Rais Magufuli atapokea ripoti ya mchanga wa madini leo Ikulu, Redio na TV kurusha LIVE!

Wadau,
Muda huu Kama dakika tano zilizopita TBC wameleta habari mpasuko (breaking news) kuwa kesho rais Magufuli atapokea report ya tume aliyoiunda kuchunguza mchanga wa dhahabu. Hivi hii nayo ni habari mpasuko? Tukio ambalo bado halijatokea wanaliita habari mpasuko.
Hahaha...hivi TBC kwanini lakini? dah
 
Wamechelewa naskia acacia ndo wanafunga mgodi 2019 wanatuachia shimo. [HASHTAG]#CCM[/HASHTAG] NI JIPU KUU
 
18620065_10211493863415260_2789757105371520368_n.jpg
Siku akipokea na report ya nape ya uvamizi wa clouds atuambie tumsikilize
 
Muda huo si mlituambia watanzania tuchape kazi na mpaka bunge mkalizima ili tu tuchape kazi??

Hivi mbona JK hakuwa na upuuzi kama huo?
nyie ndio maajabu ya wa tz. yaani unaona huo ni upuuzi. ulitaka iwe kimyakimya au sio? kusudi uweze kuzua uongo.
 
nyie ndio maajabu ya wa tz. yaani unaona huo ni upuuzi. ulitaka iwe kimyakimya au sio? kusudi uweze kuzua uongo.
Kwani hata wakipiga porojo zao kesho tutapata nini?? Mlianza kupiga porojo bandari ufanisi huko umeendelea? Mizigo imeongezeka huko kuliko kipindi cha JK? Mkatupigia porojo na pesa zenu kwenye mabenki ya biashara sasahivi Private sector iko mahututi.. Endeleeni na porojo na upuuzi wenu hakuna kitakachobadilika..
 
Wengine muda huò tutkuwà tunatekeleza hapa kazi tuu. Magazeti, TV , mitandao jamii, na redio tujulisheni jioni
 
Ripoti hii yaweza kuanzisha ukurasa mpya wa mikataba ya uchimbaji.
Kama nadharia zitakuwa nyingi kuliko uwezekano wa kutenda kwa ufanisi, sekta ya madini itarudi nyuma kimaendeleo, kinyume chake faida ya madini itaonekana.
 
Mbona bunge halioneshwi live?


Tume huru idaiwe mapema Tanzania ccm itoke vinginevyo watanzania mtapata tabu sana.
 
Back
Top Bottom