Rais Magufuli awaapisha viongozi mbalimbali wa Mikoa na Wilaya aliowateua hivi karibuni

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,741
141,603
Rais Magufuli leo anawaapisha wakuu wa mikoa ya Tabora na Kigoma, Ikulu jijini Dodoma. Kadhalika Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri watakula viapo vya maadili.

Tukio hilo litarushwa mubashara na TBC na Channel ten

Up dates;
===

Leo Julai 6, 2020, Rais MagufuliJP anatarajia kuwaapisha viongozi mbalimbali wa mikoa na wilaya aliowateua hivi karibuni, shughuli itakayofanyika Ikulu, Chamwino, Jijini Dodoma.


UPDATES:
10:17
Rais Magufuli amefika katika eneo la kuapishia hapa Ikulu Chamwino

10: 19 Tobias Emily Andengenye ameapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.

10: 21 Dr. Philemoni Sengati ameapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

10: 23 Miriam Perla Mbaga ameapishwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa.

10: 26 Mathias Julias Kahabi ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Biharamuro Mkoani Kagera

10: 29 Ismail Twahir Mlawa ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro

10: 33 Albinus Bandio Mngonya ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro

10: 33 Wilson Samuel Shimo ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chang'wale- Geita.

10: 38 Abbas Juma Kayanda ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

10: 40 Martine Stephan Ntemo ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani

10: 42 Toba Alnason Nguvila ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga

10: 44 Lazaro Jacob Twange ameapishwa kuwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara

10: 47 Jamila Yusuph Kimaro ameapishwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi

10: 50 Salum Abdallah Kali ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza

10: 56 Viongozi wateule kwa Makundi wanatoa kiapo (Ahadi ya uadilifu kwa Viongozi wa Umma).

11: 05 Godwini Gondwe amewawakilisha wengine kutoa salamu katika viongozi walioteuliwa ambaye kwa nafasi hii amemshukuru Rais kwa kumuamini na kumpeleka katika Wilaya nyingine pamoja na kumpongeza Rais na Serikali kwa ujumla.

11: 10 Tobias Emily Andengenye amesimamishwa kutoa salamu kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa walioteuliwa. Amemshukuru Rais kwa kumteua pamoja na kuwapongeza walioteuliwa na kuwasisitiza kutimiza majukumu yao katika Seheu walizopangiwa. Pia, ametoa rai kwa Wateuliwa wote wamsaidie rais katika kutatua kero za Wananchi hasa zilizopo katika ngazi za vijiji.

11: 15 Hotuba ya Profesa
Waziri Kabudi amepewa nafasi ya kutoa salamu katika mkutano huo. Ambaye pia amempongeza Rais Magufuli kwa mambo makubwa aliyoyakamilisha katika Utawala wake.

Katika kusisitiza hilo Prof Kabudi amesema "Mungu mwema amekupa kibali cha kuwa Rais wetu. Hakika mwakani tutakapoandika kitabu cha miaka 60 ya Uhuru. Sura ya mwisho itajaa mambo makubwa uliyoyakamilisha - Sura hiyo wewe unaikamilisha; Mwalimu aliianzisha wewe umeikamilisha"

Zaidi ya Hayo, Prof Kabudi amewasisitiza Viongozi walioteuliwa kutimiza kila wajibu na majukumu wanayoyafanya. Sambamba na hilo, Prof amewasisitiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ya Morogoro kuwa ni mkoa wa kimkakati hivyo wanapaswa kuchapa kazi.

Prof Kabudi amesema "Sisi tulioapishwa tutunze viapo vyetu na uaminifu wetu. Tujue kazi unayopewa na Rais ni muhimu na ya thamani, usitamani nyingine - Umepewa wajibu. Wajibu ni mkubwa utunze na uheshimu. Unapopewa kazi na Rais aliyekuamini, kutekeleza kinyume si busara"

"Rais umetupa utumishi sio umaarufu. Wanaotaka umaarufu si awamu hii, wanaotaka utumishi tena utumishi wa mbio hii ndio awamu yenyewe - Mnaokwenda Mkoa wa Morogoro mjue mnakwenda kwenye mkoa wa kimkakati kama ni treni hiyo ndio injini"

Prof Kabudi ameongeza kuwa "Utumishi wa Umma hauna kupanda wala kushuka ni mwendo mbele. Rais umewadhihirishia Watanzania ni namna gani moyo wako umejaa huruma kwa anayekiri makosa - RC wa Kigoma ukasome Zaburi ya 113 na kufanya kuwa sehemu ya ibada yako. Sisemi kwa kuwa ni shemeji yangu"

11: 32 Hotuba ya Waziri Jafo
Waziri Jafo amepata nafasi ya kutoa salamu ambapo ameanza kwa kumpongeza Rais kwa kazi kubwa anayoifanya katika hili Waziri Jafo amesema "Rais kazi yako haina mfano, Watanzania wanakuona unavyowahangaikia na wewe hujihangaikii. Niwapongeze walioteuliwa ila mjue hapo mmevishwa joho la madaraka, nendeni mkayatunze. Unaweza kufahamu kuwa ulikuwa umevaa Joho siku litakapokuvuka"

Watu zamani Kituo cha Afya kinapewa fedha miaka 3 hakikamiliki. Ndugu zangu tusiwe washona suti, washona suti ni watu ambao wamekaa mezani mwaka mzima hatembei, twendeni tukafanye kazi"

Akisisitiza kuhusu Mafanikio ya Rais Magufuli Waziri Jafo amesema "Tuna wingi wa vituo vya Afya hadi leo wananchi wanasema Mhe. Rais hana haja ya kufanya kampeni, ni kutokana na watu kuacha kukaa ofisini. Wizara yetu ni ya mchakamchaka, usipofanya hivyo utaonekana unapwaya mapema"

11: 35 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amepata nafasi ya kutoa salamu ambapo pia ameitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais kwa Mafaniko na uchapakazi alioufanya. Sambamba na hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amempongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza miradi mbalimbali ukiwemo wa SGR kwa kutumia pesa zetu za ndani.

11: 41 Hotuba ya Rais Magufuli
Ameanza kuwapongeza Wateule wote kwa nafasi walizoteuliwa na kusisitiza kuwa amewafuatilia sana na anaamini watakwenda kufanya kazi nzuri.

Katika hili Rais Magufuli amesema Namfahamu kila mmoja, nimewateua nikiwa nawajuwa. Nendeni mkafanye kazi. Jukumu letu ni kwenda kuwatumikia Watanzania tukatimize wajibu wetu. Hatuwezi kuwafurahisha wote ila tukatimize wajibu wetu. Mifano mizuri mnaona kwa viongozi waliowatangulia Wakuu wa Wilaya na Mkoa

Katika kuwasisitiza Viongozi hao kuwajibika Rais Magufuli amesema "Nchi yetu hii ina changamoto nyingi sana na sisi tukizisimamaia vizuri tutawasaidia Watanzania ambao sasa ni zaidi ya milioni 60 - Nasikitika sana ninapokwenda sehemu Wananchi wa pale wanakutolea masikitiko wakati viongozi uliowateua wapo pale

Mkoa wa Kigoma una maendeleo mengi, sasa hivi tunajenga barabara ya kwenda hadi Nyakanazi, Tabora na Katavi - Mkuu wa Mkoa (Thobias Andengenye) nenda kafanye kazi kazunguke na kafanye kazi. Kawatumikie Wananchi. Kasisitiza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma azunguke azijue na atatue changamoto mbalimbali zilizo katika mkoa huo.

Akimuelezea Mkuu wa Mkoa mpya Tabora (Sengati) Rais Magufuli amesema "Ngoja nikwambie umefanya kazi nzuri . Wapo wengine waliokutisha wakijifanya wananifahamu sana kuwa wanakuja kukusemea kwa Rais - Ukawaambie tangulieni, mimi nachapa kazi hapa. Nikaona unaweza ndiyo maana tumekupa Tabora, kawatumikie wananchi.

Zaidi ya hayo Rais magufuli amewapongeza Wateule wote kwa kazi nzuri walizozifanya awali pamoja na kuvipongeza viombo vya ulinzi na usalama.

Katika hili Rais Magufuli amesema "Vyombo vya Ulinzi na Usalama navipongeza sana. Jana niliona wa Madawa ukienda milimani kule. Kijiji kidogo kuna Bangi, kidogo bangi - Hii inaonesha kuwa wanaonisimamisha kule hawafanyi kazi. Haiwezekani wewe utoke Dodoma hapa ndio ukagundue hizo bangi"

Rais Magufuli ameamua kuwaondoa baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi Meru, ambapo amemuamuru IGP Mkuu wa Polisi pamoja na Afisa Usalama wa Meru kuondoka.

Katika hili Rais Magufuli amesema "IGP nataka Mkuu wa Polisi wa Meru aondolewe, Afisa Usalama wa Meru aondoke. Maana hawakutimiza wajibu wao - OCCID wote watoke, ikiwezekana washushwe cheo maana hatuwezi kwenda kwenye utaratibu huo. Na wewe wa Kitengo cha Madawa nakuthibitisha leo."

Rais Magufuli amesisitizwa kusikitishwa na suala la madawa ya kulevya ya Mkoa huo kukutwa na wengine waliotoka Dar. katika hili Rais Magufuli katika Mkoa huo kuna viongozi hawakutimiza wajibu wao.

Zaidi ya hayo, Rais Magufuli amesisitiza kuwa kwa viongozi wanaotaka kuomba ruhusa ruhusa hizo zipo. Hivyo, kiongozi yoyote anayetaka kuomba ruhusa anakaribishwa.

Rais Magufuli akiendelea kuwasisitiza wateuliwa wote ameongeza kuwa "Kila mtu akaridhike na kile alichokipata. Hata mfano wa Yesu, pengine sio mzuri hapa ila wale waliopewa talanta hawakupewa zinazolingana - Mkaridhike na nafasi zenu na kuwaongoza vizuri Wananchi. RCs, DCs, RPCs na kila mmoja mnajitahidi kufanya kazi".

Mwisho, Rais Magufuli amewasisitiza wateuliwa wote kuwa wawajibikaji na kuendelea kutimiza majukumu mbalimbali wanayopewa kwa Maslahi ya Watanzania kwa ujumla.
 
Kuna mwamba ametrend sana kati ya wanaoapishwa leo nasikia ni mtu katili hatari kwenye yale Mambo ya barrot box ni "Ngwanidako"
 
Kumekucha Sasa Hivi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Akiwa Kwenye Majukumu Yake Ya Kila Siku
 
Ni live kutoka IKULU YA CHAMWINO- DODOMA Uteuzi huo upo live Tbc, Itv, Clouds tv
 
NILIHACHAGA KUANGALIA TBCCM BAADA YA KUZUIA BUNGE LIVE NA HATA NYUMBANI KWANGU NIMEIBAN IVYO MKO KAMA 300 TU IVI MNAOFUTATILIA HIZO SANAA
 
Back
Top Bottom