Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha kupisha uchunguzi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,883
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ametengua Rasmi nafasi ya Mtendaji Mkuu wa shirika la Elimu Kibaha Dkt Crispin Mpemba ili kupisha uchunguzi wa Tuhuma mbalimbali za kiutendaji zinazomkabili.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Rebecca Kwandu Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini Kutoka Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa imeeleza kuwa kwa sasa nafasi hiyo inakaimiwa hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.

------
Iliwahi kujadiliwa hapa JF kuhusu mradi wenye harufu ya ufisadi, zaidi soma Shirika la Elimu Kibaha, mkataba huu una harufu ya rushwa, uchunguzwe
 
Bora wamemtoa. Pesa ya call allowances yeye anaitumia kulipia bills za umeme na maji. Aende zake huko
 
Tuhuma za huyu mtu,ziliandikwa kwa kirefu sana na gazeti la MwanaHalisi.
Na katika kuandika kwake,likaingia kwenye mgogoro na ofisi ya Rais Ikulu,maana kichwa cha Habari kilionyesha kama Rais anahusika na ubadhirifu wa Shirika la Elimu Kibaha.

Mgogoro ule ulifanya MwanaHalisi lipewe masaa 48 kukanusha la sivyo litafungiwa,walikanusha na kukubaliwa...bila shaka ofisi ya Rais ilifuatilia na kujiridhisha juu ya tuhuma zile.

Kwa hiyo kumbe watu waendelee tu kupaza sauti,na ili Rais achukue hatua,inabidi kuwe na "ujanja" wa kumuhusisha na tuhuma,halafu ukiambiwa ukanushe na kuomba radhi,unaomba tu...Maana Rais akihusishwa anakasirika haraka na kuchukua hatua za uchunguzi.

Hata hili la Bashite,inawezekana linachelewa sbb hajaguswa moja kwa moja!!
 
Kumbe ile habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Mwanahalisi ilikuwa na chembe chembe za Ukweli, maana walichokisema Mwanahalisi leo hii rais kaamua kukifanyia kazi.

Hongera sana Mwanahalisi.
Wale wapuuziii waliotaka kulifungia gazeti la mwanahalisi waje sasa kuliomba radhi hadharani gazeti la Mwanahalisi na sisi watanzania.
 
Pale Kibaha kuna mengi zaidi, kuanzia kwenye COTC mpaka Hospitalini Tumbi.
Watu wa pale bado wako katika enzi za business as usual.
Hata bosi wa Kibaha COTC aondoke tu....
 
Tuhuma za huyu mtu,ziliandikwa kwa kirefu sana na gazeti la MwanaHalisi.
Na katika kuandika kwake,likaingia kwenye mgogoro na ofisi ya Rais Ikulu,maana kichwa cha Habari kilionyesha kama Rais anahusika na ubadhirifu wa Shirika la Elimu Kibaha.

Mgogoro ule ulifanya MwanaHalisi lipewe masaa 48 kukanusha la sivyo litafungiwa,walikanusha na kukubaliwa...bila shaka ofisi ya Rais ilifuatilia na kujiridhisha juu ya tuhuma zile.

Kwa hiyo kumbe watu waendelee tu kupaza sauti,na ili Rais achukue hatua,inabidi kuwe na "ujanja" wa kumuhusisha na tuhuma,halafu ukiambiwa ukanushe na kuomba radhi,unaomba tu...Maana Rais akihusishwa anakasirika haraka na kuchukua hatua za uchunguzi.

Hata hili la Bashite,inawezekana linachelewa sbb hajaguswa moja kwa moja!!
Acha kukumbatia mchezo mchafu.Hata ukitumia huo ujanja kumhusisha rais kama huna facts itakula kwako.
Mwanahalisi walitumia jina la Rais ili wauze tu gazeti ingawa walikuwa na facts,lakini wasingeuza gazeti kwa kuanika uozo KEC.Bila ya kumuandika Magufuli au Makonda huuzi gazeti hao ndio ma Star wetu kwa sasa!
Usijaribu kumchafua Rais,ili tuhuma zako ziwe na mashiko,jenga hoja nzito tu. Hata iweje,kwa Magufuli haachwi mtu
 
Magu kama unanyia kazi taarifa za kiuchunguzi za mwanahalisi usisahau na tuhuma Daudi Bashite zilizoelezwa na Mwanahalisi tarehe 6/3/2017
IMG-20170306-WA0009.jpeg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ametengua Rasmi nafasi ya Mtendaji Mkuu wa shirika la Elimu Kibaha Dkt Crispin Mpemba ili kupisha uchunguzi wa Tuhuma mbalimbali za kiutendaji zinazomkabili.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Rebecca Kwandu Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini Kutoka Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa imeeleza kuwa kwa sasa nafasi hiyo inakaimiwa hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.

------
Iliwahi kujadiliwa hapa JF kuhusu mradi wenye harufu ya ufisadi, zaidi soma Shirika la Elimu Kibaha, mkataba huu una harufu ya rushwa, uchunguzwe

SERIKALI INA UBAGUZI HII .....KUNA MAKUNDI YA WATEULE ......WA NYUMBANI AMBAO WAO HATA WAHARIBU VIPI HAWAPEWI HATA ONYO....
ALAFU WALIO WENGI NDIO HAO AMBAO WAMEANDIKWA KWA CHAKI AMBAO KUTWA WANATISHIWA KUFUTWA

SAD
 
Back
Top Bottom