Rais Magufuli atengua uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dkt. Ave Maria Semakafu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,796
11,959
792511D1-DAFC-4EB0-B19A-33099BEE7AEC.jpeg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Oktoba, 2020 ametengua uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu.

Nafasi hiyo itajazwa baadaye.


PIA SOMA
= > Siku ya Mwalimu Duniani: Wizara ya Elimu yafuta rasmi mafunzo ya Ualimu wa shule ya msingi na awali ngazi ya Cheti Tanzania

= > News Alert: - Dodoma: Rais Magufuli apiga simu mubashara kwenye Kongamano la CWT na kukanusha kufutwa kwa Ualimu Ngazi ya Cheti
 
Maamuzi mazito Kama Yale ni ngumu kuwa maamuzi bila Baraka toka juu, anawatumia wenzake Kama mpira
Kabisa! Huyu mama katolewa kafara. Uamuzi wa kubadili sera usingeweza kufanyika bila ridhaa ya baraza la mawaziri ambapo Rais ni mwenyekiti, wizara inatekeleza tu.

Sasa hapa eti tunaaminishwa kwamba uamuzi huo ulifanya na NAIBU katibu mkuu? Wala sio katibu mkuu au naibu waziri au waziri? Hizi hadaa nyingine hapana..
 
Kabisa! Huyu mama katolewa kafara. Uamuzi wa kubadili sera usingeweza kufanyika bila ridhaa ya baraza la mawaziri ambapo rais ni mwenyekiti, wizara inatekeleza tu. Sasa hapa eti tunaaminishwa kwamba uamuzi huo ulifanya na NAIBU katibu mkuu? Wala sio katibu mkuu au naibu waziri au waziri? Hizi hadaa nyingine hapana..

Hizi sarakasi za Magufuli huwa zinajulikana.
Ahamashishe wenzake wampige chini October
 
Hapo mbwa kala mbwa.
Japokuwa kile kimama kimeonewa, lakini kile kimama kilikuwa na nyodo za kiCCM sana, kilikuwa kinajiona kimeshafika pale kisa kuteuliwa na Rais. Leo kimetumbuliwa usiku usiku. Huko kilipo lazima kipandishe sukari.

Yote kwa yote walimu walishaamua kuitosa CCM na Magufuli kwenye uchaguzi huu. Oktoba 28, kichapo kipo pale pale. Magufuli ajipange kulizwa tu.
 
Back
Top Bottom