Rais Magufuli awashangaa CCM na wananchi wa Iringa mjini kwa kutompa ubunge Dr. Mahiga

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,891
141,824
Rais Magufuli ameshangazwa na CCM pamoja na wananchi wanachama ambao walishindwa kuona umuhimu wake alipokuja kuomba ubunge wakati wa kura za maoni.

Amesema matokeo yake ubunge ukapotea na jimbo likakosa mtu makini wa kutekeleza ilani ya CCM na kuwaletea wananchi wa Iringa mjini maendeleo.

Rais Magufuli amesema kwa kutambua umuhimu na uimara wa Dr. Mahiga aliamua kumpa ubunge na uwaziri kwa manufaa ya wananchi wa Iringa mjini na taifa kwa ujumla.

Chanzo: TBC habari
 
Mtu makini kama huyu angepotelea tu kwenye anga za kimataifa,badala ya kulinufaisha taifa.
 
Huyu hajui ni muda gani yupo kwenye ziara za Serikali na zipi za kichama.
Sasa hapo mbunge asipohudhuria mikutano ya Rais watu wanawalaumu.
Rais wetu amebobea kwenye unafiki, amewakataza wapinzani wasifanye siasa ilanyeye yupo bize na kampeni za majimbo. Kwa unafiki wake kesho wapinzani nao wakipita huko na kushangaa kwanini Watanzania walipigia kura ccm wakati ni wezi atawafungulia kesi za uchochezi.
Rais ajitathimin na matendo yake, asione yeye ndio mwenye haki pekee ya kufanya haya ila wengine wakifanya sio wazalendo.
Kweli madaraka yamekabidhiwa kwa washamba.
 
Back
Top Bottom