Rais Magufuli awapa maofisa wa TAKUKURU ukurugenzi wa wilaya

Abel 2015

Senior Member
Sep 5, 2015
112
55
Kumpa Steven Magoiga Ukurugenzi Wa Wilaya, Kutazuia Sana Mianya Ya Rushwa Katika Halmashauri Ya Wilaya Ya Bariadi..
 
Safi sana. Hapa Kazi Tu lazima ionekane kwa macho. Wasiwasi wangu mtu aliyekuwa anapambana na rushwa asije akawa adui wa TAKUKURU
 
mbona walikuwepo hadi wa usalama wa taifa na rushwa inaliwa tuu? tatizo ni mfumo
 
mbona walikuwepo hadi wa usalama wa taifa na rushwa inaliwa tuu? tatizo ni mfumo
observer1994.jpg


swissme
 
Kumpa Steven Magoiga Ukurugenzi Wa Wilaya, Kutazuia Sana Mianya Ya Rushwa Katika Halmashauri Ya Wilaya Ya Bariadi..
Sidhani kama katatua tatizo.

Chini ya mfumo huu mbovu na wakidhalimu hakuna litakalowezekana kwa asilimiaa 75.
 
Mtu mmoja DAS same time DC atawezaje kuwatumikia mabwana wawili. RAIS azingatie division of labour
 
Takukuru ni kama darasa ukihitimu unaenda field kutekeleza yakupasayo so mleta uzi usistaajabu Rais atawatumia sana hawa.
 
Magoiga alikuwa Takukuru au alikuwa ni wakili wa kujitegemea pale mwanza.... na naona kapelekwa kishapu na sio bariadi...
 
HAMNA JIPYA HAPO CCM NI ILE ILE CHAMA CHA MAJAMBAZI.
Rushwa ipo kila mahala kwenye ulimwengu huu. Mataifa mengi yamejitahidi kupambana na mfumo unaotengeneza rushwa. Tatizo hap kwetu hakuna dalili za kupambana na mfumo huu. Mfano kumteua afisa wa takukuru kuwa mkurugenzi kwenye halmashauri sio kigezo kuwa rushwa haitakuwepo kwenye hiyo halmashauri uzoefu unaonyesha hata ndani ya takukuru kuna maafisa wala rushwa wakubwa, tukirudi kwenye teuzi za hivi karibuni baadhi ya makada walioteuliwa ndy walikuwa wanatumika kugawa rushwa Dodoma na wanajulikana. Sasa leo ukisema rushwa itaondoka nauliza kiviip wakati watuhumiwa wanatamba na kuteuliwa nafasi mbalimbali
 
mbona walikuwepo hadi wa usalama wa taifa na rushwa inaliwa tuu? tatizo ni mfumo
Kuna ofisa usalama wa taifa wa wilaya, ni kinara wa Rushwa ile mbaya. Uzuri kastaafu mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka huu. Natumai atakayeridhi mikoba yake atakuwa muadilifu na muaminifu ili kulinda sifa za TISS zilizotukuka.
 
Kumpa Steven Magoiga Ukurugenzi Wa Wilaya, Kutazuia Sana Mianya Ya Rushwa Katika Halmashauri Ya Wilaya Ya Bariadi..
Nimepapenda hapo lakini usisahau katika tumbua tumbua ya majipu kuna maofisa waliosimamishwa kazi katika taasisi hiyo nyeti. Ninachotaka kusema ni kuwa sio kila aliyeko huko au atokaye huko ni malaika bali ni sehemu yetu ambao wengi 'tumeharibikiwa' kimaadili!
 
Kuna Wilaya kapewa "Brigedia"...Juzi Wanyarwanda wameenda na AK47 zao wakateka kijiji kizima mpaka Mission ya Masista wa Kanisa Katoliki kwa masaa kadhaa,wakafanya yao then wakatambaaa!!!

Usihangaike sana mkuu,sasa hivi we jali familia yako na mkeo(kama umeoa),hizi siasa za nchii utauguwa madonda ya tumbo.Aliteuwa mwanae Ukuu wa Wilaya ya Kisarawe,Lumumba na HQ-Dodoma yakazuka malalamiko ya chini chini kwa vijana waliozunguka kumnadi,basi kagawa vyeo vya Ukurugenzi wa Wilaya hadi kwa makada wa chama ambao hawajawahi kuwa hata watumishi wa umma
 
Back
Top Bottom