Rais Magufuli atoa maagizo kuwaokoa viboko Hifadhi ya Taifa Katavi

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
Rais John Magufuli ameiagiza Mamlaka ya Hifadhi za Wanyamapori nchini (Tawa) kuchimba bwawa na kujaza maji kwa ajili ya viboko wanaoishi katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Alhamisi Oktoba 10, 2019 wakati akizungumza na wananchi wa Mpanda Mjini ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani Katavi.

Amesema alipita kwenye hifadhi ya Katavi na kuona maji yakiwa yamekauka kwenye mto wenye viboko na baadhi wameanza kupasuka kutokana na kupigwa jua. “Ninawaagiza Tawa kuanzia kesho wapeleke maji wachimbe bwawa wajaze maji.

Wanyama hao wanatuingizia fedha nyingi, kwa nini tushindwe kuwatunza,” amesema Rais Magufuli. Wakati huo huo, Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kufungua mabucha ya nyamapori kwa ajili ya watu wa Mpanda.

Amesema maisha bora kwa Watanzania ni pamoja na kunufaika na rasilimali zao. “Watu wa maliasili leteni hapa bucha ya nyamapori hata mara moja kwa wiki. Haya ndiyo maisha bora kwa kila Mtanzania.

Haiwezekani umezaliwa karibu na hifadhi lakini hujawahi kula nyama ya porini,” amesema Rais Magufuli. Kuhusu suala la wakimbizi, amesema baadhi wamekuwa wakijihusisha na ujambazi na kuibua hofu kwa wakazi wa Mpanda. Amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa wote watakaobainika
 
Management ya wanyama pori inafuata nature au inakwenda kiasilia bila binadamu kuingilia.
Wakifa sana kwa ukame na hutokea kila mwaka, ni sehemu ya ikolojia ya sehemu husika. Fisi watapata chakula. Pengine hata Simba. Ndiyo nature. Kuingilia ni kuharibu huo mtiririko.
Kesho atasema wale nyumbu wajengewe daraja mto Mara wasiliwe na mamba. Halafu mamba wale nini?
Aelimishwe asivamie taaluma za watu.
 
Usemayo ni ya kweli ,lkn kuna haja ya kutafakari zaidi kuhusu hiyo nature, kumbuka kuna mabadiliko ya Tabia ya nchi ,yanaipelekesha dunia ,kwhy tafakari.
Management ya wanyama pori inafuata nature au inakwenda kiasilia bila binadamu kuingilia.
Wakifa sana kwa ukame na hutokea kila mwaka, ni sehemu ya ikolojia ya sehemu husika. Fisi watapata chakula. Pengine hata Simba. Ndiyo nature. Kuingilia ni kuharibu huo mtiririko.
Kesho atasema wale nyumbu wajengewe daraja mto Mara wasiliwe na mamba. Halafu mamba wale nini?
Aelimishwe asivamie taaluma za watu.
 
“Ninawaagiza Tawa kuanzia kesho wapeleke maji wachimbe bwawa wajaze maji.

Hii kali, miradi ya maji kwa binadamu imekwama lakini viboko wapelekewe maji kesho, nakumbuka kauli ile ya waziri ya atakayewasumbua twiga apigwe risasi, ipo siku nchi itabakia na wanyama tu binadamu watatoweka kwa either kupigwa risasi au kukosa huduma muhimu.
 
Management ya wanyama pori inafuata nature au inakwenda kiasilia bila binadamu kuingilia.
Wakifa sana kwa ukame na hutokea kila mwaka, ni sehemu ya ikolojia ya sehemu husika. Fisi watapata chakula. Pengine hata Simba. Ndiyo nature. Kuingilia ni kuharibu huo mtiririko.
Kesho atasema wale nyumbu wajengewe daraja mto Mara wasiliwe na mamba. Halafu mamba wale nini?
Aelimishwe asivamie taaluma za watu.
Acha uongo ndugu ,mbona mbuga ya Lake Babati wamechimba bwawa kwa ajili ya hao hao viboko na wanyama wengine ,pia nadhani huelewi unachozungumza,ni kwamba huo mto hapo nyuma ulikuwa haukauki maji,viboko waliishi salama,lakini baada ya shughuli za kilimo na mifugo kuanza kuvamia hilo eneo ndio tatizo la maji kukauka lilipo anza,kwa hiyo hapo ikolojia unayoisema haipo
 
Kila ikolojia ina namna yake. Katavi NP Ina viumbe wengi.
Tatizo huna elimu ya ikolojia. Tulia.
 
Naunga mkono hoja, viboko waokolewe ila tusiishie kuokoa viboko tuu bali hata adhabu ya viboko ifutwe, ni udhalilishaji.
P
Mkuu viboko vina heshima yake, ingawa vinauma lakini haviui.

Viboko vinaondosha viburi vichwani mwa watu na kurejesha heshima, potelea kwa mbali hata iwe ni heshima ya uoga.

Chukulia viboko vilivyotembezwa na Rc sikuile, unadhani hao watoto watakuja kurudia tena ujinga 'kabila hiyo' maishani mwao?

Sisi wenyewe tulilambwa mboko tukanyoosha maneno, tukapigana vita na ushindi ukapatikana(kalitaka kutokea kamgomo ka uzanzibar/bara, ama ni uoga tu wa mtutu wa adui) ingawa sisemi ni wapi!

Mkuu viboko ni dawa.
 
Kweli ni dawa ila matokeo yake ni kuharibu vipawa vya uvumbuzi vya watoto wetu!. Angalia wasomi wetu wamevumbua nini?.

Chuo Kikuu tunafundisha English Literature toka uhuru, where is our Ngungi wa Thiongo or our Chunua Achebe?, ni kutokana na viboko.
Tuache adhabu za inflicting pain to our kids tubuni adhabu mbadala.

Wanyama viboko walindwe ila viboko mashuleni...
P
 
Management ya wanyama pori inafuata nature au inakwenda kiasilia bila binadamu kuingilia.
Wakifa sana kwa ukame na hutokea kila mwaka, ni sehemu ya ikolojia ya sehemu husika. Fisi watapata chakula. Pengine hata Simba. Ndiyo nature. Kuingilia ni kuharibu huo mtiririko.
Kesho atasema wale nyumbu wajengewe daraja mto Mara wasiliwe na mamba. Halafu mamba wale nini?
Aelimishwe asivamie taaluma za watu.
Si vyema kukariri aisee. Jiulize mbona wanyama wanatibiwa na kunafanyika udhibiti wa mbung’o( Tsetse flies) hatusemi ecology?
Hukusikia stori iliyovuma mwaka jana ya Simba mdogo aliyefanyiwa operation ya hernia Ngorongoro!
 
Management ya wanyama pori inafuata nature au inakwenda kiasilia bila binadamu kuingilia.
Wakifa sana kwa ukame na hutokea kila mwaka, ni sehemu ya ikolojia ya sehemu husika. Fisi watapata chakula. Pengine hata Simba. Ndiyo nature. Kuingilia ni kuharibu huo mtiririko.
Kesho atasema wale nyumbu wajengewe daraja mto Mara wasiliwe na mamba. Halafu mamba wale nini?
Aelimishwe asivamie taaluma za watu.
Ulichoandika Ni ujinga mtupu.majii ni mahitaji muhimu kwa wanyama wote sio viboko tu.Hivyo Kama mito inakauka wanyama wote watakufa SI viboko peke yao.Huna Cha taalumaa Wala Nini wewe mjinga tu.Serengeti kukitokea Ukame wanyama huhamia Kenya na baadaye kurudi.Mpanda hawana pa kwenda Ina maana unataka wafe? Kama hiyo ndio taaluma uliyosomea mzazi wako alipoteza pesa zake bure
 
Management ya wanyama pori inafuata nature au inakwenda kiasilia bila binadamu kuingilia.
Wakifa sana kwa ukame na hutokea kila mwaka, ni sehemu ya ikolojia ya sehemu husika. Fisi watapata chakula. Pengine hata Simba. Ndiyo nature. Kuingilia ni kuharibu huo mtiririko.
Kesho atasema wale nyumbu wajengewe daraja mto Mara wasiliwe na mamba. Halafu mamba wale nini?
Aelimishwe asivamie taaluma za watu.
@Sibonike kukauka kwa maji ya mto nayo ni nature si ndivyo..?? Ebu sumbua ubongo wako kidogo.
 
Back
Top Bottom