Rais Magufuli atoa msaada wa zulia la kuswalia na Tsh 2M kwa msikiti wa Noor kijijini Mkange, Chalinze mkoani Pwani

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waumini wa dini ya Kiislam wa Msikiti wa Noor uliopo katika Kijiji cha Mkange, Miono, Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani, wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa msaada wa zulia la kuswalia na fedha taslim Shilingi milioni Mbili.

Zulia pamoja na fedha hizo zimekabidhiwa na Msaidizi wa Rais Kanali Mbaraka Mkeremy kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Imamu wa Msikiti huo Alhaji Sheikh Khamis Nassor wa Msikiti Noor uliopo katika kijiji cha Mkange, Wilaya ya Chalinze mkoa wa Pwani.

Mara baada ya kukabidhi Zulia na fedha hizo, Kanal Mkeremy kwa niaba ya Rais Magufuli amewataka waumini wa Msikiti huo kutumia msaada huo kwa lengo lililokusudiwa.

Akiungumza mara baada ya kukabidhiwa Msaada huo, Sheikh Nassor amesema kwa niaba ya waumini wa Msikiti huo wanamshukuru Mhe. Rais kwa kuitikia ombi lao la kupata zulia, na kwamba kwa kutimiza ahadi yake hiyo Mhe. Rais amedhihirisha kuwa yeye ni mtu wa watu asiyebagua dini wala kabila katika kusaidia jamii ya kitanzania.

Sheikh Nassor amesema waumini wa msikiti huo wanamuombea na wataendelea kumuombea Mheshimiwa Rais na kuwataka watanzania wote nchini kuungana nao kumuombea Rais bila kujali itikadi za kisiasa ama imani za kidini kwani anayoyafanya Rais kwa wananchi wa Tanzania ni kwa manufaa ya wananchi wote.

Jaffar Haniu

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Pwani

17 Novemba 2017.
 
mkuu hicho kijikapeti we unacho nyumbani ndo maana unadharau.....sasa tunaomba utuambie kitu kikubwa zaidi ya kijikapeti ulichotoa msaada sehemu yako ya ibada
Nikwambie ili iweje? kwanza we kama nani? ok tu assume nimekwambia enhe? kifuatacho?
 
Milioni mbili kwa rais ni pesa ya kutangaza hivyo si matusi hayo...hivyo si petty cash tu ....ni kushushia hadhi jina la rais ,mimi angalau nilifikiri kaamua kuujenga msikiti all together ..ndio iwe na hadhi ya kutangazwa
 
hiyo sadaka ikishatangazwa hua batili na tena serikali kweli inatoa taarifa rasmi kwa kutoa kijikapeti cha 1ml
 
f7c5a2252bd260d4f1d36ea4859ea64a.jpg
Waumini wa dini ya kiislaam wa msikiti wa Noor uliopo katika kijiji cha Mkange, Miono Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani, wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa msaada wa zulia la kuswalia na fedha taslimu shilingi milioni mbili.

Zulia pamoja na fedha hizo zimekabidhiwa na Msaidizi wa Rais Kanali Mbaraka Mkeremy kwa niaba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa Imamu wa msikiti huo Alhaji Sheikh Khamis Nassor wa Msikiti wa Noor ulipo katika kijiji cha Mkange, wilayani Chalinze Mkoa Pwani.

Mara baada ya kukabidhi zulia na fedha hizo, Kanali Mkeremy kwa niaba ya Rais Magufuli amewataka waumini wa msikiti huo kutumia msaada huo kwa lengo lililokusudiwa.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa msaada huo, Sheikh Nassor amesema kwa niaba ya waumini wa msikiti huo wanamshukuru Mhe Rais kwa kuitikia ombi lao la kupata zulia, na kwa kutimiza ahadi yake hiyo.

Mhe. Rais amedhihirisha kuwa yeye ni mtu wa watu asiyebagua dini wala kabila katika kusaidia jamii ya kitanzania.

Sheikh Nassor amesema waumini wa msikiti huo wanamuombea na wataendelea kumuombea Mh. Rais na kuwataka watanzania wote nchini kuungana nao kumuombea Rais bila kujali itikadi za kisiasa ama imani za kidini kwani anayoyafanya Rais kwa wananchi wa Tanzania ni kwa manufaa ya wananchi wote.

Jaffar Haniu

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Pwani

17 Novemba 2017.
 
Kuna kipindi Mbowe alitoa msaada wa ujenzi wa msikiti kama milioni 30, waislamu wakamsema sana na wengine kumkashifu kuwa anatoa sadaka na matangazo, kusema uislamu ukitoa sadaka hutakiwi kutangaza. Ajabu leo milioni mbili na mswala wako kimya na wengine wanapongeza
 
mkuu hicho kijikapeti we unacho nyumbani ndo maana unadharau.....sasa tunaomba utuambie kitu kikubwa zaidi ya kijikapeti ulichotoa msaada sehemu yako ya ibada
Hapana.....kwa heshima ya Rais ......tena wa nchi hii ni kidogo tena ... .kapeti....daaaaaaa
 
Takbiiiir.
Hapo mwenyezi Mungu kamuona.
Kutoa ni moyo sio utajiri.
Tz hakuna udini sema kuna wapumbavu wachache sana ndio hawajui
 
Back
Top Bottom