Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anna kilango Malecela kuanzia leo.

Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Anna kilango Malecela kutungaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.

Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa na hali hiyo na kuagiza Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa kuondolewa ofisini mara moja.

IMG-20160411-WA0025.jpg

IMG-20160411-WA0026.jpg

P1280683.JPG

Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga(kushoto),mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi na wakurugenzi wa halmashauri 6 za wilaya mkoa wa Shinyanga
 
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Bi. Anne Kilango Malechela kama Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuanzia leo tarehe 10/04/2016.

Uamuzi huo umekuja baada ya kudaiwa kutoa taarifa za uongo kuwa Mkoa huo hauna watumishi hewa na baada ya tume nyingine kuchunguza ilikuta watumishi hewa 45.

Mwingine aliyetumbuliwa ni Katibu Tawala wa Mkoa.

Source: East Africa Radio
 
WATUMISHI HEWA WAMPONZA KILANGO: Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela na Katibu Tawala wa mkoa huo kwa kutoa taarifa za uongo kuwa mkoa huo hauna watumishi hewa baada ya tume nyingine kuchunguza na kubaini uwepo wa watumishi hewa 45. (source Mwananchi)
 
View attachment 336536

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anna kilango Malecela kuanzia leo.

Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Anna kilango Malecela kutungaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.

Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa na hali hiyo na kuagiza Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa kuondolewa ofisini mara moja.

Chanzo: ITV
Ona sasa tangu lini mwanamke akawa chifu wa wasukuma! Lazima karogwa tu na vizee kwa Ibadakuli.
 
Back
Top Bottom