utaifakwanza
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 14,193
- 2,812
kamuombe msamaha mkuuDuh,hakika tuliomnyima kura tutapata laana kama ataendelea hivo hadi mwisho
kamuombe msamaha mkuuDuh,hakika tuliomnyima kura tutapata laana kama ataendelea hivo hadi mwisho
Bora kamchomoa yule ustadh pale bandariXafi xana,ha ha ha
Rais Dk. John Pombe Magufuli aipiga chini Bodi ya TPA, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) Bw. Awadhi Masawe. Pia amemchomoa Katibu Mkuu wizara ya Uchukuzi Dk. Mwinjaka na kamsimamisha kazi. Pia baadhi ya wafanyakazi wa TPA na TRA wamesimamishwa kwa uchunguzi zaidi.
Massawe aliteulia na Samwel Sitta kushikila nafasi ya Mhandisi Madeni Kipande aliyesimamishwa kwa tuhuma za utendaji mbovu ili kupisha uchunguzi.
Rais Magufuli amemtimua Mkurugenzi Mtendaji Bandari TPA Awadhi Masawe na mwenyekiti wa bodi ya TPA Prof. Msambichaka na watendaji kadhaa kwa kushindwa kazi.
Aidha amemtimua Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi kwa kushindwa kuisimamia TRL.
Taarifa zaidi nawaletea soon...
Nakumbuka wakati wa kampeni mgombea wa UKAWA Edward Lowassa alisema "Uongozi ni kufanya maamuzi, ni bora ukafanya mwamuzi ukakosea kuliko kutofanya".
Rais Magufuri anafanya kile ambacho kinatakiwa, "MAAMUZI". Maamuzi afanyayo kiongozi humfanya ajipambanue yeye ni mtu wa aina gani.
kipande ndio alikua mtu sahihi na bandari ilikua infanya kazi vzr nadhan maguful amrudishe kipande enzi zake bandari ilikua inafanya kwa ufanisi '''relatively'"'
Duh uteuzi wa mkurugenzi wa bandari ulifanywa na Dr Mwakyembe kumbe hata yeye ni zero.
Pasipo juhud za upinzani na Lowassa kukatwa jina haya yote tusingeapata. Magufuli hakuwa chaguo la mkwere na ndo maana jamaa anafanya yale yote ambayo watanzania walitegemea kuyapata nje ya ccm. Usijutie mkuu...Najutia sana kumpa kura yangu Lowassa! magufuli 2020 panapo uhai nakupa kura yangu
Ukweli nausema. Namuunga mkono Rais Magufuli na Serikali yake kwa mapambano dhidi ya ufisadi,rushwa na dhuluma waliyoyaanzisha. Nawatakia kila lililo jema katika mapambano yao. Lakini, nchi si TRA na Bandari tu. Na wala si TRL tu. Nchi ni wananchi.
Fukuzafukuza na shtakishtaki inayoendelea kutokea TRA,Bandari na TRL si mwarobaini wa nchi nzima. Nchi si Dar es Salaam tu ambapo mambo yote yanayoendelea sasa yanafanyika huku. Dar es Salaam ni mkoa mmojawapo tu wa Tanzania.
Watanzania wana imani kubwa na Serikali yao. Bado wanaisubiri. Wanaisubiri kwakuwa yanayoendelea sasa hayawafaidishi moja kwa moja. Hayawapi malazi, chakula wala mavazi. Wananchi wanataka huduma. TRA,Bandari na TRL zisimkwamishe Rais kuwafikia wananchi wote.
Baraza la Mawaiziri liundwe na kazi ifanywe. Kuna maswali ya Wabunge yanasubiri kujibiwa kwa tafiti hapo Januari. Mawaziri watapata muda gani kutafakari na kuyajibu maswali? Na kadhalika na kadhalika.Muda unataradadi!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam