Rais Magufuli ateua Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wazima na Mwenyekiti Baraza la Ushindani

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
IMG_20190220_161804.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Michael Wilfred Ng’umbi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Ng’umbi alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Open University of Tanzania – OUT)

Dkt. Ng’umbi amechukua nafasi ya Dkt. Fidelice Mafumiko ambaye ameteuliwa kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Jaji Stephen Mrimi Magoiga kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal – FCT)

Jaji Magoiga amechukua nafasi ya Mhe. Jaji Barke Mbaraka Sehel ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hawa umeanza tarehe 19 Februari, 2019.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

20 Februari, 2019
 
Mzee bana atasubiri sana
 
Mbona napitwa tuu, kwamba niongeze kuvunja nazi. Ila kuna thread hapa Jf PM akionya ma DED na ma DC waache kurogana
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

*Mungu Ni Mwema Wakati Wote*
 
Again and again teuzi kwa kwenda mbele...

Nishasema hapo mwanzo Mkuu ni mkabila ona sasa kila siku wasukuma wanateuliwa ni elimu yako...
 
Back
Top Bottom