Rais Magufuli awaapisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Kamishna Mkuu TRA na RAS wa Njombe. Apokea gawio la Airtel la miezi mitatu, Tsh. Bilioni 3

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,469
141,172
Karibuni.

Viongozi wameshawasili wakiwemo wateule!

Rais ameshaingia ukumbini na sasa unaimbwa wimbo wa taifa.

Na wa kwanza kula kiapo ni mh Bashungwa waziri wa viwanda na biashara ambaye sasa anasaini baada ya kula kiapo.

Anayefuati ni mh Kichere RAS mkoa wa Njombe, ameshaapa na kusaini.

Na wa mwisho lakini siyo kwa umuhimu ni Dr Mhede Kamishna mkuu wa TRA, ameshaapa na kusaini.

Sasa wateule wote watatu wanatoa ahadi ya uaminifu mbele ya kamishna wa maadili jaji Harold Nsekela.

Tukio linalofuata ni makabidhiano ya hundi kutoka Bhart ambao ni wamiliki wa airtel.

Kwanza mtenaji mkuu wa airtel amekabidhi hundi ya kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli, ameto $ 1,000,000

Hundi ya pili ni gawio la kila mwezi na leo airtel wametoa gawio la miezi 3 jumla ya sh bilioni 3 ikimaanisha sh bilioni 1 kila mwezi.

IMG_20190610_152415.jpg

Rais Magufuli anapeana mkono na mkuu wa airtel.

Waziri wa Mambo ya Nje, Prof Kabudi

Rais nilitafakari sana niseme nini leo ktk shughuli hii kubwa ambayo ni ya mafanikio makubwa sana katika awamu yako toka ulipochukua maamuzi ya kupitia mikataba mbalimbali ya uwekezaji katika sekta ya madini katika sekta ya Mawasiliano

Wapo ambao hawakuamini kwamba hatua hiyo ilikuwa ni hatua muhimu na itakayokua na tija, wapo ambao waliomba usiku na mchana jambo hilo lisifanikiwe ili ionekane maamuzi hayakuwa sahihi

Zaburi ya 67 (7-8) zinafaa tuziseme leo kwa matokeo ya kazi kubwa uliyofanya Mh.Rais na imefanikiwa, malipo haya ya Billion 3 ni ya mwezi wa 4, wa 5 na wa 6 na kila mwezi itaingia BILIONI 1 kwa miezi 60 ijayo

Anasema yeye ( Kabudi) na Waziri wa fedha Dr Mpango wanafanana na wale wanafunzi wawili ndugu ambao Yesu aliwapenda yaani Petro na Phillipo.

Rais Magufuli alisema fedha itakayotolewa na mkuu wa airtel katika kuunga mkono juhudi zipelekwe kujenga hospitali ya Uhuru kule Dodoma.

Mh. Rais timu ya Serikali ilifanya majadiliano kwa awamu 5, Jan. 15 2019 mkataba wa makubaliano ulisainiwa na kuipa Serikali mafanikio yafuatayo; kuongeza umiliki wa hisa za Serikali ktk Kampuni ya Airtel toka 40% mpaka 49% bila kuzilipia

Makubaliano mengine ni kulipa sh. Bil. moja kila mwezi kwa miaka mitano kama malipo maalum pia imefuta deni na madai ya Airtel ya sh. Bil.937 na hivyo kuokoa sh. Bil.459.13 zilizotakiwa kulipwa na Serikali kama hisa

Tukio la leo linadhihirisha chini ya uongozi wako tumejenga mazingira rafiki kwa uwekezaji, si kila changamoto za uwekezaji kati ya Serikali na Wawekezaji kupelekwa usuluhishi wa kimataifa, tunaweza kujadiliana tukapata ufumbuzi

Faida nyingine kupitia na kuboresha nyaraka zote za umiliki na uendeshaji wa kampuni Airtel Tanzania kwa nia ya kuziba mianya, kulinda maslahi ya taifa na kuisaidia upatikanaji wa faida na gawio kwa Serikali

Mh. Rais kazi hii ya majadiliano kwa upande wa Serikali ulinipa heshima kubwa kusimamia kazi hii nami nakushukuru sana, imani uliyonipa kusimamia kazi hii na Mungu anajua sitokusahau milele. Sikutegemea heshima hii toka kwako, mimi ni nani? nimezaliwa kijiji cha vumbi, nimeishi maisha ya ufukara na baada ya kustaafu sikutegemea nitakuwa hapa lakini wewe na Mungu wako mnajua kwanini mmenitoa jalalani na kunifikisha hapa

Waziri wa Fedha, Dkt. Mpango
Uwekezaji tunauhitaji lakini uwe ni ule ambao Serikali yetu inapata faida na Muwekezaji pia anapata faida

Rais Magufuli
Leo mimi sikutakiwa kuzungumza chochote, kwangu ni siku ya furaha. Ni historia kati ya mazungumzo ya Bhart Airtel na Serikali yaliyodumu kwa mwaka mmoja. Wapo waliobeza, lakini Mungu amewaumbua. Bilioni 1 italipwa kila mwezi(bilioni 12 kwa mwaka)

Kitendo hiki naona kilishikwa mkono na Mwenyezi Mungu. Katika miaka 19 ya Airtel nchini, Serikali haikupata kitu chochote; sitaki kulaumu hiyo ni historia. Kwa miaka hiyo pia tulibambikwa deni la bilioni 930 lakini mazungumzo yakaleta makubaliano

Huyu Mkurugenzi wa Bhart Airtel ana moyo wa Kitanzania. Wapo waliomshauri aende kwenye Mahakama ya usuluhishi, angekwenda mimi nilijiandaa kufuta usajili wa Kampuni. Alitambua suluhu nzuri ni mazungumzo. Pia ametuchangia Dola milioni 1

Nilikuwa naona tabu unayopata Prof. Kabudi Bungeni, wengi wanadhani nakuandaa kuwa Rais. Rais huwa haandaliwi. Fedha hizi haziingii kwenye mfuko wangu, zitatumika kwa Watanzania. Hii Dola milioni 1 ikabidhiwe kwa Katibu Mkuu aanze ujenzi wa Hospitali

Kwa walioapishwa ninawapongeza lakini nawapa pole. Watanzania wanataka matokeo, ukitaka maneno mazuri nenda kaambiwe na Mume au Mke wako. Ninapotengua sio kwamba nakuchukia, nakupongeza Joseph Kakunda kwa kuja. Hizi kazi ni za muda tu

Ukweli ni kwamba Joseph Kakunda haku-push ninavyotaka. Kwanini asipange mkutano na wafanyabiashara? Ndio maana wafanyabiashara wanasema hawajawahi kumuona Waziri. Tumefanya biashara ya Korosho ni nani amenunua? Wizara ya Biashara imekaa tu

Innocent Bashungwa watu wanakupongeza lakini walitakiwa kukupa pole, nikiona haya yaliyolalamikiwa hayajatekelezwa natengua tena. Prof. Kabudi na Dkt. Mpango wamenizidi umri lakini 'pumbavu' nimewatukana sana, japokuwa hawasemi

Kichere nimekutumia zaidi ya meseji 20 na nyingine usiku wa manane. Watu wakilalamika mimi nilikuwa nakutumia meseji zao. Ulikuwa unaona makusanyo ya kodi ya ndani yanashuka lakini hakuna hatua inayochukuliwa. Kafanye kazi. Najua Wahehe wakichukia wanasema swela kisha wanajinyonga, nafuu na wewe ukajinyonge. Nilikokupeleka kuwa RAC ukafanye kazi la sivyo nitakutoa. Kila kitu kinategemea kodi; nisipowalipa Wanajeshi si nitawakuta hapo nje wamesimama?
 
Anafanya kazi yake kama inavyostahili. Kuna watu baada tu ya kuteuliwa badala ya kufanya kazi wanayotegemewa kufanya wanaaza kwenda kwa waganga wa kienyeji. wacha wafahamishwe kwamba mganga makini ni kuchapa kazi tuu! Tuache upuuzi bwana.
 
Mzee wa watu naona kama anajidhalilisha, anajinyenyekeza mpaka inaleta karaha, mara mimi masikini, mara nimetolewa jalalani, kwenye umasikini sifai kitu, nk

Kwa kariba ya nafasi aliyokuwa nayo kabudi Chuo kikuu mpaka hapo alipo anaongea kauli kama hizo, kweli...?
 
Huwa namshangaa sana sasa hayo anayozungumza yanahusu nini Watanzania..
Halafu hii imekuwa ni tabia yake anatakiwa ajuwe ni ya kijinga sana...anarudia rudia kila mara akipewa nafasi...
R.I.P Prof Jwan Mwaikusa...umeenda na mpaka leo kesi ya mauaji yako kimya...
 
Mchango wa kila mtanzania ni muhimu katika safari yetu ya maendeleo.

Mh. Rais usichoke kufanya maboresho kila pale inapobidi.

Kila la heri.
 
Karibuni.

Viongozi wameshawasili wakiwemo wateule!

Rais ameshaingia ukumbini na sasa unaimbwa wimbo wa taifa.

Na wa kwanza kula kiapo ni mh Bashungwa waziri wa viwanda na biashara ambaye sasa anasaini baada ya kula kiapo.

Anayefuati ni mh Kichere RAS mkoa wa Njombe, ameshaapa na kusaini.

Na wa mwisho lakini siyo kwa umuhimu ni Dr Mhede Kamishna mkuu wa TRA, ameshaapa na kusaini.

Sasa wateule wote watatu wanatoa ahadi ya uaminifu mbele ya kamishna wa maadili jaji Harold Nsekela.

Tukio linalofuata ni makabidhiano ya hundi kutoka Bhart ambao ni wamiliki wa airtel.

Kwanza mtenaji mkuu wa airtel amekabidhi hundi ya kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli, ameto $ 1,000,000

Hundi ya pili ni gawio la kila mwezi na leo airtel wametoa gawio la miezi 3 jumla ya sh bilioni 3 ikimaanisha sh bilioni 1 kila mwezi.

Rais Magufuli anapeana mkono na mkuu wa airtel.

Waziri wa Mambo ya Nje, Prof Kabudi
Anasema yeye ( Kabudi) na Waziri wa fedha Dr Mpango wanafanana na wale wanafunzi wawili ndugu ambao Yesu aliwapenda yaani Petro na Phillipo.

Rais Magufuli alisema fedha itakayotolewa na mkuu wa airtel katika kuunga mkono juhudi zipelekwe kujenga hospitali ya Uhuru kule Dodoma.

Baadhi ya makubaliano yaliyosainiwa kati ya Serikali na Kampuni ya Artel ni kuongeza umiliki wa hisa za Serikali ndani ya kampuni hiyo kutoka asilimia 40 hadi asilimia 49 bila kuzilipia

Makubaliano mengine ni kulipa sh. Bil. moja kila mwezi kwa miaka mitano kama malipo maalum pia imefuta deni na madai ya Airtel ya sh. Bil.937 na hivyo kuokoa sh. Bil.459.13 zilizotakiwa kulipwa na Serikali kama hisa

Hapa kwa habari za namna hii hutakuja kugombana na mimi hata siku moja
 
Back
Top Bottom