Rais Magufuli atarajiwa kuzindua Mahakama zinazotembea (Mobile Court), Februari 06, 2019

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli (Kesho February 6) anatarajia kuzindua Mahakama zinazotembea (Mobile Court) Jijini Dar es Salaam ikiwa ni mpango mkakati wa Mahakama wa kumaliza mlundikano wa kesi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri wa Mahakama ya Tanzania, Eva Nkya uzinduzi huo utafanyika katika sherehe za siku ya Sheria kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Mpango huo wa Makahama zinazotembea umekuja kufuatia maombi ya Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma kwa Rais Ikulu January 29 mwaka huu Jijini Dar Es Salaam wakati akiwaapisha Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ombi lililohusu kuimarisha miundombinu ya Mahakama,kuongeza Mahakama zinazotembea (Mobile Court) na kuongeza rasilimali Watu.

Akizungumza katika hafla ya kuwaapisha viongozi hao Ikulu Jijini Dar es Salaam ,Rais Magufuli alisema wazo la kuwa na Mahakama hizo zinazotembea ni wazo jema na la ubunifu katika kushughulikia kero za wananchi hususan katika upatikanaji wa haki.

Mpaka sasa nchini Tanzania tuna mahakama za Mwanzo 960, kata zaidi ya elfu 3 ambazo hazina mahakama, serikali imeona si vyema kukaa kusubili majengo ya mahakama mpaka kujengwa kwa kipindi kirefu, hivyo kuanzishwa kwa magari haya yatakuwa mkombozi kwa wananchi waishio katika kata zisizo kuwa na mahakama.

Dhana ya mahakama zinazotembea ni mahususi kwa kuwapunguzia gharama wananchi wa tanzana,kuwapunguzia muda wa kwenda mahakamani, kuwapa uhuru wa kuweza kufanya shughuli zao na kuwapa elimu wananchi juu ya haki zao za msingi katika mahakama.

Mpaka sasa serikali imeshanunua magari mawili yenye uwezo wa kusikiliza mashauri ya wananchi kwa aslimia 100, na kwa awamu hii ya kwanza wameanza na Mahakama ya mwanzo na Mahakama ya Wilaya hivyo kadri siku zitakavyozidi serikali inatalajiwa kuongeza magari mengine kutokana na mwamko wa wananchi.

Magari hayo ya Mahakama zinazotembea zinatarajia kuanza katika mkoa wa Dar es Salaam na Mwanza hii yote kutokana na wingi wa mashauli, uchache wa mahakama na idadi ya watu hasa waishio Dar es Salaam katika maeneo mbalimbali katikaikoa tajwa .

Mbali na kusikiliza kesi, mahakama hizi zinatoa elimu kwa umma na kuelimisha wananchi juu ya kupata huduma za mahakama, kufanya usuluishi kwa jamii na kuhusika kwenye oparesheni maalumu za kiusalama endapo zikitokea.
 
Amekosa cha kuzindua, maana mwaka jana siku ya sheria alizindua hizo mobile Court. Halafu mkumbusheni wengi hatujapata vitambulisho vya taifa. Na kwenye viwanda mwambieni tunangoja azindue vile viwanda vyake 3,000+ alivyosema viko Pwani, vile alivyozindua vilikuwa vya JK.
 
Kati ya watu 1,723 waliofungwa ni 158 tu ndio waliofungwa kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama.
Watu wanafungwa jela miaka bila ushahidi wowote na bila dhamana.
Huu udhaifu wa mahakama zetu kushindwa kutenda haki utasaidiwa vipi na hizi mobile court??
 
Mpaka sasa serikali imeshanunua magari mawili yenye uwezo wa kusikiliza mashauri ya wananchi kwa aslimia 100, na kwa awamu hii ya kwanza wameanza na Mahakama ya mwanzo na Mahakama ya Wilaya hivyo kadri siku zitakavyozidi serikali inatalajiwa kuongeza magari mengine kutokana na mwamko wa wananchi.

Gharama ya posho ya dereva, makarani, hakimu mafuta, vipuri nk kuzunguka nchi nzima ikifanyiwa hesabu vizuri si inaweza kuelekezwa kwenye ujenzi wa mahakama za kudumu!
 
Hahaha Hapa mnamsifu bila kujua, lakini hazitafanya kazi. WHO waliishawahi kuipa serikali Mobile clinics na Laboratory hazikufanya kazi kabisa, hivyo hata hizi itakuwa hivyo hivyo, hakuna hakimu a judge atakaa humo kuendesha kesi.
Bora kujenga mahakama kila kijiji kuliko hizi. Kesi zinazosomwa na kuahirishwa zitapata hukumu baada ya miaka 10 nadhani.
 
sio kama unavyofikiri hii ni awamu ya tano ndugu
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom