Rais Magufuli avunja rekodi ya kuzunguka Tanzania kwa muda mfupi zaidi

broken ages

JF-Expert Member
Mar 23, 2012
235
84
RAIS MAGUFULI AVUNJA REKODI YA KUZUNGUKA TANZANIA KWA MUDA MFUPI ZAIDI.
Watanzania,
Mtakubaliana na Mimi ya kwamba pamoja na mambo mengi mazuri ayafanyayo Rais wa Tanzania hili la usafi siku za jumamosi ni mojawapo ya mambo ambayo yanatufanya tuone na kuukubali utendaji na uwajibikaji wa Rais MAGUFULI ni wa ukweli zaidi

Binafsi mimi leo niko Arusha mjini nikiwa napita katika mitaa ya makao mapya na hata Unga ltd nimeona maeneo haya yakiwa safi sana,

Ni jambo la tofauti na nilivyokuwa nimeona siku za nyuma kabla ya utawala wa mheshimiwa MAGUFULI kwani usafi huu ungeonekana ikiwa kungekuwa na taarifa ya kupita kiongozi flani wa ngazi ya juu serikalini ama hata kiongozi maarufu kutoka nje ya nchi Kama vile alivyokuja Rais wa Amerika n.k

Nimestaajabu kiasi cha kumpigia simu rafiki yangu aishie mwanza kumuelezea ni kwa namna gani ninavyostaajabu kwa mazingira ya Arusha yalivokuwa safi,nilichokipata kwake ni kwamba na hata yeye anastaajabu kwa mazingira ya mwanza nayo yanavyoonekana ,
Nikagundua ya kwamba kumbe ni Tanzania nzima leo imebadilika kutoka kwenye uchafu uliokithiri hadi kwenye usafihi unaoanza kustaajabisha na hapo ndipo ninapozidi kumwona Rais MAGUFULI kama mkombozi na mwanamapinduzi wa Watanzania,anayetupa matumaini mapya tena na anayeweza kweli kuisogeza Tanzania kwenye ukurasa wa nchi zinazoheshimika na hata mataifa kutoka nje.

Pamoja na kusitisha safari za viongozi wa nchi kupishana huko angani wakifuja pesa za serikali kwa safari nje ya nchi na hata yeye mwenyewe kutokusafiri nje ya nchi .
Akiwa ndiye Rais madarakani hili la usafi limenigusa,hii ni sawa na kwamba kwa muda usiozidi masaa matano RAIS ameizunguka na kuitembelea TANZANIA nzima.kwani usafi huu ungefanyika iwapo tu angetembelea sehemu husika.

Kumbe kuna mambo ambayo ni mazuri tu yanaweza pia kufanyika ndani ya nchi hii ila kinachohitajika ni moyo wa utashi na ari ya kiongozi kwa kuwapa wananchi hamasa.HONGERA RAIS MAGUFULI TUPO NYUMA YAKO JEMADARI WETU KTK VITA HII YA TANZANIA MPYA,NA KAMA UNAVYOTUSIHI MARA NYINGI KTK HOTUBA ZAKO KUWA TUKUOMBEE KWA MUNGU,TUNAKUOMBEA KWAKE ILI AZIDI KUKUPA AFYA MOYO WA UZALENDO PAMOJA NA MAARIFA YA KUTUONGOZA.

Tunawaomba na wasaidizi wako ktk nyanja mbalimbali wasikuangushe na pia sisi wananchi tushirikiane kukuunga mkono ktk kutekeleza kwa bidii na nguvu zote (HAPA NI KAZI TU!)wajibu na majukumu yetu ktk nafasi zetu za kazi .
 
Usafi tu hautoshi tunataka kuona hawa wakuu wa miji wakifanya miji yao kuwa bora zaidi kwa kuweka viwanja vilivyo wazi kwa watoto wetu kucheza mpira badala ya kuzurura au kucheza pool.
Pia wajiongeze kwa kuweka parks na kupanda maua kwenye hizo sehemu walizozirudisha serikalini
 
Usafi Arusha? Usitanie. Baada ya dar, ARUSHA inafuatia kwa uchafu! Hivi majuzi nimekuta mzoga wa mbwa kwenye mtalo around mnara wa azimio, mkabara na makumbusho. Vipi walishamtoa?
 
Usafi tu hautoshi tunataka kuona hawa wakuu wa miji wakifanya miji yao kuwa bora zaidi kwa kuweka viwanja vilivyo wazi kwa watoto wetu kucheza mpira badala ya kuzurura au kucheza pool.
Pia wajiongeze kwa kuweka parks na kupanda maua kwenye hizo sehemu walizozirudisha serikalini
Kinacho sikitisha ni kutembea umbali mrefu mjini bila kuonekana vifaa vya kutupa taka. Vikiwepo kwa umbali mfupi vitasaidia kuchochea Tabia ya usafi. Ni vizuri watendaji wakaliona hili. Lakini vilevile iwepo mipango endelevu ya kuzoa taka zilizo kusanywa. Miji mingine sijui viongozi wake wapoje. Ukitembelea Morogoro katikati ya mji na soko kuu unajiuliza kipindupindu kitaishaje? Hili solo ukienda inabidi uvae gumboots, na liko hivi miaka tote kipindi cha mvua. Halo tayari naona kuna majipu.
 
Naona hao wanaojiita viongozi wangepelekwa Moshi tu kujionea jinsi palivyo maana usafi ni maadili toka nyumbani
 
RAIS MAGUFULI AVUNJA REKODI YA KUZUNGUKA TANZANIA KWA MUDA MFUPI ZAIDI.
Watanzania,
Mtakubaliana na Mimi ya kwamba pamoja na mambo mengi mazuri ayafanyayo Rais wa Tanzania hili la usafi siku za jumamosi ni mojawapo ya mambo ambayo yanatufanya tuone na kuukubali utendaji na uwajibikaji wa Rais MAGUFULI ni wa ukweli zaidi

Binafsi mimi leo niko Arusha mjini nikiwa napita katika mitaa ya makao mapya na hata Unga ltd nimeona maeneo haya yakiwa safi sana,

Ni jambo la tofauti na nilivyokuwa nimeona siku za nyuma kabla ya utawala wa mheshimiwa MAGUFULI kwani usafi huu ungeonekana ikiwa kungekuwa na taarifa ya kupita kiongozi flani wa ngazi ya juu serikalini ama hata kiongozi maarufu kutoka nje ya nchi Kama vile alivyokuja Rais wa Amerika n.k

Nimestaajabu kiasi cha kumpigia simu rafiki yangu aishie mwanza kumuelezea ni kwa namna gani ninavyostaajabu kwa mazingira ya Arusha yalivokuwa safi,nilichokipata kwake ni kwamba na hata yeye anastaajabu kwa mazingira ya mwanza nayo yanavyoonekana ,
Nikagundua ya kwamba kumbe ni Tanzania nzima leo imebadilika kutoka kwenye uchafu uliokithiri hadi kwenye usafihi unaoanza kustaajabisha na hapo ndipo ninapozidi kumwona Rais MAGUFULI kama mkombozi na mwanamapinduzi wa Watanzania,anayetupa matumaini mapya tena na anayeweza kweli kuisogeza Tanzania kwenye ukurasa wa nchi zinazoheshimika na hata mataifa kutoka nje.

Pamoja na kusitisha safari za viongozi wa nchi kupishana huko angani wakifuja pesa za serikali kwa safari nje ya nchi na hata yeye mwenyewe kutokusafiri nje ya nchi .
Akiwa ndiye Rais madarakani hili la usafi limenigusa,hii ni sawa na kwamba kwa muda usiozidi masaa matano RAIS ameizunguka na kuitembelea TANZANIA nzima.kwani usafi huu ungefanyika iwapo tu angetembelea sehemu husika.

Kumbe kuna mambo ambayo ni mazuri tu yanaweza pia kufanyika ndani ya nchi hii ila kinachohitajika ni moyo wa utashi na ari ya kiongozi kwa kuwapa wananchi hamasa.HONGERA RAIS MAGUFULI TUPO NYUMA YAKO JEMADARI WETU KTK VITA HII YA TANZANIA MPYA,NA KAMA UNAVYOTUSIHI MARA NYINGI KTK HOTUBA ZAKO KUWA TUKUOMBEE KWA MUNGU,TUNAKUOMBEA KWAKE ILI AZIDI KUKUPA AFYA MOYO WA UZALENDO PAMOJA NA MAARIFA YA KUTUONGOZA.

Tunawaomba na wasaidizi wako ktk nyanja mbalimbali wasikuangushe na pia sisi wananchi tushirikiane kukuunga mkono ktk kutekeleza kwa bidii na nguvu zote (HAPA NI KAZI TU!)wajibu na majukumu yetu ktk nafasi zetu za kazi .
Tunamuombea tunamuombea. Naona hii usafi wa kila Jumamosi ya wiki imekubalika koote ambao bado kubalini hili.Mimi niuko Zanzibar. Amini usiamini effect ni mpaka huku Zaniziba. KWa mfano Mtaa wetu tumejipangia wenyewe tunachangia Ths. 3,000 kwa mwezi. Kuna watu wamejiorganize wanapitia uchafu jumatano na Jumapili. Magufuli go Magufuli go we are vaery happy. na hii si si=uala la usafu tu hata uwajibikaji usikate tamaaa tuko pamoja na wewe!
 
Back
Top Bottom