Rais Magufuli awataka CHADEMA, Cuf, ACT, CCM, NCCR nk kuteua wagombea wazuri kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,448
Rais Magufuli amesema serikali za mitaa ndio chachu ya maendeleo katika sekta zote hivyo amevitaka vyama vya siasa kuteua wagombea wazalendo na waadilifu.

Rais Magufuli amesema maendeleo hayana vyama hivyo iwe Chadema, Cuf, Act, CCM na vyama vingine vya siasa viwe na uzalendo wa kutuletea wagombea wanaotosha.

Kadhalika amewataka wananchi kuwa makini wakati wa kuchagua na kuwakwepa wagombea wababaishaji.

Chanzo: Star tv!

Maendeleo hayana vyama!
 
Mda si mrefu anatoa ushauri kwa msajili wa vyama vya siasa, kwamba huyu hafai na yule anafaa, yaani yeye ndo anawashauri mzalendo ni nani kwenye vyama vyote.
 
Kitu ambacho wengi hatutaki kukubali ni kwamba ktk sifa Akili timamu kwa mgombea na mpiga kura tumeteleza kwa kutokuwa na njia ya kuwapima wagombea wetu hivyo kumpelekea wenzetu hawa wenye ulemavu wa akili kuchaguliwa mpaka kufikia level ya juu kbs. Pia kuna kundi kubwa la wapiga kura ukilitazama kwa haraka unagundua ni kundi la walemavu wa akili tena linashiriki siasa vizuri na inawezekana kwa Sasa ni kundi tawala kbs. Madhara yake ndio haya ubaguzi Ukabila matusi kejeli ujinga wizi wao wao wanaona sifa tu. Hawajui hata maana wananchi na serikali wala haki za raia. Tuondoeni Hawa vichaa wametuzidi kete kwasasa tukiendelea kufikiri kwamba wanaakili timamu tutashtuka nchi imeshaharibika
 
Huyu Mwamba inatakiwa tumpe hata miaka 30 hv atunyoshee nchi Kwanza, badae ndo awaachie wala chipsi:)
Hapana utufanye tuwe zaidi ya Zimbabwe! Kwani sasa hata nyumba zinskosa wapangaji wagu wana banana kwenye nyumba vya uswahilini . Baba , mama watoto.
Akiondoka baada ya hiyo miaka 30 manuka fame itakuwa tupu kama Zimbabwe
 
Back
Top Bottom