mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,075
- 4,111
Wakuu, MAENDELEO HAYANA CHAMA
Rais Magufuli akiwa safarini kutoka Mtwara, ameombwa na mwanakijiji Jimbo la Kilwa kwamba hawana Stendi ya Magari hivyo anaomba wajengewe. Rais Magufuli amejibu kwamba siku nyingine waangalie wawakilishi wanaowachagua ili waweze kufanya vile yeye anavyowaagiza. Mbunge wa jimbo hili aliyemaliza muda wake ni Seleman Bungara aka Bwege Mzee wa ''Umesikia Wapi'' ambaye alikuwa anatokea chama cha wananchi CUF Habari
Rais amezidi kusema kwamba miradi kama hiyo ni ya wabunge na Madiwani ndiyo wanapaswa kuisimamia hivyo kuwataka wabaki na Bwege wao
Rais Magufuli amesema haya...
Nilikuja hapa nikasema nichagulieni watu nitakaokuwa nawaagiza wanafanya ninayoyataka mkasema hapana, Mkamchagua Bwege basi shauri yenu na bwege wenu mwambie awatengenezee stendi
Kazi ya Stendi ni ya madiwani, wabunge. Ukikosea kuchagua, nafuu ukosee kuoa au kuolewa. Ukikosea kuchagua ni tatizo kubwa.
Na hili ndugu zangu niwaombe, muwe waangalifu katika kuchagua. Mchague watu ambao watakuwa kwa ajili ya watu masikini.
Tunatuma hapa fedha za road fund, tunatuma fedha hapa za halmashauri, zimeshindwa kweli kujenga stendi?
Lakini kwa sababu mnanichagulia, wao wenyewe mastendi unategemea mimi mwenyewe nifanyeje? Huo ndiyo ukweli sitaki kuwaficha mlikosea kuchagua.
Sasa katika uchaguzi wa mwaka huu mjipange vizuri, mchague mtu ambaye mtakuwa mmempa stendi akikataa nitamfukuza hata kwenye chama. Lakini leo nitamfukuza huyo aliyeko kwenye chama sijui hata yuko kwenye chama gani, nitamchukulia hatua gani?
Chama cha ACT Wazalendo kimelaani vikali na kuwahamasisha wananchi kukemea vikali kauli hizi za kibaguzi. Wamedai kuwa kitendo cha kuhamasisha ubaguzi na kuingilia mamlaka ya wananchi katika kuchagua mtu wamtakaye kinakiuka misingi ya Katiba yetu.