Rais Magufuli aungwa mkono na BAKWATA kuzuia mikutano

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
2,000
BARAZA Kuu la Waislamu (Bakwata) wilayani ya Arumeru mkoani Arusha, limeunga mkono kauli ya Rais John Magufuli ya kusitisha mikutano ya hadhara ya kisiasa na kutaka watu kufanya kazi ili kuinua uchumi wa nchi.

Bakwata imesema kauli hiyo inapaswa kuungwa mkono na wananchi wote nchini na kuongeza kuwa siasa zisizokwisha, zinaweza kuyumbisha Watanzania na kuwafanya waache kufanya kazi na kuanza kuzungumza siasa katika muda wa kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Arumeru, Mwenyekiti wa Bakwata wilayani humo, Shehe Haruna Hussein, alisema kila kitu kina muda wake na mwisho wake, hivyo siasa zilikuwa na muda wake na sasa muda huo umekwisha, kinachofuata ni kufanya kazi kwa lengo la kujenga nchi na sio vinginevyo.

Alisema wao kama Bakwata wilaya ya Arumeru wanaunga mkono kauli ya kiongozi huyo ya kusitisha shughuli zote za kisiasa ikiwemo mikutano ya kisiasa na kutoa rai kwa wana siasa kutumia fursa hiyo kufanya kazi ya kuinua uchumi wa taifa Shehe Hussein alisema kauli ya Rais Magufuli inaweza kutafsiriwa tofauti, lakini ikiichunguza sana ina maana kubwa sana hivyo Bakwata inaunga mkono kwa sababu imeona mbali na kuamua kuiunga mkono kwa asilimia mia moja.

Akizungumzia utendaji kazi, Bakwata imemshauri Rais Magufuli kuwatumia baadhi ya viongozi wenye uzoefu na rekodi nzuri ya utendaji katika awamu zilizopita ili waweze kumsaidia kuboresha utendaji kazi katika serikali yake ya awamu ya tano.

Alisema Bakwata inaunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli katika kujenga serikali yake ila inatoa rai kwa Rais huyo kutowasahau wazee wenye busara na utendaji wao mzuri wa kazi.

Aidha baraza hilo lilimtaja aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu Dk Augustine Mrema kuwa ni moja wa viongozi wenye historia kubwa na utendaji kazi hasa falsafa yake aliyokuwa akitumia ya kutoa siku 7 katika kuwabana na kuwajibisha watendaji wabovu ambapo kwa kiasi kikubwa ilifanikisha kuwanyoosha watendaji hao.

Aidha walimtaka Rais Magufuli kuendelea kuwabana watendaji wabovu ambao hawataki kuendana na kasi yake katika kutekeleza majukumu ya kuwasaidia wananchi kuondokana na changamoto za maisha zinazowakabili.

Alisema Bakwata itaendelea kuliombea taifa pamoja na Rais Magufuli hili kila hatua anayoifanya iwe na Baraka zake mungu na kuomba mwenyezi mungu kumtangulia popote anapo kabiliana na kutokomeza ufisadi, rushwa wizi pamoja na wahujumu uchumi na wenye nia ovu na serikali yake.
 

Tyta

JF-Expert Member
May 21, 2011
12,774
2,000
kwani kwa kawaida mikutano huwa inafanyika mingapi katika sehemu husika?..
 

Godfrey-K

JF-Expert Member
Jan 5, 2016
1,926
2,000
Nani asiyejua kuwa BAKWATA ni kipaza sauti cha serikali? Serikali inatumia bakwata kufikisha Ujumbe wake kwa waislamu, ndio maana sishangai shekhe mkuu kuhudumiwa na serikali kuanzia ulinzi (bodyguard) mishahara, oc za ofisi magari, chakula na hata mishahara ya wafanyakazi wengine. IPO siku tutayaeleza kwa urefu.
 

NullPointer

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
3,465
2,000
Wao wadili na uislamu, mambo ya siasa waachie serikali.
Sipendi hii nchi tunavyochanganya udini kwenye siasa. Hakuna kitu kibaya sana kama dini ikija kwenye swala zima la siasa, wafuasi wa dini hua wanabeba kila wanachoambiwa tu bila kuquestion.
 

Sakhalala

JF-Expert Member
May 2, 2011
556
500
Jamani watu wa dini enezeni dini siasa si saizi yenu. Wewe ukiambiwa kuhubiri kuna mwisho utyakubali? Tuliona mlivyotishia kufanya ugaidi baada ya kuzuiliwa mihadhara, leo mnawaingilia wanasiasa kwa kuwaambia siasa ina mwisho.

Bwana shehe elewa kuwa wewe na taasisi yako umesajiliwa kama vilivyosajiliwa vyama vya siasa kwamba kwa kushadidia zuio la siasa yawezekana kesho ikaja kwako kama shehe kuwa hupaswi kuhubiri na shughuli za mahubiri mwisho wake umekwisha na waumini wako wakafanye kazi. Shughuli za kisiasa zinatawaliwa na sheria iliyowekwa kama ambavyo shughuli za kidini zinzvyotawaliwa na sheria pia. Kufanya siasa ni haki ya msingi ya binadamu kama ilivyo kufanya ibada.

Ninakushangaa sana muheshimiwa shehe unavyoshabikia upande mwingine kunyang'anywa haki hiyo wakati hiyo shughli yako pia inatawal;iwa na sheria inayofanana na hiyo.

Unaweza wewe kufurahi padri akija azuie wewe kufanya shughuli zako za kiimani?
Kwanini mwanasiasa amzuie mwanasiasa mwnenzie kufanya siasa? Pia hawa wanaofanya na wanaoshiriki siasa mliwahi kuwaona wakikusanyika misikitini na mabakuli wakiomba msaada?

Mheshimiwa Shehe unachofanya unashabikia kuondolewa kwa ngazi unayotumia nawewe kuipandia - tafakari.
 

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,642
2,000
Hawa BAKWATA waache kuwasemea Watanzania ambao wanajua HAKI ZAO KULINGANA NA KATIBA YA JMT!
Kinachoonekana hapa na kiko wazi kwa kila GTs wa JF ni kwamba,naomba niongea kwa herufi kubwa: RAIS JPM AMEFANYA KOSA LA JINAI KWA KUWAHONGA FEDHA WAISLAMU/BAKWATA WOTE SIKU YA IDD! KILA MTU ALIONA JINSI RAIS ALIVYOGAWA MABURUNGUTU YA FEDHA KWA WAISLAMU ZIKIWEMO MPAKA ZA KUENDEA HIJJA MECCA! HII FEDHA NDIYO IMEWATIA WAZIMU NA KUWAPOFUSHA WAISLAMU KIASI CHA KUSHINDWA KUTETEA KATIBA INAYORUHUSU KILA MTANZANIA KUKUTANA NA KUFANYA SIASA WAKTI WOWOTE NA MAHALI POPOTE!!!
 

Kete Ngumu

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
6,068
2,000
Hata makonda wa daladala lazima wapige debe ili wapate chochote kitu kutokana na nauli za abiria watakaoingia ktk daladala.
 

kivava

JF-Expert Member
Apr 2, 2013
5,778
2,000
Hakuna kitu kinaitwa BAKWATA Arumeru bali wahuni wa Ngarenaro wala mirungu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom