Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa Ikulu jijini hapa, leo (Alhamisi). Rais Mkapa amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kumpa taarifa juu ya kazi anayoendelea kuifanya ya kuwa mwezeshaji wa mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.