Rais Magufuli awaalika wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Ikulu Chamwino Dodoma

VIJANA WA CCM TUKAE KWA KUTULIA.

Na Thadei Ole Mushi.

Kila nikiangalia hii picha ya Joshua Nasari, nikikumbuka na swali lililoulizwa na Mjumbe Wa NEC toka Songwe kuhusu wahamiaji kupewa Vyeo badala ya vijana waliopo CCM nacheka Sana.

Definitely tuache Hawa vijana wajinafasi kwa kuwa sioni ndani ya UVCCM mwenye uwezo wa kuwazidi. Nilipokuwa nasema Sana kuhusu hili miaka ya kuanzia 2017 Hakuna waliokuwa wanaunga mkono Hoja hiyo kila mtu alikuwa anaimba litania, Ngonjera,Pambio za Masifu, kupiga Manyanga nk.

Niliwaambia ifikapo 2020 mtakumbuka haya niliyokuwa nawaandikia na niliwaambia CCM Asilia itakuwa imetekwa na kutiwa mfukoni. Ni Dhahiri baada ya chuo Cha kivukoni kushindwa kupika vijana wa CCM Chadema inatusaidia jukumu Hilo.

Huwa nawaambia mnapata wapi ujasiri wa kuwaita Chadema Nyumbu? Hahahahah tutulie infact hatuna vijana wanaofikia viwango vya Hawa watu. Tutulie tuendelee na kujifua.

Ukiona baba yako anawagawia watoto wa Jirani Urithi ujue wewe ni mvuta bangi na mla Unga. Akikupa Urithi utauza upate hela ya kulamba Unga.

Ole Mushi
0712702602
 
Hao wanaopewa chakula ni wasannii wakiwa wanatuzwa jukwaa gani.
Acha upuuzi

Hivi huwezi kuchangia mada bila matusi? Nakushauri jibu hoja kwa kutumia hoja, kutoa maneno yasiyo na staha si vizuri. Jaribu kupnguza jasba.
Sijakuelewa unaposema wanaopewa chakula ni wasanii.

Uzi ulisema:
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) mhe. John Pombe Magufuli, awaalika wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa na wasanii chakula cha mchana eneo la ujenzi wa ofisi ya Ikulu Chamwino, Dodoma. Leo 12 Julai, 2020"

Sasa upuuzi wngu huko wapi hapo?
 
Ni sahihi kabisa kujipongeza wakiwa na Mwenyekiti wao.Wao ndio Chama tawala.Watakula, watakunywa na watapiga picha nyingi na maisha yataendelea.
KUTAWALA= Kumtawala nchi,mtu,watu
kimabavu, watake wasitake watatawaliwatu hata kwa mtutu wa bunduki.

KUONGOZA=Kuongoza nchi, watu, mtu, kwahiari, kumtoa ktk jambo lolote baya na kumpeleka ktk jambo jema.
Hapo hapatumiki nguvu wala lazima.

Ccm ni chama tawala ndy maana hakitaki kuondoka madarakani
 
Nampongeza mhe Rais Magufuli kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa ilani ya CCM 2015 / 2020.
Rais na mwenyekiti wa CCM amefanyakazi kubwa sana anahitaji pongezi.
Siyo dhambi kuwakaribisha wananchi na wana CCM katika ikulu yetu ya Chamwino Dodoma.
Pongezi kwa kazi nzuri ya ujenzi wa nchi yetu.
 
Nchambi leo atalala hoi
IMG_20200712_132116.JPG
 
CDM mwaka huu mkipata hata diwani mmoja mtakuwa kweli ni Makamanda. Ila tatizo nanyi mlimchezea sana Kikwete na kumtukana, mliutumia uungwana wake vibaya. Mkaishie kupiga madili kwa staili ya kumtisha. Mkampanikisha mzee wa watu, akaamua awaletee Chuma hiki mpambane nacho. Round ya kwanza tu kawatoa KO, sasa mmebaki kutapatapa, hamna hata mnachosimamia tena. Kampeni hazijaanza, ila Chuma leo kinapiga kampeni waziwazi na mmeufyata mkia, mmebaki kupost vithreads visivyo na nguvu yeyote JF.
 
YALIYOJIRI LEO JULAI 12, 2020 DKT.JOHN POMBE MAGUFULI ALIPOKUTANA NA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM, IKULU CHAMWINO, DODOMA

Aliyoyasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli

Hii ni Ikulu yenu, mimi ni mpangaji tu! Wenye Ikulu ni nyinyi na ndio maana sikubagua, ata wa vyama vingine nimewakaribisha kwa kutambua tuna wajibu wakujenga Tanzania moja - Dkt. John Pombe Magufuli.

Mwaka 1973 nilikua darasa la sita, Chato Shule ya msingi, maamuzi ya kuhamia Dodoma yalipotolewa na Hayati Mw. Julius Kambarage Nyerere na ata sikuyaelewa maamuzi hayo kipindi hicho.

Niliingia kwenye siasi mwaka 1995 nilipochaguliwa kuwa mbunge na Mheshimiwa Mkapa akanichagua kuwa Waziri wa Ujenzi. Sikuwahi kugombea kiti chochote cha NEC katika miaka yangu yote 20 nikiyokuwa Waziri na sikuwahi kuwa mjumbe wa Kamati Kuu

Nawashukuru Watanzania wote wa vyama vyote, makabila yote kwa ushirikiano wao mkubwa miaka yote mitano. Nawashukuru viongozi wa dini zote, waislamu, wakristo, wasabato na ata wenye dini za asili. Navishukuru pia Vyombo vya Ulinzi na Usalama

Historia ya Chamwino imeelezwa, tumeanza kuweka mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujenga ukuta wa 27KM, ukuta umekamilika na umejengwa na vijana wa JKT. Ikulu hii ni kubwa kupita Ikulu zote duniani

Tumeamua, Ikulu yote Dar es Salaam tutaihamishia hapa na itajengwa na vijana wetu wakitanzania wa Jeshi la Wananchi (JKT) na waemkua wakikesha kufanya kazi hapa. Utofauti kidogo wa Ikulu hii na ile ya Dar es Salaam ni kwamba hii itakua na ‘Underground’ na itakua ‘modified’ zaidi. Ndani ya miezi sita itakua imekamilika kabisa.

Nina deni kubwa kwa wasanii, kuhusu kuihamisha COSOTA inayosimamia shughuli za wasanii kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na nimeagiza kupitia kwa Waziri Mkuu, amenilete barua na nimeshaisaini na nimemuagiza Katibu Mkuu Kiongozi na viongozi wengine na ndani ya wiki hii ijayo itakua imekamilika.

Mhe. Mwakyembe nataka kabla ya kwenda kuchukua fomu, uje uchukue barua niliyoisaini kwa kuhamisha shughuli za COSOTA kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara kwenda kwenye Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo ili vijana wawezi kunufaika

Nataka niwaambie wanamuziki mimi huwa nawasikiliza sana. Muziki ni burudani, huwa nawafuatilia sana na mmeitangaza Tanzania vizuri, endeleni kuitangaza. Napenda kuwashukuru pia waigizaji na wanamichezo wote kwa kuitangaza Tanzania vizuri

Hapa ndio makao makuu ambapo baraka zote zililetwa na Hayati Baba wa Taifa. Dodoma ndio makao makuu, hali ya hewa ni nzuri na sisi tumeshahamia. Kutoka Dodoma kwenda Iringa Ruaha ni masaa mawili na nusu kwahiyo watu watakua wanakuja kufanya utalii.

*IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO*
IMG-20200711-WA0326.jpg
 
Back
Top Bottom