JUMAPILI ya Oktoba 22 mwaka huu (2017) nilisoma na kuvutiwa na kile kilichoandikwa na mwanataaluma ya uhasibu, Kalima Nkonde ambaye ni raia wa Zambia.
Nkonde pia ni mtaalamu wa masuala ya uongozi wa fedha (Finacial Management Expert). Ni mstaafu, na mtu huru mno katika utoaji wa maoni au uchambuzi kuhusu masuala yanayogusa taaluma yake.
Kwa miaka 25 amepata kuishi nchi mbalimbali ambazo ni pamoja na England, Afrika Kusini na Botswana.
Hiyo Jumapili, kama nilivyoeleza aliandika kitu kuhusu sekta ya shaba nchini Zambia, akirejea kile kilichofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, kiasi cha kumtaka Rais wa Zambia, Edgar Lungu kuiga mfano.
Kwa kurejea taarifa mbalimbali za kitaalamu, Nkonde anaeleza namna shaba ilivyopata kuongezeka thamani bila Wazambia kufaidika na zaidi ya hapo, namna itakavyoendelea kuongezeka thamani duniani.
Kuna mambo mawili anayachambua kuhusu shaba kuongezeka thamani. Kwanza, ukuaji wa teknolojia – hili lilianza baada ya ufumbuzi na matumizi ya magari yanayotumia umeme. Pili, ni ufumbuzi au matumizi ya nishati anuai.
*Mapinduzi ya magari ya umeme*
Anatumia taarifa za Chama cha Kimataifa cha Shaba (International Copper Association -ICA), akisema matumizi ya shaba kwenye magari ni ya kiwango cha juu, kwa mfano, shaba inayotumika kwenye ‘mabetri’ ya magari, lakini si tu katika ‘mabetri’ bali hata maeneo mengine ya magari hayo.
Kwa mfano, gari moja linaweza kutumia ‘urefu’ wa takriban kilomita sita za shaba kwa ajili ya kutengenezewa mfumo wa umeme (copper wiring). Lakini kwa magari yanayotumia kile kinachoitwa “internal combustion engines” huhitaji hadi kilo 23 za shaba kila moja, na ripoti hizi za ICA zinachambua kwamba muundo mpya wa magari yenye mchanganyiko wa teknolojia (hybrid electric vehicle) unatumia karibu mara mbili ya hizo (kilo 23), kwa maana ya kilo 40 za shaba, na ‘plug’ kwenye magari ya aina hiyo hutumia kilo 60 za shaba. Lakini kwa kutegemea na ukubwa wa ‘betri’ (battery), basi la mfumo wa umeme hutumia kati ya kilo 224 na kilo 369 za shaba.
“Bila shaba huwezi kuwa na magari yenye mfumo wa umeme, ni jambo rahisi tu,” anasema John Fennell, Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO0 wa ICA tawi la Australia, ambaye Nkonde anamnukuu kama alivyonukuliwa na Shirika la Habari la ABC.
Kwa mujibu wa ripoti ya kampuni ya ushauri ya IDTechEx, iliyopewa kazi maalumu na ICA, mahitaji ya magari yenye mfumo wa umeme yakiwamo mabasi, yanatarajiwa kuongezeka hadi kufikia milioni 27 mwaka 2027, mengi kutoka nchini China.
Vile vile taarifa ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati (International Energy Agency - IEA), inabainisha kwamba, mahitaji ya magari ya mfumo wa umeme duniani yataongezeka hadi kufikia kati ya milioni 9 na milioni 20 kufikia mwaka 2020 na baadaye, kati ya milioni 40 hadi milioni 70 ifikapo mwaka 2025.
*Kasi ya Magufuli Zambia*
Nkonde anasema, hakuna shaka kabisa kwamba Zambia itafaidika kidogo mno kama ilivyo katika miaka ya nyuma, endapo hali ya sasa itaendelea.
Kampuni za uchimbaji madini ni lazima sasa zipewe masharti ya ama kukubali kuanza majadiliano ili hatimaye kila upande ufaidike kikamilifu kati ya Zambia na hizo kampuni, vinginevyo, wafunge virago na kuondoka, na kisha kampuni nyingine zialikwe kufanya shughuli zao, kwa kuwa soko ni la uhakika.
Anaandika; “Nchi jirani iliyoko kaskazini na Zambia, Tanzania, ni mfano bora zaidi kwa sasa katika kulinda masilahi yake dhidi ya kampuni za madini. Rais John Pombe Magufuli, maarufu kwa jina la ‘tinga tinga’ amesukuma mageuzi makubwa katika tasnia ya madini.”
Anaeleza namna msukumo wa Rais Magufuli ulivyowezesha kubaini udanganyifu mkubwa kwenye sekta ya madini ya dhahabu Tanzania na namna nchi ilivyokuwa ikipoteza mapato.
Anajenga nguvu ya hoja yake kwa msisitizo akinukuu kauli ya Magufuli katika hotuba yake aliyoitoa akiwa wilayani Chato, kaskazini-magharibi mwa Tanzania; “Ni lazima tunufaike na utajiri aliyotuzawadia Mwenyezi Mungu, na kwa hiyo ni lazima tulinde rasilimali zetu, hatupaswi kuachiwa mashimo.”
Kinyume na upinzani wa wabunge wa upinzani bungeni, wakiongozwa na Chadema, mtaalamu huyu anasifu uamuzi wa Serikali ya Magufuli kupitisha sheria bungeni inayotaka serikali kuwa na hisa asilimia 16 kwenye migodi, kutaka kampuni za madini ‘ziambukize’ utaalamu Watanzania, pamoja na kampuni hizo kununua mahitaji yao mengine kwa wawekezaji wa ndani ya nchi.
*Zambia itanufaikaje na shaba?*
Anasema, kwa kutazama ukubwa wa madeni yanayoielemea Zambia na ambayo baadhi yanachangiwa na kampuni za madini kutolipa kodi inayostahili, kuna sababu za kutosha za kuisukuma serikali ya Zambia kufanya uamuzi mgumu.
Anasema Rais wa Zambia, Lungu, ni lazima atekeleze ahadi zake kutoka katika hotuba alizopata kuzitoa na kwamba kwa sasa kuna kasoro, bahati mbaya, serikali imeonyesha ubabe wake tu katika kuondoa ruzuku ya umeme, mafuta na mambo mengine yanayoathiri Wazambia wa kawaida badala ya kuonyesha ubabe huo kwenye kulinda rasilimali kama anavyofanya Rais Magufuli wa Tanzania.
*Makala hii imetafsriwa na kufupishwa kutoka katika LusakaTimes*