Rais Magufuli ataka wauaji Pwani waokoke

Masamila07

JF-Expert Member
Jun 22, 2014
4,841
2,000
pic+JPM.jpg


Rais John Magufuli amewataka wananchi kuwaombea wanaofanya mauaji katika wilaya za Kibiti na Rufiji ili waokoke na kutambua kuwa damu ya mtu ina thamani kubwa.

Pia amevitaka vyombo vya dola vifanye kazi yake kwa kuwashirikisha wananchi ili kufanikisha kazi ya kukomesha mauaji hayo mkoani Pwani.

Rais Magufuli ametoa wito huo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Kibaha katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani na ya kwanza katika mkoa huo tangu achaguliwe kuwa Rais.

Rais, pia alikataa kupokea kadi ya mwanachama wa ACT-Wazalendo aliyeamua kujiunga na CCM, akisema ziara yake ni ya kiserikali na hivyo kumuita katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho tawala, Humphrey Polepole kufanya kazi hiyo.

Badala yake, Rais alitoa fursa kwa viongozi wengine wa vyama vya siasa kutumia mkutano huo kupokea wanachama wapya, lakini hawakutokea.

Mpaka sasa tayari takriban watu 39, wakiwamo viongozi na askari wa Jeshi la Polisi, wameuawa katika wilaya za Rufiji, Kibiti na Mkuranga kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti hili limezikusanya kuanzia Mei mwaka jana.

“Huko ambako viwanda havipo mnajua ni kwa sababu gani. Nani wa kwenda kuwekeza wakati watu wanauana, nani atakwenda kuwekeza huko?” alihoji Magufuli.

“Lakini nataka niwaambie Serikali ya Awamu ya Tano si ya kuchezewa. Moto wameshaanza kuupata, ninasema moto wameshaanza kuupata. Waache, walikuwa wachache tu na watanyooka,” alisema.

“Na ninaposema watanyoka ‘actually’ wameshaanza kunyooka. Kama kuna baadhi yao wananisikiliza, wapeleke salamu huko kwamba hawatapita.”

Aliwataka wakazi wa Pwani kuacha kushirikiana na wahalifu hao kwa sababu hao ndicho chanzo cha kuchelewesha maendeleo.

“Hakuna imani yoyote ya dini inayosema watu wauane. Dola na vyombo vya ulinzi vitafanikiwa kama vitapata ushirikiano kutoka kwa wananchi. Niwaombe wananchi mtoe ushirikiano kwa vyombo hivi ili wahalifu hao wachache waache na washughulikiwe kikamilifu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa,” alisema Magufuli.

Kadhalika, Rais alitumia mkutano huo kuwaeleza wakazi wa Pwani kuwa hakwenda mkoani humo kuzungumzia CCM, bali maendeleo na kuangalia shida walizonazo wananchi.

“Sikuja kuizungumzia CCM, nimekuja kuizungumzia Tanzania. Shida walizonazo CCM, ni shida anazozipata mwana ACT, na hata asiye na chama, shida ya Watanzania si chama, bali ni shida zetu,” alisema.

Alisema ni lazima wachache waumie ili wengi wafaidike na wengi watakaofaidika ni Watanzania.

Rais alisema atakuwa upande wa wananchi wanyonge na hivyo kuomba aombewe ili azifanyie kazi changamoto hizo.

Kuhusu maendeleo mkoani Pwani, Rais Magufuli alisema itajengwa bandari kavu eneo la Ruvu, ambayo mizigo inayotoka nchi jirani itapitishwa.

“Ni fursa kubwa kwa wakazi wa Ruvu, Pwani. Tunafanya hivi kwa niaba yenu,” alisema.

Pamoja na maji, Rais alisema pia itajengwa barabara ya kisasa itakayotoka Dar es Salaam, kwenda Chalinze ambayo itakuwa na barabara za juu na njia sita.

Ahadi nyingine za maendeleo alizozitaja Rais ni pamoja na mradi wa umeme utakaogharimu Sh30 bilioni na mradi wa maji wa Ruvu Juu uliofadhiliwa na Serikali ya India, ambao maji yake yatatumika jijini Dar es Salaam, Kibaha na Bagamoyo.

Kingine ni ujenzi wa bwawa la Kidunda linalohifadhi maji ya mvua ili kukabiliana na upungufu wa maji nyakati za ukame.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alisoma taarifa ya mkoa kuhusu utekelezaji wa mpango wa Tanzania ya viwanda, inayoonyesha kuna viwanda 371, kati yake vikubwa na vya kati ni 89.

Vingozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni Polepole na mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpta Mshama.

Chanzo: Mwananchi Online
 

SDG

JF-Expert Member
Feb 28, 2017
7,652
2,000
Hadi wamefika watu 39 still wanaambiwa wajiangalie
 

brenda18

JF-Expert Member
Sep 17, 2013
5,651
2,000
ni kheri asingeongelea kuhusu kibiti, nna wasiwasi ni kama mauwaji yatazidi ili kumjibu alichokiongea hapo
 

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
15,655
2,000
The best part ya taarifa hii ni Rais kukataa kupokea kadi za wanasiasa wanaotaka kurudi CCM ....kachora mstari wa ziara ya kiserikali na kisiasa ...pia kutoa fursa za viongozi wa vyama vingine kupokea kadi za wanaotaka kuhamia huko ni very fair ....hizi issue ziwe Kikatiba na tuwe na utaratibu wa kuwajibishana anayekiuka ....otherwise Katiba itageuka pambo kama Kenya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom