G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Mwaka 2015 mwishoni Kikwete ambaye muda huo alikuwa rais wa Tanzania alitaka kuzindua mradi wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kubeba mizigo mizito zaidi (standard gauge) lakini baadaye alibaini kuwa asingeweza walau kupata fedha za kuanza mradi huo ikabidi auachilie mbali.
Juzi juzi hapa rasi Magufuli akazindua ujenzi huo na kutangaza rasmi mchakato wa tenda kw ajili ya kumpata mkandarasi.
Baadaye kidogo gazeti la serikali la kila siku likatangaza kwenye ukurasa wa mbele tena kwa habari kuu kuwa benki ya Exim kutoka China imekubali kutoa mkopo wenye riba nafuu wa Tshs trilioni 17.5 kwa ajili ya kuanza rasmi na kukamilisha ujenzi huo wa reli ya kati huku serikali ya Tanzania ikitangaza kutoa Tshs. trilioni 1 kwa ajili ya hatua za awali za mradi huo.
Juzi tena rais Magufuli akamgeukia rais wa India na kumuomba mkopo wa kiasi kilekile cha fedha ili kufanikisha ujenzi wa reli ya kati.
Sasa tumeanza kubaini kuwa kinachoendelea kuhusu mradi huo ni porojo tu za hapa na pale huku ukweli ukibaki kuwa hakuna fedha zilizopatikana (iwe mkopo au msaada) kwa ajili ya mradi huo.
Ilikuwaje gazeti la serikali likaiongopea nchi? Ilikuwaje kuanza mchakato wa tenda bila kuwa na fedha wala chanzo cha uhakika cha kupata fedha hizo?
Yapo madai yaliyotolewa na Zitto ambayo mimi nyaamini hasa kutokana na hali halisi ya sasa kuwa benki ya Exim ya China imeshajitoa katika mradi huo kutokana na sintofahamu iliyojitokeza ikiwemo serikali kuvunja makubaliano kati yao kinyemela.
Sasa serikali itueleze mpango kamili wa mradi huo na siyo kuendeleza porojo ambazo kwa hakika zimeonekana dhahiri kuutawala mradi huu.