Rais Magufuli awatimua Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mwenyekiti wa Bodi na Katibu Mkuu Uchukuzi

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
attachment.php

Waziri Mkuu,Majaliwa akionesha ripoti ya Bandari ya DSM iliyobaini mianya-ukwepaji kodi ya Makontena 2,387

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli, amemtimua Mkurugenzi Mtendaji wa Bandari (TPA) Awadhi Masawe na mwenyekiti wa bodi ya TPA Prof. Msambichaka na watendaji kadhaa kwa kushindwa kazi.

Aidha amemtimua Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi kwa kushindwa kuisimamia TRL.

Taarifa zaidi nawaletea soon...

Rais Dk. John Pombe Magufuli aipiga chini Bodi ya TPA, pia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) Bw. Awadhi Masawe kasimamishwa. Pia ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wizara ya Uchukuzi Dk. Mwinjaka na kamsimamisha kazi. Pia baadhi ya wafanyakazi wa TPA na TRA wamesimamishwa kwa uchunguzi zaidi. Amewambia Polisi wote hao wawekwe chini ya Ulinzi.

Massawe aliteulia na Samwel Sitta kushikila nafasi ya Mhandisi Madeni Kipande aliyesimamishwa kwa tuhuma za utendaji mbovu ili kupisha uchunguzi.
attachment.php
attachment.php
Rais John P. Magufuli leo amevunja Bodi ya Bandari ya Jijini Dar es Salaam, kutokana na kashfa ya upotevu wa makontena ulioisababishia Serikali hasara ya mabilioni ya Shilingi.

Mbali na kuvunja bodi hiyo, pia ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhandisi Prof. Joseph Msambichaka na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Shaaban Mwinjaka.

Maamuzi hayo yametolewa Jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, kwa niaba ya Rais ambapo amenukuliwa na FikraPevu akisema maamuzi hayo ya Rais yamekuja muda mfupi baada ya kubaini kasoro nyingi za kiutendaji kwa watumishi hao wa Serikali.

Pamoja na mambo mengine, amesema Rais amewasimamisha kazi maofisa nane kutoka Bandari ya Dar es Salaam baada ya kubainika walihusika kwa namna moja ama nyingine katika sakata hilo.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, mara baada ya agizo hilo, ameagiza wahusika wote wakamatwe na wawekwe chini ya ulinzi ili kusaidia upelelezi ikiwa ni pamoja na kueleza makontena yaliyopotea yalikuwa ya nani na yalikuwa na thamani ya shilingi ngapi.

Watuhumiwa hao watatakiwa kuwezesha makontena hayo yaweze kulipiwa kodi kutokana na awali kutolipiwa kodi.

Katika ziara aliyoifanya katika Shirika la Reli Nchini (TRL), Waziri Mkuu alibaini matumizi mabaya ya fedha ya Sh.Bilioni 13 nje ya utaratibu ambao uchunguzi unakamilishwa kwa waliohusika.

Massawe aliteulia na Samwel Sitta kushikila nafasi ya Mhandisi Madeni Kipande aliyesimamishwa kwa tuhuma za utendaji mbovu ili kupisha uchunguzi.....

Soma zaidi =>Rais Magufuli awasimamisha kazi Mkurugenzi, M/kiti wa Bodi ya Bandari (TPA) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi
 

Attachments

  • Bod Bandari.jpeg
    Bod Bandari.jpeg
    21.2 KB · Views: 19,114
Duh uteuzi wa mkurugenzi wa bandari ulifanywa na Dr Mwakyembe kumbe hata yeye ni zero.
 
attachment.php

Waziri Mkuu,Majaliwa akionesha ripoti ya Bandari ya DSM iliyobaini mianya-ukwepaji kodi ya Makontena 2,387

Rais Dk. John Pombe Magufuli aipiga chini Bodi ya TPA, pia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) Bw. Awadhi Masawe kasimamishwa. Pia ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wizara ya Uchukuzi Dk. Mwinjaka na kamsimamisha kazi. Pia baadhi ya wafanyakazi wa TPA na TRA wamesimamishwa kwa uchunguzi zaidi. Amewambia Polisi wote hao wawekwe chini ya Ulinzi.

Massawe aliteulia na Samwel Sitta kushikila nafasi ya Mhandisi Madeni Kipande aliyesimamishwa kwa tuhuma za utendaji mbovu ili kupisha uchunguzi. Baadae Kikwete akampandisha kutoka kaimu hadi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA).
attachment.php
attachment.php
 

Attachments

  • IMG-20151207-WA0017(1).jpg
    IMG-20151207-WA0017(1).jpg
    60.2 KB · Views: 28,083
  • IMG-20151207-WA0018.jpg
    IMG-20151207-WA0018.jpg
    37.5 KB · Views: 26,902
  • CVn7a0sXIAAosbU.jpg:large.jpeg
    CVn7a0sXIAAosbU.jpg:large.jpeg
    23.6 KB · Views: 11,823
safisha nchi baba, kabla ya siku ya usafi tarehe 9 desemba.

Tena ikiwezekana peleka mswada bungeni kila 9 desemba inapokaribia usafi wa namna hii ufanyike kuanzia mawizarani na taasisi zote za umma, halafu tunamalizia na mitaro ya maji machafu mitaani kwetu.

Eti uhuru, wa nchi ipi? Tanzania haijawahi kutawaliwa, labda Tanganyika
 
Back
Top Bottom