Rais Magufuli atekeleza agizo la Makonda la ukaguzi wa silaha, apeleka bunduki zake

Kweni kabla hajawa rais kwa nini hakupata hyo hasira aje aipate ghafla sasa hv?yani waTZ bwana dah!

Kuuliza si ujinga.Ninauhakika gani kama ameinunua juzi??Na hasira inapimwa wakati au muda?
 
Na mimi nashangaa kwa nini unashangaa Rais ana silaha, hivi unajua kulenga shabaha ni hobby?

Kwa hiyo ikisha kuwa hobby.Hujajibu swali langu bado.Inawezekana kwa kushangaa kwangu siko peke yangu kuna wengi nyuma yangu wanasubiria majibu
 
Yaani sasa kulikuwa na haja gani ya Rais kupiga picha na kusambaza huku akionyesha hadharani silaha anayomiliki?

Hivi ni Ulimbukeni au ni kujisahau tu?

Ashauriwe maana sioni kama utetezi wa Kuwa anaonyesha mfano mwema utakuwa na maana.
Jifunze kuacha chuki kwenye mambo ya kawaida...Raisi ni taasisi..media lazima iandike na ameonyesha mfano kutii sheria....mambo mengine tuchangie tukiwa "sober"..ili kuweka heshima na akiba itakayokuwezesha angalau kuwa na fursa ya majadiliano!
 
Kwa hiyo ina maana marais waote walikuwa wanamiliki silaha.Tatizo sijawahi kuwaona wakijionyesha publically,labda ndiyo ujinga wangu unapofikiria
1) Kama marais wote walikuwa wanamiliki silaha siyo hoja
2)Kwaba mmiliki silaha mmoja ambaye anatokea kuwa rais amejitokeza kudhibiti silaha zake hiyo ndiyo hoja.
3)Kutokujua siyo ujinga, ujinga ni kutokutafuta maalifa hata yakiwa mbele yako.
4)Kuna sababu kwa nini JPM amefanya alichokifanya.
 
I don't get it that Rais anatembea na silaha wakati anao walinzi wanaomzunguka muda wote wakiwa na silaha za kumlinda?
Nadhani alikwenda kuhakiki sasa ulitaka ile silaha aikodishie TAXI, kuibeba kwa wakati ule sidhani kama anamaanisha anatembea nayo wakati wote, kumbuka miezi 6 ilopita alikuwa ni waziri tu na hakuwa rais, Je? ulitaka baada ya kuapishwa aitupe baharini?? ni kwamba ameihifadhi ndani na kwa vile uhakiki wa silaha kunahitajika na silaha yenyewe hakuwa na budi kuibeba na kuipeleka.
 
Hii hata kama sifa imezidi.SIjawahi kuona toka enzi za JKN mpaka Kikwete,Rais kuwa na silaha.Walinzi wote wale ikulu.Au yuko first kutumia kuliko walinzi wake??Imenipa shida,nadhani hata walinzi wake itakuwa imewapa shida kumuelewa.
Hukuona hayo kwa sabab kipindi hicho wakuu wa mikoa hawakuwa kutoa agizo kama la Makonda. Na ukumbuke miezi 6 ilopita alikwua ni waziri tu kumiliki silaha ni kawaida, na katika uhakiki ni lazima aibebe haikuwa na jinsi na baada ya hapo anazifungia kabatini mpaka baada ya miaka 5 au 10 akiondoka madarakani.
 
JUZI Rais John Magufuli alikuwa mtu wa kwanza kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuhakiki silaha, ambapo bunduki zake mbili aina ya shotgun na bastola zimehakikiwa Ikulu, Dar es Salaam.

Uhakiki huo uliogeuka gumzo na jana picha zake zipamba vyombo vya habari nchini, ulifanywa na maofisa wa Jeshi la Polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa uhakiki huo, Rais Magufuli alimpongeza Makonda na Jeshi la Polisi kwa kuendesha kampeni ya uhakiki wa silaha, huku akitoa mwito kwa watu wote wanaomiliki silaha nchi nzima kuhakikisha zinahakikiwa.

Aidha, Rais Magufuli pia ametaka Jeshi la Polisi kuongeza juhudi za kukabiliana na watu wanaojihusisha na uhalifu ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo. Rais Magufuli pia alielezea kushangazwa na vitendo vya askari kunyang’anywa silaha na majambazi, huku mara kadhaa akirudia kusema ‘Ni aibu’.

Alisisitiza lazima wabadilike na kukabili kwa vitendo uhalifu., Tunampongeza Rais Magufuli kwa kuunga mkono kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ya kuhakikisha kila anayemiliki silaha anaimiliki kihalali.

Kama ambavyo Makonda alieleza wakati akitangaza mpango huo, dhamira ni kuhakikisha vitendo vya uhalifu vinavyotokana na matumizi ya silaha haramu katika Jiji la Dar es Salaam, vinatokomezwa na hatimaye Jiji linakuwa salama kwa raia na mali zao kama ilivyo asili ya jina la Dar es Salaam, yaani Bandari ya Salama.

Hivyo kwa kuwa Rais ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu ameonesha kwa vitendo kuunga mkono utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ni vyema wengine watumie miezi mitatu iliyotolewa na Mkoa kuhakiki silaha zao.

Hatua hii ikifanikiwa, itachangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa matukio ya kihalifu yanayoonekana kuota mizizi kiasi cha majambazi kuvamia popote wanapotaka, hata vituo vya Polisi na kusababisha hofu kuu kwa wananchi.

Ni dhahiri wananchi hujikuta wakikosa majibu na kujiuliza kama Polisi wanavamiwa na kuuawa, hali itakuwaje kwa raia wa kawaida ambao kwa kiasi kikubwa hutegemea ulinzi wa Polisi? Ifike mahali kila mkazi wa Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla, washiriki kikamilifu katika kampeni hii yenye lengo la kudhibiti silaha holela mitaani.

Udhibiti wa silaha una maana kubwa sana kwetu, kwani ni dhahiri matukio ya kihalifu yatapungua na kufanya wananchi wawe huru katika shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo.

Kwa kutambua umuhimu wa utulivu, amani na usalama, tunaamini juhudi za Makonda na Jeshi la Polisi za kutaka kuiona Dar es Salaam isiyo na uhalifu, zikiungwa mkono kama alivyoonesha Rais Magufuli, hakuna kitakachoshindikana.
 
Alichokifanya rais baada ya kuhakiki silaha kimezua maneno mengi lakini kuna ujumbe mmoja watu wanashindwa kuuelewa. Mkurugenzi wa shirika moja akipewa let's say msaada wa magari 40 na kampuni kubwa nchini, huwa anaingia ndani ya gari na kupozi kama vile anaendesha mojawapo ya yale magarini ni gesture inayoonyesha kupokea kwa dhati kile ambacho kampuni inakuwa imekipokea (msaada wa magari).

Juzi juzi mtoto wa rais wa awamu ya nne kakabidhiwa ambulance kwa ajili ya wagonjwa wa jimbo la chalinze, alichokifanya ni kuzunguka nalo mle mle ikulu kama gesture ya kulipokea lile gari. Rais baada ya kuihakiki silaha akaamua kutumia usanii fulani ambao kwa kweli ni usanii unaofanywa na wengi tu kwenye matukio mengi maalum, akafanya alichofanya baada ya kuhakiki ahalafu akaiweka sehemu ambayo inatakiwa silaha iwekwe, ni gesture inayoendana na tukio la kuhakiki bunduki.

Haya ni mambo yanayofanyika ulimwenguni kote, kiongozi au mhusika wa tukio fulani anaamua kufanya usanii mdogo unaokubalika, usanii ambao unaendana na tukio husika (playful gestures).
 
Simjui Magufuli,ninamfahamu tu kwamba ndiyo Rais ,na kabla ya hapo nilikuwa namfahamu tu kama Waziri wa Barabara,mengine ni Maisha yake sina tabia ya kuyafuatilia maisha ya wanasiasa wala ya binadamu mwingine.

Hongera kwa kumjua:confused::confused::confused:

Wapo wanaomjua Magufuli kwa mambo mengine, Ila kwa Uwaziri na Urais wake mengi yako wazi
 
Unauhakika yuko fast kuliko wanaomlinda.Hiyo tu.
Haaaaa kumbuka alipitaga JKT na ujue kuwa mtu anavyokuwa rais anafundishwa self-defense ni kama course maalum kwa rais hili ikitokea tatizo lolote yeye mwenyewe anaweza kujiokoa,so linawezekana pia akawa yupo fast kuliko walinzi wake
 
Haaaaa kumbuka alipitaga JKT na ujue kuwa mtu anavyokuwa rais anafundishwa self-defense ni kama course maalum kwa rais hili ikitokea tatizo lolote yeye mwenyewe anaweza kujiokoa,so linawezekana pia akawa yupo fast kuliko walinzi wake

Kwa JKT unafundishwa kujenga shabaha tu.Hiyo ya kuwa fast kuliko mlinzi kwa course ya muda mfupi sina uhakika.Mlinzi Ana miaka mingi kwenye field hiyo.Anyway tusiyatafute tusije ambiwa tunataka kuua Presida
 
Habari Wakuu,

Kweli tunaona kila kiongozi hasa nafasi ya Rais huwa ina ulinzi kwa ajili ya usalama wake.

Hivi ikitokea walinzi wake wamezidiwa labda katika shambulio fulani dakika ya mwisho Rais atakuwa na silaha yake kwa ajili ya kujitetea au ana self defense yoyote yaani michezo hatari ya kujilinda mwenyewe binafsi au ndio atabakia kuomba msamaha hata Kama wavamizi wako mikono mitupu?
 
Back
Top Bottom