Rais Magufuli awaalika Ikulu Wafanyabiashara wakubwa watano kutoka kila Wilaya

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Habari wakuu,

Rais Magufuli amewaalika Wafanyabiashara kutoka kila Wilaya Ikulu. Rais anataka Wafanya biashara Watano kutoka kila Wilaya Tanzania, amesema haijalishi hata kama ni Mfanyabiashara Mwanasiasa wala mtendaji wa Serikali

Wafanyabiashara wametakiwa kujigharamia nauli ya kufika Dar Es Salaam

Mkutano utafanyika tarehe 07 Juni 2019.
IMG_20190602_122058_593.jpg


MY TAKE:

Hawa matajiri wasikose, kwani ndio wameshikilia Uchumi wa Tanzania. Ndo wanajua mbinu ya kufanya biashara Tanzania. Bila hawa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

1. Peter Zakaria - Msoma
2. Mohammed Gulam Dewji - Ilala
3. James Rugemalira - Bukoba
4. Yusuf Manji - Kinondoni
5. Akrim Aziz na kaka yake Rostam Aziz - Kinondoni
6. Gulamali - Singida
7. Ally Mufuruki- Ubungo
8. Edward Lowassa - Monduli na rafikie Kalamagi - Bukoba vijijini

Kuna Kipindi raia Mstaafu Kikwete alisema, hii nchi kuna watu wakiguswa nchi inatikisika.





 
Mambo yamekuwa magumu,

Ameamua kuomba POOOO,

AWAGHARIMIE,

WATANZANIA SIYO WAJINGA,

Ukitaka tajiri aishi kama SHETANI, tambua kuwa wananchi wataishi kama MAZOMBIE na uchumi wa serikali utaporomoka.

No one has ever seen further without standing on the shoulder of the giant!

Tunasubiria awaite pia watumishi wa umma
 
Tatizo la Magufuli anadhani Wafanya biashara ndiyo wanachangamoto pekee. Kikubwa anatakiwa ajiulize kwanini biashara Imedorora? Tafsiri Kubwa ni Kuwa Watu hawana Pesa, sasa Wafanyabiashara Watamuuzia nani?

Hataki Kuingiza Pesa kwenye Mzunguko. kwavile Watumishi ndiyo Watumiaji Wakubwa na hali zao Mbaya, Watatoa wapi za Kununulia ili Pesa iingie Mtaani. Wakulima wenyewe hoi bin taabani, Sekta binafsi lazima ife ama iende taraatibu, hakuna namna!

Mchawi wa Uchumi wetu ni yeye mwenyewe Magufuli. Aonywaye Mara nyingi, lakini akashupaza Shingo, Mwisho Shingo yake huvunjika!
 
Binadamu ndio tulivyo hatuna jema.
Binadamu waliuwa manabii na mitume.

Akiomba kukutana na wahusika mnasema kazidiwa.

Asipowaita wahusika mnalalamika hashauriki, haambiliki, anajiona anajua kila kitu, mara 'one man show'.

Pendekeza sasa afanye nini?
 
Back
Top Bottom