darcity
JF-Expert Member
- Jul 20, 2009
- 9,038
- 17,933
Baada ya Serikali kukusanya kodi mwezi Disemba na kufikia trilion 1.4 , Januari trilion 1.079, February trilion 1.040, March trilion 1.3,April trilion1.035 na mwezi May trilioni 1.032, serikali iangalie namna ya kumsaidia mjasiriamali mdogo ili aweze kufanya biashara zake ikumbukwe kwamba mafanikio makubwa ya awamu ya nne ya JK katika makusanyo ya kodi kutoka Tsh Billioni 177 Ya BWM kwa mwezi mpaka Billion 900 kwa mwezi (tofauti ya billion 773 kwa mwezi,sawa na ongezeko la asilimia 408.5%) kwa mwezi inatokana na serikali hiyo kuwawezesha wajasiliamali wadogo kufanya biashara katika mazingira mazuri.
Wastani makusanyo ya JPM kwa miezi sita ni trilioni 1.14 kwa mwezi ambayo ni sawa na ongezeko la Tsh billioni 240 kwa mwezi ambayo kimsingi yameongezeka kutakana na jitihada za serikali kubana mianya ya ukwepaji kodi na madeni ya wadaiwa wa kodi.
Hivyo serikali iangalie namna ya kuwajengea uwezo wajasiriliamali wadogo kwani wao ndio wanaweza kuwa wawekezaji wazuri wa viwanda vidogo vidogo badala ya kuwakamua mitaji yao kwani figure za makusanyo bado zinacheza sana baina ya mwezi mmoja na mwengine.(sometime 1.0, sometime 1.3)