beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Ameelezeka maagizo hayo kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara baada ya Kampuni hiyo, Sugar Investment Trust(SIT) kucheleweshwa kuwekeza katika uzalishaji wa sukari tangu mwaka 2017
Ametoa maagizo hayo leo Aprili 17, 2019 akiwa Ikulu jijini Dar baada ya kukutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo kutoka Mauritius, Gansam Boodram aliyeongozana na Balozi wa Mauritius nchini, Jean Pierre Jhumun
Boodram ameeleza kuwa yupo tayari kulima ekari 25,000 za mashamba ya miwa na uwekezaji huo utawezesha kuzalishwa kwa tani 125,000 za sukari, kutoa ajira za kudumu 3,000 na ajira za muda 5,000
Rais ameagiza ufanyike uchambuzi wa haraka katika maeneo ya Bonde la Mto Rufiji Mkoani Pwani, shamba la Mkulazi Mkoani Morogoro na eneo la Kibondo Mkoani Kigoma ili mwekezaji huyo aanze mara moja uwekezaji
Aidha, amezionya Taasisi za Serikali kikiwemo Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kwa kutoharakisha taratibu za kuwawezesha wawekezaji kuwekeza
Sent using Jamii Forums mobile app