Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,944
- 18,652
Rais Magufuli wakati akihutubia taifa 22, apr, 2020 aliomba taasisi za fedha za kimataifa (WB na IMF) kuangalia namna ya kuzisaidia nchi za Afrika, kwa aidha kuzifutia madeni au kuangalia namna ya kupitia upya riba za madeni hayo, kwa maana ya kuzipunguza badala ya kuruhusu nchi hizo kukopeshwa tena, ikiwa na maana ya kurundikiwa madeni tena wakati hakuna shughuli za uzalishaji mali (kiuchumi)kama ilivyokua kabla ugonjwa huu.
Kwakuwa ameshatambua kuwa uzalishaji umeshuka na hata biashara hapa nchini zimeshuka kwa kiasi kikubwa kutokana na ugonjwa wa corona, kwanini na yeye aendelee kukusanya kodi na madeni kwa wafanyabiashara? Kwanini asiwasamehe madeni wafanyabiashara au akaacha kukusanya kodi kipindi hiki kama alivyoshauri WB?
Hivi WB wanaanzaje kukusamehe madeni wakati wewe mwenyewe unaendelea kukusanya kodi kwa wananchi wako?
Nafikiri hata WB wakiamua kufata huu ushauri, hawataweza kusamehe kila nchi. Lazima waangalie mataifa yanayofanya juhudi kusaidia wananchi wake kupambana na hili janga, kiuchumi na kiafya kiujumla.
Je, Tanzania imefanya juhudi gani mpaka sasa ili isamehewa madeni?
Sijasikia hata serikali ikizuia mabenki kupokea marejesho ya mkopo kipindi hiki.
Sent using Jamii Forums mobile app