Rais Magufuli aunda kamati ya pili kuchunguza madini yaliyopo kwenye mchanga, kuapishwa kesho

Aache usanii na yeye, hivi unategemea tume zake hizi zitakuwa huru wakati alishatoa na hitimisho kabisa kuwa watanzania akituambia dhahabu iliyomo kwenye yale makontena tutalia.

Ni wazi Magufuli anaelekea kushindwa sasa, ila kama anashaurika bado ana mda wa kurekebisha mambo.

Nikiona baadhi ya Watanzania wenzetu wanatoa unhelpful comments kama za kwako nabaki najiuliza maswali mengi!! Unataka kutueleza mtaalamu aliye bobea katika fani ya Kemia hajui alisemalo??
 
Kitendo tu cha kusema hasara, 18% yake, ni chanzo cha Taarifa na mapato yetu waliyokuwa wanatudhurumu. Watengeneza na wapitisha sheria now, wamesababisha haya
 
Kwa nini kusingekuwa na kamati moja inayojumuisha wataalam wa fani tofauti? Siamini kuwa na kamati nyingi ndiyo ufanisi wa kiutendaji.
 
mkuu hii ni muhimu sio kwako tu bali hadi kwa watukuu wako.
Kukwepa kuruhusu kujua yanayoendelea kwenye madini ni kuendelea kutunza tatizo na malalamiko ambayo wenda majibu yake yangetafutwa rasmi 1998,2001 au 2009 leo tungekuwa tunafanya kazi nyingine za maendeleo.
Rais yuko sahihi kuwasiliana na wananchi wake kila anapoona inafaa.
Kulikwishafanyika uchunguzi siku za nyuma. Na ripoti zipo.

Kama kila atakayekuja atafanya utafiti wake, hili litakuwa Taifa la namna gani? Jambo hili kuna watu wanafahamu kila kitu, shida ni kwamba tunataka kuambiwa kisichokuwepo. Tukiambiwa ukweli ambao hatuutaki, tunaona siyo kweli, ili kupata tunachotaka kusikia ni kuendelea kuunda kamati mpya mpaka siku tutakapoipata kamati itaayotuambia tunachotaka kusikia.
 
Back
Top Bottom