Rais Magufuli atoa onyo kwa wanaojenga mabondeni, wakipata madhara wasiilaumu Serikali

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Rais wa Tanzania, John Magufuli amewataka wananchi kujihadhari kujenga nyumba kwenye maeneo ambayo kuna mkondo wa maji.

Mkuu huyo wa nchi ametoa tahadhari hiyo leo Jumatano Desemba 18, 2019 wakati anazindua mradi wa Visima vya maji Chato na kuzungumza na wananchi wa Chato katika uwanja wa Shule ya Msingi Chato mkoani Geita.

Akitolea mifano ya maeneo ambayo wananchi wamejenga mabondeni, amewataka kuchukua tahadhari wanapojenga nyumba zao ili wasije wakailaumu Serikali badaye.

“Ninajua siku nyingine mvua zinazidi kidogo lakini wakati mwingine tunazichokoza mvua sisi wenyewe mfano pale Sengerema (Mwanza) kuna bwawa linaloteta maji, watu wamelivamia lile bwawa mpaka njia ya kutolea maji kwa kujenga nyumba na maji yamekuja yametuletea madhara mpaka vifo vya watu” amesema

Amesema hata Dar es Salaam kuna watu wamejenga hadi kwenye mto Msimbazi hivyo wasije wakailaumu Serikali.

Mwananchi
 
Mimi nashauri itungwe sheria kwamba anayejenga kwenye mkondo wa maji ashtakiwe sawasawa na mtu aliyejaribu kujiua.
 
Back
Top Bottom