Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Igunga kwa kutwaa ardhi ya wananchi bila kufuata taratibu

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,426
7,736
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Revocatus Kuuli.

Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Kuuli leo Desemba 28, 2020 kutokana na kukabiliwa na tuhuma za kutwaa ardhi ya wananchi bila kufuata utaratibu, utendaji kazi usioridhisha na matumizi mabaya ya fedha za maduhuli ya Serikali.

JPM amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Phillemon Sengati kuteua Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo mara moja.

IMG-20201228-WA0014.jpg
 
Mkurugenzi hata akitumbuliwa bado hawezi tena kuwa masikini!

Kama kweli kaharibu AFUNGWE
 
Rushwa na ubadhirifu wa pesa za walipa kodi ndo uti wa mgongo wa fisiem

#mi5tena
 
Huyu huyu ndie aliiba kura za wapinzani akawapa CCM. Sasa kuna shida gani na wizi kafundishwa na CCM?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom