Uingereza alipokuwa anasoma, lakini amefarijika sasa kuna reli ya hivyo Tanzania

Amesema wapo waliomuona anaota wa kuwa aliposema nataka kujenga reli. Amewapongeza viongozi wote wa dini na wanachi kwa ujumla kwa juhdui zao za kufanikisha reli hiyo iliyogharimu Tsh Trilion 6.05

Amesisitiza kutumia fedha za ndani, kutumia cash kukamilisha ujenzi huo

Amesema anatambua matatizo yanayowakumba watu wa maeneo hayo kuwa ni migogoro ya mashamba, ambayo ni kwa kuwa mashamaba mengi yamechukuliwa na matajiri na wameshafuta mashamba zaidi ya 40,

Alichotaka kifanyike kwa wilaya ya Kilosa, wajadili jinsi ya kuyagawa bure mashamba yaliyofutwa, mashamba hayo yatagawiwaw kwa wananchi masikini. Amesema kuwa migogoro hiyo inawahusisha kwa kiasi kikubwa viongozi

Magufui aagiza ndani ya siku sabab mashamba mengine yaliyobaki wayafute na kisha kuyagawa kwa raia.

RAIS ATAJA SABABU ZA KUWAFUKUZA VIGOGO MTERA
Amesema viongozi walikuwa wanafungulia maji bwawa la Mtera ili waseme kina cha maji kimepungua, ili umeme uwe wa mgao ili waweze kuuza majenereta

Pia amezungumzia matatizo mengine ikiwemo kuuza vitu ghafi na kuagiza vitu kama tomato sauce, kwenye upande wa pamba tulikuwa tunauza pamba ikiwa ghafi ambayo walionunua walitengeneza nguo na kuvaa kisha kuturudishia mitumba.

Katika uzinduzi huo, aliyekuwa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali alikuwepo na alimsimfu Magufuli kwa kutengeneza miradi mbalimbali
 
Rais John Magufuli yupo live Tbc, Itv, kuzindua Uwekaji jiwe la Msingi Mahandaki Reli ya kisasa
 
Rais ni binadamu Kama sisi Kuna wakati anajisikia kutia maneno kwa lengo la kuharmonise Hali tu.

Hata waliolengwa na hiyo kauli wenyewe wanajua ule ulikua utani.
Acha nao waisome namba. Tu;ipokuwa tunakandamizwa upinzani mlikuwa mnacheka. Nanyi isomeni namba!
 
Huku ni kupoteza muda na kuonyesha desperation za kijinga...jiwe la msingi lilishawekwa sasa ...hadi madaraja na mahandani ambayo ni sehemu ya mradi yanahitaji kuwekewa uzinduzi ...tunachekesha sasa

Reli ya tazara ina madaraja na mahandaki mengi kuliko reli ya kati ya sasa ukizingatia imepita kwenye eneo la nyanda za juu lakini hata siku moja hatusomi kuwa kulikuwa na uzinduzi wa mahandaki ...zaidi ya nyerere kuwa anatembelea tu mradi mara kwa mara
 
Huku ni kupoteza muda na kuonyesha desperation za kijinga...jiwe la msingi lilishawekwa sasa ...hadi madaraja na mahandani ambayo ni sehemu ya mradi yanahitaji kuwekewa uzinduzi ...tunachekesha sasa

Reli ya tazara ina madaraja na mahandaki mengi kuliko reli ya kati ya sasa ukizingatia imepita kwenye eneo la nyanda za juu lakini hata siku moja hatusomi kuwa kulikuwa na uzinduzi wa mahandaki ...zaidi ya nyerere kuwa anatembelea tu mradi mara kwa mara
Umenena vyema sana Mkuu! Mungu awabariki Wazazi waliojinyima wakakulipia ada
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom