Rais Magufuli atoa Ndege kusafirisha Mwili wa aliyekuwa Katibu Tawala Arusha kwenda Mwanza

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Iddy Kimanta amesema kuwa mwili wa aliyekuwa katibu Tawala mkoa wa Arusha Richard Kwitega aliyefariki jana kwa ajali ya gari, utaagwa kesho katika uwanja wa mpira wa Sheikh amri abed jijini Arusha na Kisha kusafirisha kwa ndege ya serikali iliyotolewa na Rais Magufuli, kwenda Mkoani Mwanza kwa mazishi yatakayofanyika siku ya jumamosi wilayani Sengerema, nyumbani kwa marehemu.

Marehemu Kwitega alipoteza maisha hapo Jana katika eneo la Mdorii Mkoani Manyara wakati akielekea Dodoma Kikazi ambapo Dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo amelazwa katika hospital ya Mkoa iliyopo mjini Babati akipatiwa matibabu baada ya kunusurika.

IMG_20210204_154650_575.jpg
FB_IMG_1612374016240.jpg
 
Tujihadhari na hizi kauli za ukabila, kauli hizi hazitatufikisha popote, kauli hizi zitatugawa na taifa hili ni bado changa. Ukabila uijieruhi Ethiopia na nchi zingine za maziwa makuu. Kusafirishwa na ndege ya serikali au ndege binafsi yote ni sawa. Apumzike kwa amani Kitega!
 
Ndege hazina kazi, maana zimezuiwa kuruka kila kona. Ndiyo maana zinapasha injini kwenye misiba ili injini zisi-knock.

Nchi imepewa level 4 ya korona. Hakuna cha kupeleka mbuzi Dubai wala kwenda kuchbeba watalii.

Sasa hivi ndege zitabaki kuwa mazalia ya popo na zitakuwa zinabeba misiba mpk ya madiwani wa Chato.
 
Back
Top Bottom