Rais Magufuli awateua Dkt. Mpango kuwa Waziri wa Fedha na Prof. Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje

Hongera zao!

Kwa kuwajulisha history vijana wetu ya Wizara hiyo

Mpaka sasa Dr Mpango ndio Waziri alieshika Wadhifa huo kwa muda mrefu zaid mfululizo tangu tupate uhuru

Waziri wa fedha wa kwanza Mzawa ni Hayati Paul Bomani

Waziri wa fedha wa kwanza kujiuzulu/kufukuzwa kwa kutokubaliana na Bosi wake kimsimamo ni Mzee Edwin Mtei

Aliekaa muda mfupi zaid ni Luteni Kanali mstaafu Jakaya Kikwete

Walioshika wadhifa huo kwa vipindi tofauti kwa maana ya kuingia na kutoka na kurejea tena ni Cleopa David Msuya na Prof Kighoma Malima

Waziri wa Fedha alieshika wadhifa huo chini ya Marais wawili tofauti ni Prof Malima, alikuwa Waziri wa Mwisho wa Mwl Nyerere na Mzee Ally Hassan Mwinyi

Zakia Hamdan Meghji ndio Waziri wa fedha wa kwanza Mwanamke hapa nchini

Mawaziri waliofariki wakiwa bado ni mawaziri wa fedha ni Steven Kibona na Mh Mgimwa

Aliejiuzulu kwa tuhuma ya Wizi ni Prof Simon Mbilinyi

Basil Mramba ndio Waziri wa fedha wa kwanza kupatikana na hatia ya ubadhirifu Mahakamani na kufungwa gerezani

Itafuata Wizara ya Ulinzi bila shaka kama style hii ya kutangaza kidogo kidogo itaendelea
Mkulo hujamtaja

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Huyu Kabudi si ndiyo huyu huyu amepita bila kupingwa, duh!! ama kweli HAKI Tanzania haipo kabisa.
 
Back
Top Bottom